UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KITETO:Je Upinzani wako tayari kuungana?

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Heshima Mbele wnabodi,Tayari Jaji Mstaafu Lewis Makame keshatangaza tarehe ya uchaguzi wa jimbo la kiteto ambalo Mbunge wake alifariki Desemba 16 mwaka jana,marehemu Benedict Kiroya Losurutia.Uchaguzi utafanyika tarere 24 Februrari 2008 na uteuzi wa wagombea ni tarehe 29 Januari 2008 na kampeni zitaanza tarehe 30 Januari mpaka 23 Februari 2008.

wapinzani wa vyama vikubwa vinne waliungana,Je hawaoni ni wakati muafaka kwa sasa kupendekeza jina la mtu mmoja ambaye atagombea na kushinda jimbo hilo la kiteto?.Naomba wanachama wa JF wamependekeze ni nani apewe jukumu la kugombea.Je ni mzee wa kilalacha arude bungeni(MREMA)?Je James Mbatia?tunahitaji tingatinga ili likaongezee nguvu ya upinzani bungeni.Ninaamini kukiwa na ushirikiano na busara za JF tukipigia kampeni ya kuamsha hari basi tarehe 25 Februari kutakuwa na mbunge wa upinzani.

pendekezeni jina la mgombea unafikiri anuzika na asiye fisadi,na kwasababu mawazo naamini viongozi wa vyama hivi vinne ni wanachama wazuri wa JF ,tunahitaji kumkoma Nyanmi giladi sababu tumeshachoka kuzugwa bila kuzugika.

tuna siku 15 tu kuweza kuchagua mgombea wa Upinzani.Naomba kuwasilisha
 
Nadhani ifanyike analysis kwanza ya wabunge wa upinzani waliogombea uchaguzi uliopita. Na kuona ni nani hasa anakubalika ktk jamii hiyo
 
In Kiteto, Benedict Losuruti of CCM won with 30,483 votes, while his close opponent, Chadema’s Victor Kimesera followed with 22,565 votes. That was 2005 election. What should we expect from the by election?

Asha
 
Jambo ambalo linanishangaza kuhusu Tume ya uchaguzi ni namna inavyotangaza uchaguzi katika majimbo. Nakumbuka Mbunge Pharesi Kabuye wa jimbo la Biharamulo TLP(kama sijakosea) matokeo yake, yalitenguliwa na mahakama mapema hata kabla ya kifo cha huyo wa kiteto, lakini nashangaa uchaguzi katika jimbo hilo haujatangazwa mapka leo. Kwa nini?
 
kwa matokeo hayo.kwa asilimia 80 mapndekeza victor agombee tena.Je ukijumlisha kula za Upinzani.walikuwa wanamfikia maregemu Benedict?
 
Honestly, we should expect Chadema's Victor Kimesera to contest again if he not yet crossed the border to CCM aka Fisadi party. Nguvu za pamoja TLP, CUF NCCR, UDP, PPT Maendeleo etc lazima jimbo lichukuliwe...inshallah naomba kuwakilisha
 
In Kiteto, Benedict Losuruti of CCM won with 30,483 votes, while his close opponent, Chadema’s Victor Kimesera followed with 22,565 votes. That was 2005 election. What should we expect from the by election?

Asha

Wagombea wa CUF,TLP,na NCCR je walipata kura kiasi gani? tukijua hizo walizopata basi hapo itakuwa kama kumsukuma mlevi vile...ushindi kwa Victor

Na ofcourse hapa mkakati wa kuwaangusha hawa mafisadi ni muhimu, make bila hivo twafa!! yaani inabidi kakitokea kanafasi ni kukapigania hadi dakika ya mwisho!
 
Jambo ambalo linanishangaza kuhusu Tume ya uchaguzi ni namna inavyotangaza uchaguzi katika majimbo. Nakumbuka Mbunge Pharesi Kabuye wa jimbo la Biharamulo TLP(kama sijakosea) matokeo yake, yalitenguliwa na mahakama mapema hata kabla ya kifo cha huyo wa kiteto, lakini nashangaa uchaguzi katika jimbo hilo haujatangazwa mapka leo. Kwa nini?

Kabuye alikata rufaa. Hicho kiti hakiwezi kutangazwa kuwa wazi hadi mwisho wa process za mahakama, including kupeleka nakala ya hukumu kwa Spika na Tume ya Uchaguzi.
 
na kweli wajimini hebu hawa wapinzani wetu watushow hata imani kidogo tuweze kuboost up hari na kuwapindua hawa mafisadi...waungane wateue strong mtu ambaye akienda bungeni hatalala hata kidogo bali ni kuwapa majibu ya maaana na kuibua kashfa kibao za robbery wanayodo serikali yetu on our majasho....

lakini hodu yangu yaja kwenye nani wa kuteuliwa ndipo ugomvi utaanza
 
alaa zimenichanganya hizi nanii ziko mbili using same vichwa vya habari hata same wawekaji wajimini!!
for the time being kama habari ndio hiyo basi if huyo victor bado yuko fiti kupambambana na mafisadi kwa vile anajulikana na wananchi wa kule angalau so far basi apewe backup na wapinzani woote!!!
lakini kule si ndio mwa kina sumaye na usheee??ama?maana nao wakitoa fisadi strong basi mechi itakua ngumu
 
Kabuye alikata rufaa. Hicho kiti hakiwezi kutangazwa kuwa wazi hadi mwisho wa process za mahakama, including kupeleka nakala ya hukumu kwa Spika na Tume ya Uchaguzi.

Nashukuru kwa taarifa hii ndg Kiungani. . .Naomba kuuliza tena, sasa kama hali iko hivyo, jimbo hilo linakuwa halina mwakilishi bungeni au kabuye ataendelea kuwakilisha ikisubiliwa hukumu ya rufaa?
 
Nampendekeza victor agombee tena, kwanza dhamira yangu inanieleza kuwa hata hizo kidogo alizozidiwa ni baada ya ufisadi kufanya kazi, wenye habari za maendeleo ya victor watupatie hapa kama bado anamsimamo wake wa mwanzoni.

KILA NAFASI KAMA HII IKITOKEA POPOTE TANZANIA TUTAWAHAMASISHA WANANCHI HATA KWA EMAIL NA SMS
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom