Uchaguzi Mkuu 2015: Mkakati uwe ni kuongeza idadi ya wabunge CHADEMA na siyo kupata Rais wa CHADEMA

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Waungwana wanaJF, naomba nioneshe msimamo wangu kuwa mimi ni CHADEMA damudamu, lakini kuna mambo mawili nataka niwashirikishe.

1. Wakati naangalia kipindi cha Bunge Juzi jioni niliona namna wabunge wetu wa CHADEMA wanavyopata taabu kupitisha hoja kutokana na uchache wao bungeni. Wana CCM, wabunge wanapitisha maamuzi kwa kusema NDIYOOOOOOOOOOOOOOOOOOO kubwa lakini za kinafiki huku hata waliolala huamshwa na kusema NDIYOOOOO!! Huu ni upuuzi. Lazima tuwe na idadi kubwa bungeni ili waseme NDIYOOOOOOOOOO na kushinda CCM.

2. Kutokuwepo nia ya dhati ya serikali kutoa fursa kwa vyama vya upinzani kuwa na demokrasia ya kweli katika shughuli za wanasiasa za ndani na nje ya bunge. Wabunge wetu wanadhalilishwa kwa kupindisha sheria za nchi. Idadi kubwa ya wabunge itaifanya serikali kukubaliana na maamuzi yao maana ndio watakuwa na sauti kubwa bungeni.

WanaJF, mnasemaje hapo?? Naomba michango yenu kwa kuzingatia hali halisi inavyoendelea Bungeni.
 
Ushauri wako unamapungufu ondoa.uCHAGUZI MKUU UNAHUSISHA Rais , wabunge na Ma-diwani.Hapa unacholeta ni utani hujatoa ushauri
 
mzee yani ujakosea kuingiza wabunge wengi wa upinzani na namba ikawa balance or atleast inakaribia kubalance bungeni kutakuwa hakuna mambo ya kipuuzi katika hoja za msingi ambazo zinaitaji maelezo ya kina na sio blaa blaa ilimradi siku ipite kama inavyofanyika sasa kwamba ikifika katika swala la issue ya msingi kupigiwa kura upinzani unapata tabu kwasababu ya namba ya chama cha magamba
 
Mimi natofautiana kidogo na wewe!dawa ni kuuondoa kabisa utawala wa CCM!(overhauling the whole system)!!
 
Mkakati ni wa kuchukua dola sambamba na kuongeza wabunge madiwani na wenyeviti wa vijiji
 
Nawashukuru wanachi watz kwa kuwa na imani na cdm,hiyo ndiyooooooooooo!!!!!!!!! ni ya mwisho mwisho, mkuu ccm inadondoka amini usiamini 2015,
 
Waungwana wanaJF, naomba nioneshe msimamo wangu kuwa mimi ni CHADEMA damudamu, lakini kuna mambo mawili nataka niwashirikishe.1. Wakati naangalia kipindi cha Bunge Juzi jioni niliona namna wabunge wetu wa CHADEMA wanavyopata taabu kupitisha hoja kutokana na uchache wao bungeni. Wana CCM, wabunge wanapitisha maamuzi kwa kusema NDIYOOOOOOOOOOOOOOOOOOO kubwa lakini za kinafiki huku hata waliolala huamshwa na kusema NDIYOOOOO!! Huu ni upuuzi. Lazima tuwe na idadi kubwa bungeni ili waseme NDIYOOOOOOOOOO na kushinda CCM.2. Kutokuwepo nia ya dhati ya serikali kutoa fursa kwa vyama vya upinzani kuwa na demokrasia ya kweli katika shughuli za wanasiasa za ndani na nje ya bunge. Wabunge wetu wanadhalilishwa kwa kupindisha sheria za nchi. Idadi kubwa ya wabunge itaifanya serikali kukubaliana na maamuzi yao maana ndio watakuwa na sauti kubwa bungeni. WanaJF, mnasemaje hapo?? Naomba michango yenu kwa kuzingatia hali halisi inavyoendelea Bungeni.
I can't agree with you more... CDM wanachotakiwa kufanya sasa ni intelligensia ya kuidentify potential candidate na kuwagroom. Infact kutoa elimu husika ili watu wenye uwezo wajitokeze. Issue siyo kuwa na raisi toka CDM au chama chochote cha upinzani. Ktk mfumo wetu tunaona mbali na kuwa raisi ni executive kimaandishi.. Ukweli ni kwamba he is more of a symbol. Kinachotakiwa kufanya ni kubadili sheria nyingi tu na zoezi hilo hufanyika ndani ya bunge. Imaagine unakuwa na premier hajui hata wajibu wake kama kiranja ... Nchi inakuwa gizani hakuna serious actions zinachukuliwa wakati kuna Raisi PM na wabunge wanaosifia bajeti ambao hawako objective kutokana na mfumo ulipo etc. Watu wanaopashwa kusimamia serikali wanaelekezwa au wanaagizwa na chama tawala kutetea bajeti ya serikali.
 
Nchi inahitaji mabadiliko ya kisiasa na hakuna mabadiliko iwapo utashindwa kukiondoa chama kilichokosa mwelekeo madarakani. Hapa tulipofika tunahitaji uongozi mpya sio viraka vya hapa na pale wakati biashara inaendelea kama kawa....Jamani wana Jamiiforums hivi mchakato wa katiba unaendelea kweli? naona kama vile mambo yamesimama maana bila Katiba Mpya itakayotupa tume huru ya uchaguzi tutakua(watanzania) tunatwanga maji kwenye kinu.
 
Tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa 2015. CCM inatosha kwa yote mema na mabaya waliyotutendea. Tunataka chama kingine kishike dola.
 
Nadhan mawazo yako sio mabaya. Ni kweli hiyo inaweza ikawa ni mkakati mzuri tu wa kuikomboa nchi hii.

Kwa upande wangu nafikiria kuwa uwezekano wa CDM kushinda urais wa nchi hii ni mkubwa sana. Angalia matokeo ya uchaguzi uliopita. Pamoja na matatizo yote ya mfumo wa uchaguzi lakini kura za kutosha zilipatikana. Matumizi ya usalama wa taifa katika kuchakachua matokeo na tume ya uchaguzi ya chama tawala tukiweka machache.

Sasa kwa mwendo huu wa uendeshaji nchi unaofanywa na chama tawala naona wanakabidhi nchi mikononi mwa CDM wenyewe. Kikubwa ni kuweka mikakati ya kutosha na ninaamini kabisa CDM ina watu makini wanaoweza kupanga mipango hiyo.

Inawezekana kabisa kuongeza idadi ya wabunge na pia kushinda urais kwani hawa watawala wameshachoka kabisa.
 
Nadhan mawazo yako sio mabaya. Ni kweli hiyo inaweza ikawa ni mkakati mzuri tu wa kuikomboa nchi hii.

Kwa upande wangu nafikiria kuwa uwezekano wa CDM kushinda urais wa nchi hii ni mkubwa sana. Angalia matokeo ya uchaguzi uliopita. Pamoja na matatizo yote ya mfumo wa uchaguzi lakini kura za kutosha zilipatikana. Matumizi ya usalama wa taifa katika kuchakachua matokeo na tume ya uchaguzi ya chama tawala tukiweka machache.

Sasa kwa mwendo huu wa uendeshaji nchi unaofanywa na chama tawala naona wanakabidhi nchi mikononi mwa CDM wenyewe. Kikubwa ni kuweka mikakati ya kutosha na ninaamini kabisa CDM ina watu makini wanaoweza kupanga mipango hiyo.

Inawezekana kabisa kuongeza idadi ya wabunge na pia kushinda urais kwani hawa watawala wameshachoka kabisa.
Wapenda mageuzi tutakuwa tunakosea sana kama nguvu zetu tutakuwa tunazielekeza kwenye uchaguzi tu. Mimi nafikiri kabla ya kuota kushinda uchaguzi, nguvu zielekezwe kwenye katiba nzuri itakayotoa nafasi kwa tume huru ya uchaguzi. Vinginevyo tutaendelea kulia mwaka hadi mwaka na ccm itaendelea kupora uchaguzi. Kabla ya uchaguzi wa 2010 watu hapa JF walikuwa wanasema ngoja uchaguzi ufike, ukafika na hamna lolote lililotokea. Na hiyo 2015 itakuwa hivyo hivyo. ccm inatumia mbinu ya kuwaachia wabunge wachache wa upinzani wapite lakini wanahakikisha wengi waliopita ni ccm. Watanzania tuamke tusiseme tu subiri uchaguzi ufike ndio tufanye mabadiliko, mabadiliko yahitajika sasa na ikiwezekana leo hii hii..
 
hapa dawa ni kuongeza wabunge wa chadema na Kumpata RAIS pia wa CHADEMA kwani ndo wenye uchungu na inji hii.Hapo vipi?
 
Mkakati unatakiwa uwe kupiga kotekote unapoongelea uwe kushinda Ubunge inamaana hujui contribution ya Kura za Urais katika kuongeza hiyo idadi ya Wabunge unayoisema.
 
Kote kote,rais,wabunge,madiwani,wenyeviti wa mitaa,mabalozi wa shina,familia,mtu moja moja,watoto,vijana,kina mama,kina baba,wazee na tanzania yote
 
Back
Top Bottom