uchaguzi mdogo Lwezera:Vincent Nyerere atinga Geita kuongeza nguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

uchaguzi mdogo Lwezera:Vincent Nyerere atinga Geita kuongeza nguvu

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by WABHEJASANA, Oct 27, 2012.

 1. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wakuu wa JF:
  Natumai hamjambo na mmeamka salama wasalmini,Kesho ndio kesho ambapo kutakua na uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Lwezera Tarafa ya Bugando wilayani Geita.

  Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Anatory Mkufu ambaye alifariki dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea jijini mwanza mapema mwaka huu.

  Kiukweli ni kwamba pamoja na kwamba ccm ilikuwa ikishikilia kata hiyo lakini chama cha wananchi C.U.F kilikuwa kikionekana kina nguvu sawa na CCM kwa mgawanyo ufuatao.

  C.u.f ilikuwa ikiongoza vijiji viwili kati ya Vinne vilivyoko katika kata hiyo,huku pia ikiongoza Vitongoji vitatu kati ya tisa vilivyoko katika kata hiyo,hivyo ccm nayo ikabaki na vijiji viwili,na vitongoji 6.

  Lakini baada ya kutokea kifo cha Diwani huyo na uchaguzi kutangazwa na kampeni kuanza CDM wameonekana kubadili upepo wa kata hiyo baada ya kuingia kwa kasi kubwa kwenye uchaguzi huo,na hivyo kuonekana kuimeza C.U.F na CCM.

  Kwa mujibu wa mgawanyo huo niliouonyesha hapo juu ni wazi kwamba mshikemshike utakuwa kati ya CCM na CDM ingawa kwa mujibu wa uchunguzi wangu CCM wanaweza kuibuka na ushindi kwa vile C.U.F kwa vyoyote bado inang'ang'ana kuhakikisha kwamba inaendelea kuwa na heshima kwe ye kata hiyo na si ya kubeza,hivyo CDM kwa vyovyote vile kutokana na kasi yake itagawana kura na C.U.F ambayo ni asilimia 50 kwa mujibu wa mgawanyo wa madaraka ya kata hiyo kati ya C.U.F na CCM.

  Kutokana na hali hiyo huenda CCM ikaendelea kumantain kura zake za ushindi ilioupata kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 kutokana na hivi vyama viwili nilivyovitaja hapo juu kuendelea kulumbana na kutoleana maneno ya kejeli,huku kila kimoja kikitamba kuiangusha ccm.

  Hata hivyo katika kuhakikisha kwamba CDM wanashinda asubuhi hii tayari makamanda kadhaa wakiongozwa na Vincent nyerere wamekwishaingia kwenye eneo kuanza purukushani za mwishomwisho kuhakikisha kwamba wanalikomboa jimbo hilo.

  Hata hivyo tayari Dr Slaa wiki mbili zilizopita alikuwa kwenye kata hiyo kumwaga sumu kwa wananchi ili kuhakikisha kwamba wanavipiga kumbo C.U.F na CCM kwenye uchaguzi wa kesho.

  yote kwa yote ni lazima kutakuwa na mvutano mkali kwenye uchaguzi wa kesho lakini iwe isiwe kwa namna upepo ulivyo mshindi atakua ni kati ya ccm ama cdm,nina hakika nitakuwa eneo la tukio kuwajuza LIVE bila utata matokeo mazima.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Safi sana kamanda Vincent Nyerere.kamua hao magamba.
   
 3. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,361
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  M4C, twanga kotekote!
   
 4. C

  CNN Senior Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2012
  Messages: 112
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Poa kaka ufike salama kesho utupe taarifa live
   
Loading...