Uchaguzi Mdogo Jimbo la Sumbawanga Kitendawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Mdogo Jimbo la Sumbawanga Kitendawili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wikolo, May 30, 2012.

 1. w

  wikolo JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema haiwezi kuitisha uchaguzi mdogo kwa sasa katika Jimbo la Sumbawanga Mjini, mkoani Rukwa, kwa vile kuna kusudio la kutaka kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga, uliotengua matokeo ya ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo (CCM), Aeshy Khalfan Hillary.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema kutokana na kusudio hilo, wataitisha uchaguzi huo iwapo Mahakama ya Rufaa itatengua uamuzi huo wa Mahakama Kuu.

  “Hatuwezi kufanya uchaguzi (katika Jimbo la Sumbawanga Mjini), Mawasiliano yaliyopo ni kuwa kuna nia ya kukata rufaa Mahakama ya Rufaa, Tunasubiri kama kutakuwa na utenguzi au la,” alisema Mallaba.

  Uamuzi wa kutengua matokeo hayo ulitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Bethwell Mmilla, ambaye alisikiliza kesi hiyo.

  Kesi hiyo namba 01 ya mwaka 2010 ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Norbert Yamsebo.

  Katika uchaguzi huo uliofanyika mwaka juzi, ulikuwa na ushindani mkubwa, ambapo Aeshi alipata kura 17,328 wakati Yamsebo alipata kura 17,132.

  Jaji Mmilla alisema alitengua matokeo hayo kutokana na madai ya kuwapo kwa vitendo vya rushwa na vurugu zilizokuwa zikifanywa na wafuasi wa CCM wakati wa kampeni.

  Source: IPPMEDIA

  Naomba mwenye uelewa na hili anisaidie kujua zaidi. Rufaa haijakatwa bado lakini tume inasubiri kwa sababu kuna mtu ana nia ya kukata hiyo rufaa. Hivi itakuwaje kama rufaa hiyo itakatwa 2014? Huwa kuna ukomo wa muda ambao tume inaweza kusubiri? Je, hili lipo kisheria?
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu maswali unayojiuliza wewe hata mimi najiuliza!kama kuna mwanaJF mwenye maelezo ya kutosha, tafadhari tunaomba msaada wako!
   
 3. Encyclopaedia

  Encyclopaedia Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimejiuliza maswali kama hayo pia, then nikaingiwa na wasiwasi au kwa kuwa aliyetenguliwa ni GAMBAAA
   
 4. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,670
  Likes Received: 2,205
  Trophy Points: 280
  kuna muda kisheria wa kusubili kama kuna m2 atakata rufaa. Sina kumbu kumbu sahihi lakn hauzid miez mitatu.
  na kesi ikikatiwa rufaa inasikilizwa ndani ya mwaka mmoja na si zaid!
   
 5. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  suala la kukata rufaa au kutokata rufaa ni la mtu binafsi. Mi nadhani tume wangetangaza uchaguzi kwenye majimbo yote likiwemo la Arusha ili mahakama ndio isimamishe chaguzi hizo ili kusubiri matokeo ya hukumu hizo. napata tabu tabu kidogo na uelewa wa wataalamu wa tume yetu ya uchaguzi. kama ni hivyo basi Makongoro naye asimamishwe ubunge ili tyusubiri rufaa ya Mpendazoe kule segerea shame on tume ya wachakachuaji
   
 6. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Katika sheria kuna hatua mbili katika kufikia rufaa.Kuna kusudio la kukata rufaa(Notice of Appeal) na kuwasilisha Hati ya Rufaa(Memorandum of Appeal).Kusudio la rufaa huisha ndani ya siku 21.Hata Hati ya Rufaa nayo ina ukomo wake.Nayo ni siku 21.Naishia hapo...
   
 7. K

  KIJIGOJUNIOR Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wakuu wa JF,

  To cut the long story short, I was in court this morning (High Court Dar es Salaam District Registry) and I was able to meet Adv. Nassoro, who represented Hillary in the High Court case in Sumbawanga. He told me that yesterday they lodged their appeal before the Court. So let us maintain patience for the Court of Appeal to do justice
   
 8. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mh, kweli hapa wataalam wetu wa kisheria mnahitajika kutoa mchango, hasa kutumegea sisi tusio na taaluma hiyo kwamba huo mda inakua vipi, manake haya maswali tutajiuliza wengi sana, au wana andaa tena mazingira ya rushwa??????
   
 9. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  point, let's keep the faith
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  tatizo ni tume ilikuwa inasubiri kwa maelekezo gani? ya mdomo? kutoka kwa mrufani au kwa raisi? haya mambo hayajawekwa wazi.
   
 11. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani Arusha nako wametangaza uchaguzi mdogo ni lini? Hata mi najiuliza kwa nini?Tuendelee kuuliza
   
 12. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi magamba hayawezi kubali kurudi katika chaguzi!

  Yanajua hayashindi kamwe!

  BTW, kama rufani imekatwa tungoje!
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Thank you Mkuu for your useful comment!
   
 14. M

  MWananyati Senior Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Mtengeti,
  Suala la Mkongoro na Aeishy ni tofauti kidogo.
  1. Najua huwa una kipindi kinachowekwa kwa mshtaki/mshtakiwa kukata rufaa iwapo hajaridhika na maamuzi ya mahakama. Wanasheria wanaweza kufafanua zaidi hili.
  2. KWa sula la makongoro ni kuwa hakuvuliwa ubunge, so anaendelea kutekeleza wajibu wake kikatiba kama mbunge halali kwasababu mahakama haijatengua ubunge wake. Aeshi kapoteza ubunge. Ya aeshi ni kama ya Lema ingawa lema tayari amesha-forward sualal lake mahakama ya rufaa

  CHAMSINGI ni huyo mkurugenzi wa nec angetoa ufafanuzi juu ya muda ambao bado bwana aeshi anao ili kukata rufaa. Otherwise sio ukwapuaji wa demokrasia
   
 15. w

  wikolo JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Ok, kama atakuwa amekwambia hivyo tutaendelea kusubiri na kuona.
   
 16. w

  wikolo JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hili nalo neno.
   
Loading...