UCHAGUZI Meya Musoma Mjini; CCM yaanguka chali mbele ya CHADEMA

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
Kama manavyofahamu kwa kanuni za halmashauri, Naibu wa Meya hchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja. Naibu Meya Angela derrick Lima(CHADEMA) amemaliza muda wake kikanuni na hivyo hii inawalazimu waheshimiwa Madiwani kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi katika Baraza hili kuchaguwa mtu mwingine wa kukalia kiti hiki! Kinachoendelea hapa kwa sasa ni waheshimiwa kuwasili ukumbini na shughuli itaanza punde! Kumbuka CCM, CHADEMA, CUF wote wana wawakilishi ila CHADEMA ndio wengi ...... More updates in a minute...

UPDATES...
Mstahiki Meya amekwisha fika hapa, Dua imesomwa, na sasa anatoa maneno ya utangulizi, kuna uchaguzi wa N/Meya, uchaguzi wa Kamati mbili za Kudumu na kupokea Report ya maendeleo ya Mwaka, Agenda zote zimethibitishwa.

Shuguli zilizotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Musoma
kushiriki katika zoezi la kusafisha kumbukumbu za watumishi
.....
Kinachoendelea hapa ni kusomwa kwa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Manispaa

uchaguzi umemalizika Mgombea wa CHADEMA Mh Nyamwero amepata 13, huku Mh Jamal wa CCM amelamba 4 tu, huu ni mwendelezo wa kipigo kikali kinachoendelea kutolewa na peoples....

Mgombea wa CUF amekula kona ....
 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewagaragaza mahasimu wao wa kisiasa CCM, katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma, kwa kura 13 dhidi ya 4.



Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Jumanne, mgombea wa CHADEMA, Bwire Nyamweto Bwire ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwisenge (alikosoma Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere), alipata kura 13 dhidi ya kura 4 alizopata mgombea wa CCM, Ali Jamah Hersy.


Mbali ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini kupata nafasi ya naibu meya, pia wagombea wake, walifanikiwa kushinda uenyekiti wa kamati zote manispaa hiyo, ambapo Aloyce Renatus Mawazo
Diwani wa Makoko alichaguliwa kuongoza Kamati ya Afya.


Naye Diwani wa Kata ya Bweri, Zedi Shaaban Sondoki alichaguliwa kuongoza Kamati ya Fedha na Uchumi, huku Diwani wa Kitaji, Siza Haile Tarai alichaguliwa kuongoza Kamati ya Mipango Miji.

Itakumbukwa kuwa Manispaa ya Musoma inaongozwa na Meya anayetokana na CHADEMA, Mheshimiwa Alex Malima Kisurura.


Manispaa hiyo ina jumla ya madiwani 18, ambapo CHADEMA ina madiwani 11, CCM madiwani 4 na CUF madiwani 3.


Diwani wa Mkendo ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, hakuwepo katika uchaguzi huo kwa sababu ya majukumu mengine ya kibunge mjini Dodoma.


Kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo (na nini tena) zinazoongoza Serikali za Mitaa, uchaguzi wa Naibu Meya hufanyika kila baada ya miaka 2.


Kwa hiyo katika Manispaa ya Musoma, CCM wanaendelea kushikilia nafasi ya upinzani. Tanzania bila CCM inawezekana, safari ya kutafuta mabadiliko ya mfumo na utawala katika nchi hii inasonga mbele, muda ni huu.

 
Viva CHADEMA,hawa magamba hawana jipya kwani wanagharamia kukimbiza mwenge kwa mamilion ya shilingi huku wakiwasahau walimu.
Kaburi la ccm naliona kwa ukaribu zaidi.
 
Back
Top Bottom