Uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki kufanyika Mei 19

Hawa wehu kiwango Chao cha kichaa kitakuwa kikubwa sana yaani mtu unaona bora uchaguzi urudiwe upoteze mabilioni kuliko kuwapelekea huduma za afya na maji waliokupigia kura.
 
Lengo la JF Ni kuchangia maoni yetu sio ku assess akili Za member wenzako
Humu JF toka mwanzo kabisa kumejipambanua kama HOME OF GREAT THINKERS sasa kwa huu utahira nanyi ni ma_great thinkers? uzoba muache
 



Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage ametangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Mei 19 mwaka huu.

Jaji Kaijage ameitoa taarifa hiyo leo akiwa mkoani Morogoro ambapo ameeleza kwamba tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania.

"Nafasi ya jimbo la Arumeru ipo wazi na imetokana na aliyekuwa mbunge Joshua Samwel Nassari kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika," amesema Jaji Kaijage

Machi 14, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alimuandikia barua Mwenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage kumtaarifu jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo.

Aidha Mwenyekiti Kaijage amevitaka vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya uchaguzi wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo.

Nassari anadaiwa kutohudhuria, mkutano wa 12 wa Septemba 4 hadi 14 mwaka 2018, mkutano wa 13 wa Novemba 6 hadi 16 mwaka 2018 na mkutano wa 14 wa 29 Januari hadi Februari 9 mwaka 2019.
 
Nasari anagombea tena kulitetea Jimbo lake kupitia CCM
P
 
Nasari anagombea tena kulitetea Jimbo lake kupitia CCM
P
Hivi sheria mpya inamruhusu kuhama na kugombea tena??

Wa sukumaland
 
Namshauri Nassari aende ccm akagombee tena jimbo hilo jilo
Nasari anagombea tena kulitetea Jimbo lake kupitia CCM
P
Hivi sheria mpya inamruhusu kuhama na kugombea tena??

Wa sukumaland
 
Hivi sheria mpya inamruhusu kuhama na kugombea tena??

Wa sukumaland
kaka ccm ikiamua hakuna suala la sheria wala sharia.. na sasa hici hali halisi ilivyo ccm ndio wanaamua nani awe mbunge na nani asiwe mbunge hakuna demokrasia hili lipo wazi asilimia zote
 
Nasari anagombea tena kulitetea Jimbo lake kupitia CCM
P

Hiki kitakuwa kituko cha karne!
Mtu atimuliwe kwenye nafasi anayoshikilia kwa makosa ya kinidhamu halafu apewe tena nafasi ya kugombea nafasi hiyo hiyo hata kama ni kwa tiketi ya chama kingine?!
 
Back
Top Bottom