Yaani huwezi amini. Zikiwa zimebaki siku 5 tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA bado hawajafahamika mpaka sasa.
Mimi nipo katika mkoa wa Dar es salaam. Na nimefuatilia kwa karibu sana zoezi hili la kuchagua wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Lakini nimeona kuna ujanja mkubwa unafanywa ili kuingiza wasimamizi ambao kwa namna moja au nyingine watapendelea chama tawala.
Ukienda kwa mkurugenzi wa manispaa iwe ya Temeke, Kinondoni hata Ilala. Ukaulizia majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura atakwambia , majina hayo yameshapelekwa katika Kata husika. Ukienda kwenye kata yako nao wanakwambia hatujaletewa bado hayo majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kutoka kwa mkurugenzi .
Lakini katika pita pita zangu mitaani nimepata taarifa kwamba tayari hayo majina yameshatoka na watu sasa hivi wapo kwenye semina za namna ya kusimamia vituo vya kupigia kura na namna ya kuiba kura.
Kama unabisha nenda sasa kwa ama mkurugenzi wa manispaaa husika au kwenye kata yako waulizie hayo majina wameyabandika wapi uone kama watakupa.
Huku viongozi wetu wa siasa wakiwa wamejikita katika kufanya kampeni tu, wakifikiri ndo watashinda , lakini hiyo ni kama kujaza maji kwenye tenga. Maana wenzenu chama tawala mwaka huu wa 2010 watatumia Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika KUCHAKACHUA matokeo ya uchaguzi. Hivyo vyama vya upinzani "kalaga baho" na kubobea katika kupiga kampeni tu, wakati mchakato mzima wa kuwapata Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura unafanywa katika misingi ya KUCHAKACHUA matokeo !!!!
Mwisho ningependa kusema kwamba Zoezi zima la kuwapata WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA mwaka huu katika jiji la Dar es salaam limejaa UFISADI MTUPU !!!
MUNGU IBARIKI DAR ES SALAAM !!!