Uchaguzi mdogo wa madiwani kufanyika octoba, 28. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi mdogo wa madiwani kufanyika octoba, 28.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Sep 21, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ratiba Ya Uchaguzi Mdogo Wa Madiwani
  .
  Na Veronica Kazimoto- MAELEZO Dar es Salaam 20/09/2012.
  Uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata ishirini na tisa na halimashauri ishirini na saba Tanzania bara utafanyika tarehe 28 Oktoba, mwaka huu. Akizungumza katika mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na viongozi wa siasa ngazi ya Taifa leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Mallaba amesema maandalizi ya uchaguzi huo yameanza rasmi ili kuhakikisha kwamba kila raia mwenye sifa anapata fursa ya kushiriki na kuchagua kiongozi anayemtaka. Amezitaja Kata na Harimashauri hizo kuwa ni pamoja na Bangata (Halmashauri ya Wilaya ya Arusha), Darajambili (Halmashauri ya Manispaa ya Arusha), Msalato (Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma), Mpwapwa (Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa), Magomeni (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Lwezera (Halmashauri ya Wilaya ya Geita) na Bugarama (Halmashauri ya Wilaya ya Kahama). Nyingine ni Mwawaza ambayo iko Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Vugiri (Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe), Tamota (Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto), Makata (Halmashauri ya Wilaya ya Liwale), Mnero Miembeni (Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea), Mlangali (Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa), Luwumbu (Halmashauri ya Wilaya ya Makete), na Mpepai (Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga). Zimetajwa pia Kata za Mletele (Halmashauri ya Wilaya ya Songea), Ipole na Kiloleli (Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge), Miyenze (Halmashauri ya Wilaya ya Tabora), Karitu (Halmashauri ya Wilaya ya Nzega), Mpapa na Myovizi (Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi), Lubili (Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi), Kilema Kusini (Halmashauri ya Wilaya ya Moshi), Nanjara/ Reha (Halmashauri ya Wilaya ya Rombo), Mtibwa (Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero), Mahenge (Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga), Likokona (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu) na Kitangari (Halmashauri ya Wilaya ya Newala).
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Katika mkutano huo Mallaba ametangaza ratiba ya uchaguzi mdogo wa madiwani kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 2 oktoba, 2012, kampeni za uchaguzi zitaanza oktoba 3 hadi oktoba 27, 2012 na fomu za uteuzi kwa wagombea na wasimamizi wa uchaguzi zimeanza kutolewa.
   
 3. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Wale watano (5) waliofukuzwa kule Arusha vipi?? Any news??
   
 4. t

  tenende JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kata zao hazimo katika mchakato. sehemu kubwa ya kata hizo madiwani walifariki dunia. Mmoja alijivua gamba.
   
 5. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hivi wa Arusha vipi au Tendwa anataka kuchakachua haoni kama majimbo yako wazi muda mrefu na wananchi wanahitaji wawakilishi
   
 6. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  TENDWA siku zote anasubiri maelekezo kutoka ccm, NADRA sana kufanya uamzi kwa kutumia akili zake tu.
   
Loading...