Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Katika hali ya kupigwa marufuku mikutano ya kisiasa nchini, kuonekana na kuimarika kwa mhimili wa Serikali katka uendeshaji wa dola na uwepo wa mfumo ule ule wa uchaguzi, uchaguzi wa marudio wa Ubunge, Udiwani, na Serikali za Mitaa haukuwa kipimo cha kukubalika au kutokukubalika kwa Serikali ya Rais Magufuli.
Siasa ni kama biashara katika kutegemea matangazo na kusikika kila wakati. Wakati biashara ikitegemea matangazo runingani na magazetini, siasa hutegemea matangazo yake kwa njia ya mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali za nchi. Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa huzalisha wanachama na wafuasi.
Kimsingi, mikutano ya hadhara ya kisiasa hubadili mtazamo wa watu na kuwafanya wabadili vyama na hata kujiunga na vyama vya siasa. Kutokuwepo kwake kunafanya kila chama cha siasa kibaki na wanachama wale wale na hata wengine kuwa wanachama 'wafu' kwakuwa vyama vyao havisikiki. Mikutano ya hadhara ya vyama vya kisiasa, kama ikiratibiwa vizuri, ni ya kujenga demokrasia, umoja na mshikamano.
Mkutano ya hadhara ya vyama vya siasa isipokuwepo, vyama vya siasa hufifia na vingine kufa kabisa. Sambamba na hilo, wananchi wanapoteza ladha ya kufuatilia siasa na kuwafamnya kutoshiriki ipasavyo katika mambo ya kiuchaguzi na kadhalika. Ndiyo maana, kila wakati idadi ya wanaojiandikisha kupiga kura na wale wanaopiga kura huzidi kuporomoka.
Kwasasa, washindi wa Ubunge, Udiwani na Serikali za Mitaa huchaguliwa na asilimia ndogo ya wananchi wao. Viongozi wa aina hii hawana baraka za walio wengi. Viongozi hawa hupata wakati mgumu katika kupanga na kutekeleza mambo ya kimaendeleo na wananchi wao. Kuna haja kuwa na siasa hai na si mfu kama ya sasa.
Iko wazi kuwa uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita si kipimo cha kukubalika kwa sera na uongozi wa Rais Magufuli wala kutokukubalika kwake. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina kazi ya kufanya katika kuwaelimisha watanzania umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura.