Uchaguzi mdogo Zanzibar Chadema yajikongoja si haba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi mdogo Zanzibar Chadema yajikongoja si haba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Apr 19, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Magharibi, Suluhu Ali Rashid leo amemtangaza mgombea wa CCM, Hamza Khamis Juma kuwa mshindi katika Uchaguzi huo kwa kupata kura 807 dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani.

  Mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Ali Juma alipata kura 559, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata kura 33 kati ya kura halali 1,399 zilizopigwa. Waliojiandikisha walikuwa 4,059.

  Uchaguzi huo umefanyika kutokana na kifo cha Haji Hamad (CUF) kilichotokea mwaka jana.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Good ina maana hao 33 hawakujali vitisho vya CCM na CUF kuhusu Chadema
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Inatia matumaini, kama unapata 33 ndani ya nyumba ya wenzi!!
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Kamilisha statement walikuwa na uchaguzi wa ngazi ipi ya uongozi? maana idadi ya kura za mshindi inanistuwa kwa sababu ninapoishi mimi hata mwenyekiti wa serikali ya mtaa hawezi akashinda kwa kura chache hivyo.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Ni uchaguzi wa Diwani yani idadi inazidiwa na kura za mjumbe wa mtaa wangu, unapoambiwa idadi ya kura za wabunge wote wa CUF ni sawa na kura alizopata Mnyika unafikiri uongo.
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  Apart from names do you detect any difference between the two parties?
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo utagunduwa ile hoja ya wabunge kutetea kupewa magari ya kifahari haina mashiko, maana wapo wabunge ambao wana uwezo wa kutembelea jimbo lake kwa mguu na ndani ya lisaa limoja anakuwa ametembelea jimbo zima.
   
 8. A

  Albimany JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Hata kura za Diwani wa China Ni nyingi kuliko za Rais wa Tanzania.

  Sijui kwa hoja hizo Wachina waongezwe kiti chengine UN au haki yao iwe kubwa zaidi ya Tanzania?
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Mtu mwenye upeo mdogo wala hupati shida kumgunduwa, nakupa kaswali kadogo tu, China inafuata siasa za mlengo gani? na je unafahamu vizuri mfumo wa uongozi wa china? unajuwa China ina majimbo mangapi? ni vizuri kabla ya kuja kuongea uharo na pumba hapa JF nakushauri uwe unapitia kwanza google, ukishapata elimu ya bure kutoka google ndio uje hapa na data. usidhani watu hapa tupo kwa ajili ya porojo.
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Tunaongelea rationale ya wabunge/diwani kupewa uzito sawa hata kama anaongoza mitaa miwili tofautisha Tanzania na China ambayo hatuna common interest nayo.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sikutegemea kwa Zanzibar wangepata hata kura 2!...nilikuwa na uhakika wa kura 1 ya mgombea pekee!
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Mambo yanaenda yanabadilika.
   
 13. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Albimany Tanzania ni nchi moja na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, hivyo hakuna uwiano na mgawanyo wa rasilimali za Taifa. Zanzibar tunawanyenyekea na kuwabembeleza sana. Inawezekanaje kwa upande wa Zenji kila baada ya mitaa mitatu kuwe na mbunge? Wakati Bara mbunge anawakilisha zaidi ya watu laki 2 au 3? Hoja ni ya msingi lakini wewe unajivua gamba kukwepa hoja!
   
 14. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Unajua mkuu, pengine mgombea ni shababi lenye wake wa 4 na watoto 16,ukijumlisha na ndugu zake wa karibu wanaomtegemea kura 30 anafikisha kirahisi kabisa bila ata ya kupiga kampeni nje ya nyumba yake.
   
 15. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Albimany is right, hamkuipenda tu argument yake. Sasa tatizo lenu ni nini na Zanzibar ndio mlioamua kuivamia? Kama Zanzibar ni kero na inawaumiza, daini Tanganyika yenu halafu muungane na Congo DR yenye watu wengi.

  Mkifanya uzembe, iko siku mtajikuta hamna Tanzania wala Tanganyika wadau
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sanks ni kweli
   
 17. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi moja na Zanzibar ni nyengine usipoteshe Mkuu:

  Katiba ya Zanzibar inasema;

  (9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.

  (9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …

  (10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:

  (10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.

  (12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.

  (21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…

  (23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…


  Lete jengine Mkuu.
   
Loading...