Uchaguzi mdogo wa madiwani kufanyika Mei 19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata zilizopo kwenye halmashauri sita katika mikoa sita ya Tanzania Bara.
312d936b2e68a5c17bfa51cea7e0dd79

Mwenyekiti wa Tume NEC

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Rufani Semistocles Kaijage, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa uchaguzi huo utafanyika Mei 19, mwaka huu.
Akisoma taarifa kwa umma iliyotolewa na Tume, Jaji Kaijage, alisema fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa Aprili 15 hadi 19, mwaka huu.

Jaji Kaijage alisema uteuzi wa wagombea utafanyika Aprili 19 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Aprili 10 hadi 18, mwaka huu.
Alifafanua kwamba uchaguzi katika kata hizo, utafanyika sambamba na uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Kiti cha ubunge cha Arumeru Mashariki kiko wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Joshua Nassari, kukosa sifa za kuendelea kushikilia nafasi hiyo kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo vya bunge kama kanuni zinavyosema.

"Tume inapenda kuvikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha uchaguzi huu mdogo," alisema Jaji Kaijage.

Awali Jaji Kaijage alisema uamuzi wa kutangaza uchaguzi kwenye kata hizo umefanyika baada ya tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 aliiarifu tume juu ya uwapo wazi wa nafasi hizo.

Alisema nafasi hizo wazi zimetokana na vifo vya madiwani watano (5) na mmoja kujiuzulu.

Kata hizo ni za Uwanja wa Ndege (Mpanda mkoani Katavi), Kitobo (Missenyi mkoani Kagera), Kyela (Kyela mkoani Mbeya, Mikocheni Manispaa ya Kinondoni (Dar es Salaam), Mvuleni (Lindi) na Manda Chamwino mkoani Dodoma.
 
Back
Top Bottom