Uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki kufanyika Mei 19

Q

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
17,925
2,000
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage ametangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Mei 19 mwaka huu.

Nasikia Nasari anajipanga kukata rufaa itakuwaje, lkn mbona NEC wamefanya haraka haraka sana ina maana wanafanyakazi hadi wikendi.
 
mekuoko

mekuoko

JF-Expert Member
Nov 15, 2012
318
250
Kama Ni sahihi hakuna shida. Ila haki itamalaki na ionekane ikitendeka vinginevyo mbunge wa Jimbo hilo ateuliwe na dola ili tusipoteze muda, pesa na uhai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
34,735
2,000
mie napendekeza serikali imteue ,Nasary sumai awe mbunge badala ya kupoteza mda na fedha bure
 
E

East African

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
597
1,000
Watu wanalalamika kuwa Nasari kaonewa ila hawajui kuwa alifanya makusudi.
Ngoja aje kuwatia aibu akichukua fomu ya ccm ndio mtapoona.

Tofa
 
Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,241
2,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki ni Mei 19, 2019.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 31, 2919 mkoani Morogoro amesema tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha sheria ya taifa ya uchaguzi aliitaarifu Tume kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge katika jimbo hilo.

"Nafasi ya jimbo la Arumeru ipo wazi na imetokana na aliyekuwa mbunge Joshua Samwel Nassari kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika," amesema Jaji KaijageAmesema amevitaka vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya uchaguzi wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo.Machi 14, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alimuandikia barua Mwenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage kumtaarifu jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo.Mikutano hiyo ni ule wa 12 wa Septemba 4 hadi 14 mwaka 2018, mkutano wa 13 wa Novemba 6 hadi 16 mwaka 2018 na mkutano wa 14 wa 29 Januari hadi Februari 9 mwaka 2019.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,743
2,000
Aliposhindwa kesi aliambiwa aeleze wananchi wake kilichotokea, ameshaeleza?
 
LIMBOMAMBOMA

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
5,828
2,000
hapo ccm wapitishe tu mgombea hakuna haja ya uchaguzi
 
Meshe

Meshe

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
234
250
Uchaguzi utakuwa haki na huru!!
Chonde Chonde Tume Mtende haki msije mkabeba dhambi bure.... kwa usemi wa Mkulu !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,457
2,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki ni Mei 19, 2019.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 31, 2919 mkoani Morogoro amesema tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha sheria ya taifa ya uchaguzi aliitaarifu Tume kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge katika jimbo hilo.

"Nafasi ya jimbo la Arumeru ipo wazi na imetokana na aliyekuwa mbunge Joshua Samwel Nassari kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika," amesema Jaji KaijageAmesema amevitaka vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya uchaguzi wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo.Machi 14, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alimuandikia barua Mwenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage kumtaarifu jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo.Mikutano hiyo ni ule wa 12 wa Septemba 4 hadi 14 mwaka 2018, mkutano wa 13 wa Novemba 6 hadi 16 mwaka 2018 na mkutano wa 14 wa 29 Januari hadi Februari 9 mwaka 2019.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bilioni 2 na ushee inaenda kuchomwa aisee.
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,801
2,000
Nassary amenichafua sana roho yangu, sitaki hata kumsikia
 
T

Twoten

JF-Expert Member
May 4, 2014
1,384
2,000
Ujinga, ndiyomaana walifuta bunge live ili tusiwaone wabunge wetu kama wanahudhuria bungeni au la.
 
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
29,980
2,000
Tume ya uchaguzi imetangaza tarehe 19/05/2019 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki lililoachwa wazi na Joshua Nassari.

Source ITV habari!
 
L

Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
3,040
2,000
nassar ahamie ccm haraka
 
Top Bottom