Uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki kufanyika Mei 19

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage ametangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Mei 19 mwaka huu.

Nasikia Nasari anajipanga kukata rufaa itakuwaje, lkn mbona NEC wamefanya haraka haraka sana ina maana wanafanyakazi hadi wikendi.
 
Kama Ni sahihi hakuna shida. Ila haki itamalaki na ionekane ikitendeka vinginevyo mbunge wa Jimbo hilo ateuliwe na dola ili tusipoteze muda, pesa na uhai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mie napendekeza serikali imteue ,Nasary sumai awe mbunge badala ya kupoteza mda na fedha bure
 
Watu wanalalamika kuwa Nasari kaonewa ila hawajui kuwa alifanya makusudi.
Ngoja aje kuwatia aibu akichukua fomu ya ccm ndio mtapoona.

Tofa
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki ni Mei 19, 2019.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 31, 2919 mkoani Morogoro amesema tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha sheria ya taifa ya uchaguzi aliitaarifu Tume kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge katika jimbo hilo.

"Nafasi ya jimbo la Arumeru ipo wazi na imetokana na aliyekuwa mbunge Joshua Samwel Nassari kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika," amesema Jaji Kaijage

Amesema amevitaka vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya uchaguzi wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo.

Machi 14, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alimuandikia barua Mwenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage kumtaarifu jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo.

Mikutano hiyo ni ule wa 12 wa Septemba 4 hadi 14 mwaka 2018, mkutano wa 13 wa Novemba 6 hadi 16 mwaka 2018 na mkutano wa 14 wa 29 Januari hadi Februari 9 mwaka 2019.

Bilioni 2 na ushee inaenda kuchomwa aisee.
 
Ujinga, ndiyomaana walifuta bunge live ili tusiwaone wabunge wetu kama wanahudhuria bungeni au la.
 
Tume ya uchaguzi imetangaza tarehe 19/05/2019 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki lililoachwa wazi na Joshua Nassari.

Source ITV habari!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom