Uchaguzi Mitaa: Kampeni mwisho Oktoba 24; Kupiga kura tarehe 25-Mambo Mawili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Mitaa: Kampeni mwisho Oktoba 24; Kupiga kura tarehe 25-Mambo Mawili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Oct 24, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Leo tarehe 24 Oktoba ni Siku ya Umoja wa Mataifa lakini pia kwa hapa nchini ni siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa. Upigaji kura ni tarehe 25 Oktoba, 2009.

  Kama nilivyobashiri kwenye mfululizo wa makala zangu kuhusu uchaguzi huu kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu(Makala hizo zinapatikana kwenye blogu http://mnyika.blogspot.com); pamekuwa na ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu za uchaguzi. Uchaguzi si upigaji kura tu na utangazaji wa matokeo; uchaguzi ni mchakato wenye hatua mbalimbali.

  Kati ya hatua muhimu za uchaguzi ni pamoja uandikishaji wa wapiga kura; uteuzi wa wagombea; kampeni; elimu ya uraia; upigaji kura na utangazaji wa matokeo- lakini roho ya uchaguzi ni hatua ya ‘usimamizi wa uchaguzi’. Hatua hii huanza mwanzo mpaka mwisho wa uchaguzi. Usimamizi wa uchaguzi ndio kimsingi huamua kama uchaguzi utakuwa huru na haki ama ni uchafuzi tu wa demokrasia na maendeleo.

  Nimesikiliza kauli za hivi karibuni za viongozi waandamizi wa CCM na serikali yake; kauli ambazo ni bezo kwa utawala bora.

  Alianza Rais Kikwete kwa kusemwa kwamba anatoa mwito kwa wote watakaoshindwa kukubali matokeo badala ya kwenda mahakamani kwa kuwa uchaguzi unaigharimu serikali. Kikwete anayesema hayo akijua kabisa jinsi Wizara ya TAMISEMI(Chini ya Waziri Mkuu Pinda, na Waziri wa Nchi Kombani) imeacha mwanya wa hujuma kwa wagombea kwa kuwatumia watendaji wa kiserikali kama nilivyowahi kubashiri. Kabla kauli ya Kikwete haijakauka, ndani ya Kata yake mwenyewe ya Lugoba; ufa uliotokana na kura za maoni za chama chake, ulisababisha wanavitongoji na vijiji kuhakama CCM kwa wingi na wananchi kuamua kuunga mkono CHADEMA. Kuona hivyo, watendaji wakaamua kuwaengua wagombea waliopitia CHADEMA kwa sababu zisizo na msingi. Wapo walioenguliwa kwa maelezo kuwa hawana kipato kinachowawezesha kuishi; wakulima wa kawaida wanaojulikana kijijini; wengine wakiwa ni wafanyabiashara pale Lugoba miaka nenda miaka rudi. Mmoja baada ya kuleta leseni na risiti za michango ambayo amekuwa akitoa kutokana na biashara yake, bado akaenguliwa kwa kigezo kwamba hana TIN namba! Mgombea wa Uenyekiti wa Kijiji cha Lugoba yeye akaenguliwa kwa maelezo kwamba amedhaminiwa na ngazi ya kata ya chama; jambo ambalo kwa miaka nenda rudi halikuwa na utata miaka nenda miaka rudi kwani kanuni zinaeleza tu kuwa kinachotakiwa ni mgombea kudhaminiwa na chama; kuhusu ngazi gani ni uamuzi wa chama chenyewe. Ya Lugoba ni mfano tu wa jinsi wagombea walivyoenguliwa kwa maelfu katika maeneo mbalimbali ya nchi hususani vijijini. Lakini hata hapa DSM katika uso wa Kikwete mambo hayo hayo yamefanyika; mfano Mgombea wa Uenyekiti hapa Sinza D ameendolewa kwa maelezo kwamba amedhaminiwa na Kata; wakati wagombea wengine wote wameachwa na kimsingi jimbo zima la Ubungo wagombea wamedhaminiwa na kata katika mitaa mbalimbali. Huyu ameondolewa kwa sababu tu Diwani wa Sinza-Mwaking’inda akishirikiana na Meya Londa; swahiba wake mkubwa katika tuhuma zote za Halmashauri ya Kinondoni; wameweza kufanya shinikizo. Ikumbukwe Kamati ya Rufaa ina wajumbe wawili tu wenye kura; mwenyekiti akiwa na Afisa Tawala, katibu wake akiwa ni Afisa ndani ya ofisi yake. Maamuzi hayo, mgombea wetu amepatiwa jana mchana; huku tayari alishaanza kampeni toka tarehe 18 Oktoba. Kamati ya Rufaa ilipaswa kufanya kazi yake mpaka tarehe 18 Oktoba na kutoa taarifa kwa wahusika; lakini kwa kuwa Ofisi ya Afisa Tawala; chini ya Bwana M. Mkapa; inafanya kazi kwa shinikizo, ndio maana haya yanatokea!.

  Baadaye Waziri Mkuu Pinda akajitokeza akisikitika kwamba watu wengi hawajajitokeza kujiandikisha na akaja na hoja kuwa sasa serikali inafikiria kuunganisha uchaguzi huu na wa madiwani ili kuongeza mvuto. Watu wakaona Pinda amekuja na wazo jipya, kumbe ukweli ni kuwa hii imekuwa ni hoja ambayo wadau wamekuwa wakiitaja na kutaka serikali ibadili sheria toka mwaka 2004. Lakini Pinda alisahau kuwa kitendo cha ofisi yake kuhodhi mamlaka ya kutoa elimu ya Uraia na mpiga kura kwenye uchaguzi huu kimepunguza nguvu ya wadau wengine kufanya hivyo. Mathalani hapa Kinondoni, ziara zangu za mikutano ya hadhara zilizuiwa na Kamanda wa Polisi kwa maelekezo kwamba vyama vya siasa haviruhusiwi kufanya mikutano ya aina hiyo. Pinda anajua ni ofisi yake ndiyo iliyokiuka kanuni kuhusu uandikishaji; tarehe 25 Julai ilichapa magazeti ratiba sahihi kuwa uandikishaji ungefanyika tarehe 4 mpaka 24 Septemba; hii ingekuwa kwa siku 21, na mchakato ungekamilika siku 21 kabla ya uchaguzi. Lakini baadaye pamoja na kuwa kanuni zinataka ratiba itolewa siku 90 kabla ya uchaguzi; Ofisi yake ikatoa ratiba nyingine mwezi Septemba kuwa uandikishaji ufanyike tarehe 4 mpaka 10 Oktoba; kwa siku 7 tu; na hivyo umekamilika chini ya siku 21 kama kanuni inavyotaka. Lakini anajua kuwa kwa kufanya hivyo, ofisi yake imechanganganya ratiba hiyo na uboreshaji wa Daftari la Kudumu(DKWK) ambao unaendelea. Kwa mfano katika Jimbo lake yeye mwenyewe la Mpanda Kati; kabla ya kuanza kuandikishwa daftari la mitaa; lilianza la Kudumu; hivyo wananchi wengi walijua kwamba wameshajiandisha tayari hawawajibiki kujiandikisha tena.


  Kama Kikwete alijua, kauli yake ikafuatiwa na ile ya Makamba ya kutangaza kwamba CCM imepita bila kupingwa. Siku Makamba anatoa kauli hii alikuwa anajua kabisa kule nyumbani kwake Tanga; watendaji walichelewesha fomu na kujifisha ili wagombea wa upinzani wasipate; na pia mamia ya wagombea waliofanikiwa kuchukua fomu baada ya nguvu kubwa wakaenguliwa na watendaji kwa sababu zisizo na uzito wowote; jamii ya hizo hapo juu.

  Hata hivyo, ndondondo si chururu; pamoja na hujuma zote hizo, bado idadi ya wagombea wa upinzani imeongezeka hali inayoashiria kupanuka kwa upinzani na vuguvugu la mabadiliko. Makamba anasema CCM imepita bila kupingwa vijiji takribani elfu 3; hii ni dalili njema kwani kwa tafsiri yake ni kwamba zaidi ya vijiji elfu 10 kuna wagombea wa upinzani; kwa upande wa vitongiji anasema elfu 20 wamepita bila kupinga; hii tafsiri yake ni kwamba zaidi ya vitongoji elfu 80; CCM imepata wapinzani. Hili ni ongezeko ukilinganisha na mwaka 2004; ambapo CCM ilipita bila kupingwa vitongoji vingi zaidi na hatimaye ikashinda kwa ujumla kwa asilimia 96 huku vyama vya upinzani vikigawana asilimia 4; hali ya mambo inaonyesha kuwa pamoja na hujuma zote matokeo ya 2009 yatakuwa tofauti sana na yaliyopita. Yapo maeneo ambayo CHADEMA kwa mfano haikuwa na mtandao mpana wa kichama mwaka 2004 lakini sasa imepanuka kuanzia ngazi ya chini; mathalani Jimbo la Ubungo mwaka 2004, CHADEMA ilikuwa na Mgombea 1 tu wa uenyekiti wa Mtaa; Sasa inawagombea kwenye Mitaa 54; wataalamu wa hesabu wanaweza kukukotoa ni ongezeko la Asilimia ngapi, hii ni ishara njema tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2010.

  Hata hivyo, tunapoelekea uchaguzi wa kesho Oktoba 25; kuna mambo mawili lazima yatolewe ufafanuzi kwa umma haraka; mambo haya niliwaeleza TAMISEMI ana kwa ana tarehe 8 Oktoba, wakaahidi kuyafanyia ngazi; ukimya wao unaacha maswali mengi. Hata yanahusu mchakato wa upigaji kura hiyo kesho.

  Mosi, TAMISEMI haikuwa imepanga utaratibu wa kuwa na wino usiofutika kama ilivyo kawaida; matokeo yake ni kwamba mianya ya watu kupiga kura zaidi ya mara moja imeachwa wazi. Walijieleza kwamba muda hautoshi kwa mujibu wa sheria ya ununuzi kuagiza wino toka nje ya nchi; niliwaeleza njia mbadala ni kutumia wino hata wa ndani. Kama wameweza kuwa na masanduku ya kura ya kawaida na karatasi za kura za kawaida; kwa nini kila halmashauri isipewe maelekezo ya kutafuta wino wake kama zilivyopewa mamlaka ya kutengeneza makaratasi ya kura?

  Pili; uchaguzi wa mwaka huu karatasi za kura hazitakuwa na picha za wagombea, wala majina yao wala ya vyama vyao; Mpiga kura atapewa kura iliyowazi ataandika mwenyewe majina ya anaowachagua. Kwa miezi wadau mbalimbali tumekuwa tukihimiza umuhimu wa kuwa na majina na nembo katika karatasi lakini msimamo wa serikali umekuwa ni kukataa kwa sababu mbalimbali. Lakini hivi karibuni, niliwapa pendekezo mbadala ya kwamba majina ya wagombea yasibandikwe nje pekee kama kanuni zinavyoelekeza bali Ofisi ya Waziri Mkuu itoe maelekezo kwa wasimamizi wote majina yabandikwe pia ndani karibu na eneo ambalo mpiga kura atasimama kuandika majina yake.

  Haiingii akilini kwa uchaguzi ambao; kwa upande wa mijini ambapo nafasi zinazogombewa ni saba; Mwenyekiti wa Mtaa na Serikali yake yenye wajumbe Sita; eti mpiga kura aingie ndani akiwa amekumbuka majina kamili ya wagombea wote akayaandike mwenyewe kwa ukamilifu wake; na kwamba makosa yanafanya kura inakuwa imeharibika.

  Kichekecho zaidi ni vijiji ambapo pamoja na Mwenyekiti, Halmashauri za Vijiji huwa na wajumbe kati ya 15 mpaka hata 25; Je, unaweza kukariri majina kamili ya watu wote hao halafu akapewa karatasi tu ndani ukayaandike? Mfumo huu wa kura; unafanyika katika nchi ambayo asilimia kubwa ya wananchi hawajui kusoma na kuandika!

  Hivyo ndiyo vituko vya uchaguzi huu; na kwa kweli matokeo ya uchaguzi hayawezi kuwa kiashiria kamili cha matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ambayo mfumo na utaratibu wake ni tofauti kabisa. Tufuatilie tuone!
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kama ni kweli, and I dont have a reason to doubt you, mpaka Tamisemi waseme vinginevyo, this is a mockery of democracy, which they have taken oath to defend.
   
 3. E

  Engineer JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyika,

  Mambo mengine unayoyasema ni sawa lakini pia hata vyama vya upinzani mnatuangusha kwa kubaki kuwa vyama vya mjini.

  Hawa viongozi wanaochaguliwa sasa ndio watasimamia uchaguzi wa 2010. Nyie badala ya kuweka nguvu kwenye uchaguzi huu ili mupate viongozi wengi wilayani, mmebakia kutegemea CCM wagombane na wale waliochukia ndio wagombee CHADEMA.

  Hapa nilipo mimi Kyela kwenye baadhi ya matawi ndivyo ilivyotokea lakini tatizo ni kwamba hao watu hawana msaada wowote toka CHADEMA wilaya zaidi ya kugonga mihuri kwenye fomu zao. Wakati CCM wilaya wanazunguka kata zote kupiga kampeni, CHADEMA mmemwachia mtu mmoja mmoja apigane vyake vyake.

  Pia viongozi mtakaowapata kwa njia kama hiyo, dakika yoyote wakishawishiwa na CCM, wanaweza kurudi CCM.

  CHADEMA mlifanya mkutano wa maana sana hapa Kyela mjini lakini badala ya kutumia hata siku mbili na kupita mpaka kwenye baadhi ya vijiji, wao wakaishia mjini tu. Watu wa mjini ni matapeli na sio wa kuwaamini kabisa, wanashangilia kila upande. Kura za maana ziko vijijini ambako wananchi wakielewa huwa hawabadiliki.

  Lazima muanze kuimarisha chama chenu huku vijijini, vinginevyo mwakani mtaongeza kura lakini sio kwa kiwango cha kuitikisa CCM.

  Hapa Kyela asilimia zaidi ya 60 CCM wamepita bila kupingwa.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nilidhani mabadiliko halisi yangeanzia kwako bwana injinia!unawezaje kusubiri mnyika aje kyela?itakuwa haina maana kwa wewe kwenda shule,au niseme kujiunga na jf!

  smtms ingefaa mkapunguza nadharia na ushauri mwingi wakati mnajua kabisa mnatakiwa muwe PART OF CHANGES!AM I CLEAR?

  sio lazima uwe unapost tu unapost tu na nadharia kibao.ukweli watu wa aina yako mnaniudhi sana tena sana
   
 5. W

  Wasegesege Senior Member

  #5
  Oct 24, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchambuzi yakinifu ni yule anayeeleza mazuri ya mtu anayemchambua na kisha anaeleza maoungufu yake na mwisho anaeleza nini kifanyike. Lakini hawa jamaa wa Upinzani kila siku wao wanaeleza suala la MAPUNGUFU ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Lakini hawasemi kwamba mwaka huu 2009 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mara ya kwanza unabadiliko makubwa tangu Jamhuri ya Tanganyika izaliwe na hatimae kuibinafsha kwenye Jamhuri ya Muungano.

  Unajua Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu utakuwa na mabadiliko yafuatayo:

  1. Kwanza wananchi wamejiandikisha ili kuweze kuwatambua wananchi halali wa kwenye Kata, Mtaa na hata Kitongoji na majina hayo yatabandikwa kwenye Mbao za Matangazo ili kila mwenye kutaka kuthibitisha fulani ni Mkaazi halali au siyo halali. Uchaguzi wa Mwaka 2004 hili halikuwepo, kila Mtu alikuwa anaweza kwenye kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji au Mtaa na akasimama akasubili kupiga kura bila kufahamika kama ni Mkaazi halali wa eneo hilo.

  2. Uchaguzi wa Mwaka huu watu watatumia karatasi maalum kupiga Kura. Karatasi hizo zina majina ya wagombe ana Vyama wanavyoviwakilisha ambapo kila Mtu atapiga kura kwa kuweka alama ya vema kwenye kisanduku chini ya Mgombe anayedhani ataweza kuleta mabadiliko. Karatasi hizo zina nembo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hili halikuwepo kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2004, wakati ule ilikuwa kila Mtu akifika Mkutanoni anapewa kijikaratasi na kuandika jina la Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kama wagombea ni zaidi ya mmoja na kama mgombe ni mmoja alitakiwa kuandika kwenye hicho kikaratasi ndiyo au hapana.

  3. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2009 kuna masanduku ya kutumbukiza kura zinazopigwa ba wananchi. Kuna sanduku la Mwenyekiti wa Serikili ya Kijiji au Mtaa na kuna sanduku la Wajumbe 20 wa Serikali ya Kijiji au Mtaa na kuna sanduku la Wajumbe 5 kutoka miongoni mwa Wanawake kwenye Mtaa au Kijiji. Hili halikuwepo mwaka 2004. Wakati ule nakumbuka zilikuwa zinatumika hata kofia kuhifadhia Kura. Mtu anavua kofia na watu wanatumbukiza karatasi walizowachagua ndani ya kofia hiyo.

  4. Uchaguzi huu sasa unafanyikia kwenye ngazi ya Kitongoji hii ikiwa na maana ya kwamba, baada ya kuona wananchi wengi huwa hawajitokezi kwenye Mikutano Mikuu ya Kijiji au Mtaa sasa wananchi wanafuatwa huko huko kwenye ngazi za Vitongoji. huku ni kukua kwa Demokrasia. Mwaka 2004 wananchi walikuwa wanatakiwa kwenda kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji au Kitongoji, ama walikuwa hawafiki inavyopaswa ama walikuwa wanafika lakini wengi wakiwa ni wale wa KUPANDIKIZWA.

  5. Uchaguzi wa mwaka 2009 hadi sasa inajulikana idadi halisi ya watu waliojiandikisha - kwa sababu kulikuwepo na Daftari la kujiandikisha kupiga kura kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mwaka 2004 ilikuwa unasubili hadi kura zipigwe ndipo unajua ni Idadi ya watu wangapi wamepiga kura wa walipiga kura.

  6. Vyama vya siasa, Asasi za Kiraia n.k. vilishirikishwa kwenye Mchakato mzima wa kutayarisha Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hapa hakuna wa kumlaumu kwamba TAMISEMI inatubuluza HAPANA. Tulimuona Mhe. Makaidi, tulimuona Mhe. Lipumba n.k wakiweka saini makubaliano ya Mabadiliko ya Kanuni za Uchaguzi na hata CHADEMA waliwakilishwa na Watu wao.

  Nasema tatizo la vyama vya Siasa ni kutaka hata jukumu lao la kuwahamasisha wafuasi wao liwe la TAMISEMI, hili haliwezekani. Pia, nataka niwape uzoefu mmoja. Uchaguzi wa Busanda wale wote waliokuwa wanahudhuri Mikutano na kujaa siyo wote waliopiga Kura.

  Pia, Vyama vya Siasa viwaandae wagombea wao, kila nafasi ya Uongozi ina Sheria zake zinazotakiwa kufutwa kabla hujapendekezwa kuwa Mgombea.

  Mfano Uchaguzi Mdogo wa moja ya majimbo ya Mkoani Mbeya. Mgombea wa CHADEMA alifutwa kwenye nafasi ya kugombea baada ya kukosea taratibu za kupata kiapo cha hakimu. Sheria ya Uchaguzi wa Ubunge inasema kila Mgombea wa nafasi ya Ubunge anatakiwa akapate saini kwa Hakimu wa Mahakama ya mwanza. Lakini kwa kuwa CHADEMA pamoja na kuwa na Wanasehria wazuri haikumuandaa Mgombea wake vyema, badala yake akaenda kuwekewa saini na Wakili. Jamani WAKILI siyo HAKIMU WA MAHAKAMA ya mwanza. Sasa hapa utasema nini.

  Vyama vya Siasa viache kukaa Mijini ni kweli. Nataka niwaambie watu wa mjini siyo wapiga kura. Wapiga kura wapo Vijijini ambapo vyama vya Upinzani huenda wakati wa kufanya Kampeni.

  Assalam Aleykum
   
Loading...