UCHAGUZI Meya Musoma Mjini; CCM yaanguka chali mbele ya CHADEMA

Hapo chacha......! Mzee stivini wa-hasira upooo! Ooonh chadema kusambaratika......ooooonh...aaaaalaaah!
 
Huyo alie maliza muda wake anatoka chama gani.
"
"Naibu Meya Angela derrick Lima(CHADEMA) amemaliza muda wake "kwa nini usisomethread yote kuepuka kuuliza maswali ambayo majibu yake yapo obvious????
 
salamu kwa Nyambari Chacha Maliba Nyangwine

Hivi lile lingine la Thomas Nyangwine alilikana kumbe? Ndo jina alilolitumia kusomea Sekondari...au yale yale ya Lameki Madelu wa kule Kinampanda na Ndako na Shelui na Misigiri?
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewagaragaza mahasimu wao wa kisiasa CCM, katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma, kwa kura 13 dhidi ya 4.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Jumanne, mgombea wa CHADEMA, Bwire Nyamweto Bwire ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwisenge (alikosoma Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere), alipata kura 13 dhidi ya kura 4 alizopata mgombea wa CCM, Ali Jamah Hersy.

Mbali ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini kupata nafasi ya naibu meya, pia wagombea wake, walifanikiwa kushinda uenyekiti wa kamati zote manispaa hiyo, ambapo Aloyce Renatus Mawazo
Diwani wa Makoko alichaguliwa kuongoza Kamati ya Afya.

Naye Diwani wa Kata ya Bweri, Zedi Shaaban Sondoki alichaguliwa kuongoza Kamati ya Fedha na Uchumi, huku Diwani wa Kitaji, Siza Haile Tarai alichaguliwa kuongoza Kamati ya Mipango Miji.

Itakumbukwa kuwa Manispaa ya Musoma inaongozwa na Meya anayetokana na CHADEMA, Mheshimiwa Alex Malima Kisurura.

Manispaa hiyo ina jumla ya madiwani 18, ambapo CHADEMA ina madiwani 11, CCM madiwani 4 na CUF madiwani 3.

Diwani wa Mkendo ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, hakuwepo katika uchaguzi huo kwa sababu ya majukumu mengine ya kibunge mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo (na nini tena) zinazoongoza Serikali za Mitaa, uchaguzi wa Naibu Meya hufanyika kila baada ya miaka 2.

Kwa hiyo katika Manispaa ya Musoma, CCM wanaendelea kushikilia nafasi ya upinzani. Tanzania bila CCM inawezekana, safari ya kutafuta mabadiliko ya mfumo na utawala katika nchi hii inasonga mbele, muda ni huu.

Hapo kwenye red nadhani haupo sahihi. Huko Musoma, ccm ndio chama kikuu cha upinzani!
 
yaani adhabu hii haitakomea msoma tu kwa kifupi ccm inakazi kubwa sana hata leo hii uchanguzi ukifanyika jk hawezi hata pata kura alizoiba nakumuweka kwenye urais
 
Namimi nakitambua rasmi kwamba hiki ni moja ya kipigo kikali kwelikweli kwa ccm, damu mdomoni, masikioni, mapuani watu wanakikimbia hawataki kukisaidia, nawashauri hapo msoma nendeni mkakitupe chama hiki mto kirumi kikawe chakula ya mamba.
 
ni kweli ila walinichukiza sana walipoliachia jimbo la Tarime kizembe
Mkuu kama una kumbukumbu, mgombea waliyemsimamisha 2010 alijiunga na CDM kwenye uchaguzi mdogo baada ya kifo cha Wangwe. Huyu hakujiunga na CDM kwa kuwa alikuwa na mapenzi nacho. Alijiunga baada ya kukosana na Nchimbi huko CCM. Watu wa aina hii wanaweza kugawa wanachama na kura, na hicho ndicho kilichotokea Tarime. Mwera hakufurahishwa kuondolewa na wakuja kwenye chama, akaingia CUF na kuzigawa kura. (Falsafa ya bora tukose wote)

Bila shaka 2015 watakuwa makini zaidi. Hawa wanaosubiri watengenezewe mambo tuwaulize miaka yote walikuwa wapi. Mtu anapokuja, apewe walao miaka 3 kabla ya kupewa nafasi ya uongozi. Chama kinao wanachama wengi sana wanaoweza kukijenga bila kuhitaji hawa wanaotemwa na magamba. Kama vipi waende huko ADC wakatigite.
 
nakushukuru mkuu kwa analysis yako ya kisayansi big up!!
 
Back
Top Bottom