Uchaguzi mdogo kata ya Chipogolo,mkoani Dodoma jimbo la Kibakwe

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,182
1,490
Maelezo ya KATA
Sehemu:Kata ya CHIPOGOLO ipo Mkoa wa Dodoma,Jimbo la Kibakwe,Wilaya ya Mpwapwa,kata ilipo ni kilometa zaidi ya 91 kutoka Makao Makuu ya Mkoa.

Vyama vilivyochua Fomu na kutudisha ni
1.CHADEMA
2.CCM

Wagombea ni vijana wote wana umri chini ya miaka 30 na wahitimu wa Vyuo vikuu...

HOSEA MANYIA FWEDA ni mgombea wa CCM

.
3fb06cf40bdf47a54a834ca69644a587.jpg


JAFARY JUMANNE SIMBA ni mgombea wa CHADEMA....

a62ec7e1b9752c48b7da2c169ac7add9.jpg


Kipenga kiipurizwaaaaaa Chipogolo kazi inaanza,nimeanzisha huu Uzi kwaajili ya kueleza kampeni zote mpaka mwisho kwenye Uchaguzi huu mdogo pekee mkoani Dodoma!
 
http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/43e40c7068040f60b890d19186b2dc3f.jpg[/IMG

[IMG]http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/a54f8ee85d500146cf733b5e47a30b71.jpg

Jengo la ofisi za CCM kata ya Chipogolo na Chadema hawana ofisi
 
wajinga wengi wakipiga kura husababisha matokeo ya kijinga na werevu wengi wakipiga kura husababisha matokeo yenye "akili"
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WALIOENGULIWA WAMEKATA RUFAA

Baada ya uamuzi wa baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi katika uchaguzi wa marudio nafasi ya udiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu, kutowateua na hivyo kuwaengua wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kata 6, wagombea hao wamekata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa mujibu wa Sheria ya Chaguzi za Serikali za Mitaa (2015).

Baada ya kupokea taarifa na kuzifanyia kazi hoja za mapingamizi yaliyosababisha wagombea wa CHADEMA kuenguliwa, wanasheria wamebaini kuwa, sababu zilizotumika kuwaengua wagombea hao hazina mashiko ya kisheria kwa mujibu wa taratibu zinazosimamia uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2015, Kanuni za Sheria ya Gharama za Uchaguzi za mwaka 2010 na Maelekezo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea ya mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taratibu hizo, zimeainisha bayana sababu ambazo zinaweza kumfanya mgombea kuwekewa pingamizi, masharti hayo hayakufuatwa wakati wa kuwekwa kwa mapingamizi hayo.

Lakini jambo la kushangaza ni kuwa wasimamizi wa uchaguzi wameyakubali mapingamizi hayo ambayo yako kinyume kabisa na sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa mfano wapo wagombea ambao wamewekewa mapingamizi kwa hoja kuwa sio wakaazi wa kata husika wakati ni watu wanaoishi kwenye kata husika na pia waliwahi kuchaguliwa kuwa Madiwani katika kata hizohizo kama ambavyo imetokea katika kata za Saranga na Siuyu.

Kwa sababu mapingamizi hayo hayajakidhi matakwa ya kisheria kama ambavyo ilitakiwa kuwa kwa mujibu wa sheria, wagombea wa CHADEMA walioenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi katika kata 6 kati ya kata 43 zinazotarajiwa kurudia uchaguzi na wamejaza fomu namba 12 za kukata rufaa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi.

Tumaini Makene,
Afisa Habari CHADEMA.
 
Back
Top Bottom