Uchaguzi Mkuu 2010 Zanzibar: Hatima ya Demokrasia na Upinzani Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Mkuu 2010 Zanzibar: Hatima ya Demokrasia na Upinzani Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rev. Kishoka, Jun 21, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nikimuangalia Mousavi na vijana wake wanavyoandamana kupinga ushindi wa Ahmedimjinga, nikinusa harufu ya damu na hamasa za kutokuogopa dola kwa jina la Demokrasia na Upinzani wa kisasa kunakotokea Iran, nakuja na jibu moja kuhusu hatima ya Demokrasia Tanzania, uhai na muelekeo wa vyama vya Upinzani Tanzania: Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2010!

  Ningekuwa mimi Chadema, TLP, NCCR na wengine wote wasioitwa CUF au CCM, ningewekeza nguvu zangu za kichama kuleta msukumo wa mapinduzi ya kweli ya kisiasa na Demokrasia Tanzania kupitia Zanzibar.

  Funzo la Uchaguzi 1995, 2000 na 2005 linatosha kuonyesha wazi ni vipi Zanzibr ina nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko ya kweli kisiasa Tanzania na hata ile dhana ya kuing'oa CCM madarakani inawezekana na ndoto kutimilika.

  Si urongo (sic) kuwa chaguzi zote hizo tatu 1995, 2000 na 2005, CCM ilishindwa vibaya na hasa kwenye Urais, lakini Utamu wa Hatamu ulifanya wagombea wa CCM watoke videdea huku maelfu ya Wazanzibari waliokuwa ni upande wa Upinzani ama kupoteza maisha au kufanywa wakimbizi kutoka nchi yao.

  Ni Wazanzibari pekee, iwe ni wa kutoka Pemba au Ungujam ndio walio na kende imara kuandamana na hata kutoa damu kupigania haki zao na kulilia kilicho chao.

  Ingawa tunawadharau na kuwaona kuwa ni sawa na mke kwenye suala la Muungano, lakini nawavulia kofia kwa ujasiri wao wa kupigania kilicho chao na mtaona kwa dhati ni vipi hata ndani ya CCM, kundi la Zanzibar huwa na nguvu za ajabu licha ya vitisho vya rungu la Kichama au Dola ya Serikali ya Muungano.

  Swali linakuja kwa Upinzani, ni vipi basi mnalazia damu kuiteka Zanzibar yote kwanza na kuicha CCM kama si Solemba bali chali mithili ya kifo cha mende?

  Kinachotokea Iran kinanipa jawabu moja kubwa, nalo ni kwa upinzani kuwekeza nguvu zao zote wakati wa uchaguzi mkuu wa Taifa 2010 Zanzibar.

  Iwe ni Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Rais wa Zanzibar na hata Wabunge wa Bunge la Muungano, Upinzani nguvu zao za kujijenga na kukubalika kisiasa machoni pa Watanzania wengi kutatokana na turufu ya kuishikilia Zanzibar!

  Mwaweza sema Mchungaji kalewa mvinyo, lakini jiulizeni ni kwa nini Mkapa alimpeleka Omar Mahita na vikosi vya Dola kule Pemba na Unguja kutuliza rabsha? Jiulizeni ni vipi mwaka 1995, ilibidi Salmin Amour asalimishe kende zake kwa Nyerere akiomba msaada?

  Jibu laki ni kuwa CCM ilipoteza Urais na Uwakilishi Zanzibar katika chaguzi zote hizo mbili!
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Heshima Mbele Mkuu,
  Tatizo moja tu ndiyo mpaka leo CCM ipo madarakani zanzibar,hofu ya dola ya jamhuri ya muungano wa tanzania,inalazimisha ima faima lazima CCM ibaki madarakani,wazanzibar wakiipenda wasiipende.
  Na hofu yao ni kuwa once CCM imekwenda zanzibar na ndugu zetu wa bara hawatakuwa na haja nayo tena, nako muda si muda itaishia kama UNIP ya Kaunda kule Zambia na KANU ya Moi kule Kenya.
  Mabadiliko yakianzia zanzibar, bara haitokuwa salama nako yataikumba tu, na hili wakubwa wakilifikira linawakosesha usingizi.
  Kwasababu hiyo ndo maana Rais Mkapa alikhiyari kuuwa na kumwaga damu za wazanzibar wasiokuwa na hatia, kwa sababu tu ya kuinusuru CCM na baadhi ya vibaraka wake zanzibar.
  Dola ndiyo inayoirudisha nyuma zanzibar na ndiyo inayonyang'anya matakwa na ridhaa za wazanzibar.
  Time will come we will see dawan.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Junius,

  This time, there will never be a Mkapa trick on any body in Zanzibar. CCM will never be able to pull magic trick to maintain leadership and govern Zanzibar!
   
 4. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  .
  Ujasiri huo huo ndio utakao mtoa bibi ZANZINBAR Katika ndoa ya lazima zidi ya bwana TANGANYIKA
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Call me mchochezi, but this could be face of Zanzibar November 2010!

  [​IMG]
   
 6. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha kusema uwongo wewe.Wazanzibari gani hao unawaafanyia reference wewe. Twende kisanduku cha kura.
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Sifikiri hiyo itatokea.Ila mimi ninachoona ni kuwa Wapinzani watapata Rais na huku bara tuanze kuandaa kabisa namna ya kuita jina nchi yetu sijui itabaki TANGANYIKA ama TANZANIA BARA
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Narejea makala ya kaka yangu Mzee Mwanakijiji juu ya utabiri wa kisiasa wa Tanzania na hali ya Kisiasa ya Iran, maana kuna kila dalili kama zile kuja kwetu na Tanzania wale watu ambao wanaitwa wafaidhina na Ndio hao leo utawakuta Zanzibar. Maana kuna Watu ambao ni maconservatives sana , then Kizazi cha sasa hakijui kabisa kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Kuna haja ya utawala wetu kujifunza toka huko Iran
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi unajua kuwa wapo Wazanzibari ambao wanataka CCM iende ili wairejesha ASP yao?
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Sijakuelewa vizuri.
  Nawazungumzia wazanzibar waliopiga kura mwaka 1995, 2000 na 2005, ambao matakwa na maamuzi yao hayakuwa lolote wala chochote zidi ya yale ya dola, kadhalika nawazungumzia wazanzibar waliouwawa Jan 26/27 kwa sababu tu ya kutekeleza haki yao ya msingi ya kidemokarasi ya kuandamana.
  Siku zote nakuambia Pakacha,pindipo only pindipo(ww unalifahamu vyema neno hili 'pindipo') zanzibar ikifanya uchaguzi huru na haki, CCM itakuwa historia, kubali au kataa lkn huu ndo ukweli.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwanza nikwambie tu kuwa kitu ASP zanzibar ni kama "kivuli kinachoishi", zanzibar inaongozwa na kivuli hicho na kinalindwa na CCM, ukisikia habari za 'huyu mwenzetu na yule si mwenzetu usifikiri CCM!!! hapo anatazamwa je alipitia kisiwanduwi huyu. Nikupe mfano kila siku napenda kuurejea nikisisitiza nukta hii, Dr. Salim Ahmed Salim aliletewa kauzibe ya UHIZBU wakati akitafuta tiketi ya kuteuliwa kugombea urais wa muungano, kwa "kivuli" kilekile cha "kwani mwenzetu huyu?"
  Kwa taarifa yako ASP inaishi na mkitaka kuona kituko mngemlazimisha Karume aunde serikali ya Mseto mkaona unyago wa kima.
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni vigumu kumkuta mtoto wa kizanzibar aliyefika walau darasa la saba kama mm kuwa haijuwi historia ya Mapinduzi "matukufu ya 1964".
  Tatizo lililokuwapo ni kuwa wengi wao hawajuwi upande wa pili wa historia hiyo, wengi wao hawajuwi kuwa Mapinduzi hayo hayajafanywa na ASP kama inavyodaiwa, wala Mzee Karume hakuwahi kupanga, kuongoza wala kushiriki mapinduzi hayo.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ndicho ninachosema kuwa kwao CCM ni kama kivuli tu cha kulinda chama chao halisi, hivyo wala hawana hofu ya ccm kuondoka kwa sababu wanajua wanacho chama chao halisi ambacho ndicho kimsingi kinachoendesha mambo yao
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mpita Njia,

  Je mwenye mali ni nani?
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu saafi sana na kwa kuongezea tu hakuna mtu ndani ya hilo Baraza wanajiita Baraza la Mapinduzi au ASP kwa ujumla wake aliyeshiriki, kuandaa wala kuongoza Mapinduzi... lakini waone wanavyodai nchi kuwa yao..
   
 16. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Tulishayashuhudia 1995, 2000, na 2001. Kwa hiyo hapatakuwa na jipya ila ni mwendelezo ule ule. Iran ndiyo wamejifunza kwa Zanzibar. Ushauri wako kuhusu vyama vya siasa kuitumia Zanzibar kama kitovu cha mageuzi ni mzuri, lakini umesahau kwamba hao wote unaowashauri ni "wanasiasa" na malengo yao ni tofauti na wanavyojinadi ... utakujagundua nia zao wakishaingia madarakani ... ndipo utabaki kustaajabu utakayokuwa unayaona wakati huo.
   
 17. mohammedzahor

  mohammedzahor Member

  #17
  Jun 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana kwanza nawapongeza kwa kuwa na akili yenye kuona upande mmoja tu wa shilingi, na pili nawapongeza kwa jitihada za kuitakia mabaya zanzibar, na la tatu kwa uwezo wenu maini wa kujikita juu ya zanzibar pekee na kwamba kama ni ukosefu wa haki na demokrasia uko zanzibar tu.
  Langu mimi kwenu ni ushauri kwamba zanzibar ilikuwepo kwa salama na amani na itaendelea kuwepo kwa salama na amani na kama lengo ni kujitahidi ili mwaka 2010 kuwe na fujo kama la iran au lile la 2000 hadi 2005, hilo naon kama mmechelewa mana kila mtu hasa wa zanzibar kama ni wa ccm au wa cuf tumechoshwa na tendo la umwagaji damu, na hasa ukizingatia sio viongozi wenyewe wala jamaa zao ndio wanaoshiriki na kumwaga damu au kupoteza maisha yao, hivyo tendo la kushabikia zanzibar kmwagwa damu huo hni ufinyu na ulimbukeni wa mawazo na insha allah kama lengo lenu ni kushabikia na kuhamasisha fujo mwaka 2010 halitatimia, sisi sote ni watanzania na hutupendi chama chochote kishinde kwa hila ,lakini hatupendi damu imwagike eti sababu ni kutafuta haki. Mana ukweli hata upinzani wanajua kama ni wizi wa kura kule pemba wanaiba kura nyingi kuliko hata ccm, ni nani asiyejua kwamba cuf wanapandikiza wapiga kura hewa mara nne zaidi ya wale wa ccm, ni nani asiyejua kwamba ukiwaona cuf wanalalamika ju ya tendo fulani basi wao ndio walio tenda. Waungwana jiangal;ieni nyimbo mbaya haimbiwi mtoto mchanga, kama hamu yenu ni damu basi nendeni mkamwage huko huko kwenu na zanzibar siyo sehemu ya majaribio na kwa kweli hili halitatokea kwa kisingizio cha demokrasia, na hatungependa mtu yoyote apoteze maisha kwa jambo la kipumbavu. Zanzibar itajitahidi kuendesha uchaguzi wa huru na wa haki na wala siyo tabia ya kuendeleza chuki na uhasama dhidi ya watu.
  Ccm ya leo siyo ya jana na kama mnaota na kutamani damu imwagwe ya wazanzibari basi mmechelewa , hatutaki mtu wetu hataa mmoja amwage damu kwa kisingizio cha demokrasia, tafuteni dua nyengine mupombe siyo ya umwagaji wadamu. Huo ni uhasidi na insha allah kila mwenye kuiombea zanzibar dua mbaya basi itamrudia mwenyewe.
  Tunapenda demolrasia, lakini tunaipenda zaidi zanzibar yetu. Mana zanzibar ni muhimu zaidi kuliko siasa na watu wake na maendeleo ni muhimu zaidi kuliko matashi na matarajio yenu ya kuifanya iwe ndio pilot area ya fujo au kung;oka kwa ccm. Ccm ni chama kama vilivyo vyama vyengine, ila tofauti kati ya vyama kila mtu anao muono wake na matarajio yake, msidhani wazanzibari wote au wapemba wote ni cuf au ccm, wengi wao hawana chama.
  Tafuteni jengine la kuiombea zanzibar siyo machafu kwa watu wake, umwagaji wa damu kwa zanzibar huo ni uchurio na insha allah hautfika watu wa zanzibar.
  Na wewe muhusika wa mtandao hili uiliangalie siyo vizuri watu kutumia nafasi hii kuhamasisha fujo na umwagaji wa damu kwa kisingizio cha demokrasia na uhuru wa habari. Huu ni ulimbukeni.
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Bwana Mohammed,

  CCM haijabadilika! Huko visiwani na hata makao makuu CCM haijabadilika hata hatua moja ya Kinyonga au Kiwavi.

  Siombei mabaya au kumwagika damu Zanzibar. nafikiri labda humfahamu vizuri Mchungaji.

  Zanzibar ni kitivo na kituo kikuu cha mabadiliko ya Siasa za Tanzania, tupende tusipende. Vuguvugu la kuleta mabadiliko haya Zanzibar, ndilo pekee litakalosaidia kwa Tanzania kuwa na madiliko ya kweli ya Siasa.

  Kama tukiruhusu uhaini uliofanyika 1995, 2000 na 2010 chini ya uongozi wa CCM kuendelea kutawala si kwa ridhaa ya wananchi bali ridhaa na matakwa ya CCM, kamwe hatutaweza kuwa na maendeleo ya kweli, itabakia ndoto kuhusu Uongozi Bora na Siasa Safi.
   
 19. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwanza sishangai unavyopwaga pwaga hapa kadiri ninavyokujuwa. Kada mkubwa wa CCM. Na kinachokuuma kuwa hapa imesemwa CCM ambayo haina umaarufu huo unaotaka tuamini inayo huko Unguja na Pemba(litmus Paper ni uchaguzi wa 1995...)
  Hafu nikuulize unipe ufafanuzi mzuuri, unaposema kuwa "..umwagaji damu kwa zanzibar huo ni uchuro na .....hautafikia watu wa zanzibar..." unakusudia tukueleweje hapa?
  Si CCM iliyoamuru mauaji ya raia wasiokuwa na hatia kule Pemba Jan 26/27?
  Si nyinyi mlioamuru upigwaji wa wananchi wasiona hatia Darajani pale, na kuuzingira mtaa mzima wa Mtendeni kwa mabomu ya machozi na rabsha zidi ya wananchi wasiokuwa na hatia yoyete?
  Nani mwengine kama si CCM&SMZ na nyinyi vibaraka wake wanaoisogeza zanzibar katika machafuko ya na umwagaji damu?
  Yale makundi mliyoyaanzisha ya vijana wa "janjaweed" mkayaweka kambini kule Tunguu,mkayapa bangi na silaha za kienyeji kuhujumu wapinzani bila sababu ww unayaita nini, kama si kuelekea kuiletea machafuko zanzibar, nani anaiombea mabaya zanzibar kati ya wanaosema vuguvugu la mabadiliko ya demokarasia na nyinyi mnaotengeza mitandao ya hujuma na makundi ya kihuni ya kuhujumu wananchi kwa sababu ya tu ya itikadi zao?
  Nambie kama si CCM &SMZ waolitengeneza mtandao wa wizi wa kura maarufu "ajira kama" wa kukusanya vijana mkawapa ahadi za uwongo za kuwaajiri, mkawapeleka katika makambi ya JKU na Mafunzo kule Hanyegwamchana na Kama, mkiwatayaarisha kupiga kura mara mbili mbili , hujuma hizi zidi ya demokarasia zanzibar,zinaashiria nini huko mbele kama si machafuko?
  Kwa matendo yenu haya mbali na kuchezea tume ya uchaguzi na madudu kadhaa mnayoyafanya kuhujumu demokrsia zanzibar mnafikiri ndo mnaipeleka kuzuri zanzibar?
  Fikiria vizuri nani anaitakia mema zanzibar kati ya SMZ&CCM na wananchi wakawaida wapenda demokarasia zanzibar kwa matendo yenu hayo.
   
 20. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kweli zanzibar kazi itakuwepo 2010 tuombe dua
   
Loading...