Uchaguzi Mdogo wa Madiwani - Arusha Unapigwa Danadana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Mdogo wa Madiwani - Arusha Unapigwa Danadana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wambugani, Dec 31, 2011.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  NEC: Kasoro zinachelewesha uchaguzi wa madiwani Arusha
  Na Richard Makore
  31st December 2011


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema uchaguzi mdogo wa madiwani katika jijini la Arusha unachelewa kufanyika kutokana na barua waliyoondikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuwajulisha nafasi hizo zipo wazi kuonekana ina mapungufu ya kisheria.

  Kwa mujibu wa ofisi ya habari ya NEC, kasoro hizo ndizo zinazokwamisha kuatangzwa kwa tarehe ya uchaguzi mdogo pamoja na maeneo mengine ambayo nafasi za udiwani zipo wazi.

  Ofisi hiyo ilisema kuna nafasi zaidi ya 10 za udiwani ambazo zipo wazi na kwamba baada ya kukamilsiha taratibu za kisheria tarehe rasmi ya kufanyika uchaguzi huo itatangazwa.

  “Ni kweli tuliandikiwa barua na Tamisemi kutujulisha kwamba nafasi hizo zipo wazi, lakini baada ya kuipitia ilibainika kuwa na mapungufu kadhaa ya kisheria hivyo tukaamua kuirudishwa ili ifanyiwe marekebisho,” alisema mmoja wa ofisa habari wa NEC ambaye hakutaka kutaja jina lake.

  Aliongeza kuwa sababu nyingine inayokwamisha kutangazwa kwa tarehe ya kufanyika uchaguzi huo ni kutokana na madiwani ambao nafasi zao zimetangazwa kuwa wazi kufungua kesi mahakamani.

  Madiwani watano ambao nafasi zao zipo wazi katika jiji la Arusha walivuliwa uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Oktoba, mwaka huu, baada ya kubainika kwamba walikiuka maagizo ya chama chao kwa kuingia katika mwafaka bila baraka za chama.

  Katika maeneo mengine nafasi hzio zipo wazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kufariki dunia kwa Madiwani waliokuwepo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ccm ina kiwewe cha kufiwa na diwani wake mjini humo. Uchaguzi utacheleweshwa sana.
   
 3. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndo inaweza ikawa imepotezewa hivyo c wanafaham cdm watavikomba vyote.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Uchaguzi wa Madiwani Arusha utacheleweshwa mpaka March 2012.

  Kampeni za Umeya hiyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...