Elections 2010 Uchaguzi mdogo, CCM 3, CUF 3, Chadema 1

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
Chadema imetetea jimbo la Mpanda Mjini, CCM imepata majimbo ya Nkenge, Mpanda Vijijini na Magogoni Zanzibar, CUF wamepata Jimbo la Mtoni, Mwanakwerekwe na Wete.
CUF imeongeza majimbo mawili mengine kutoka Unguja.
 
Tatizo langu je NEC itagawaje vile viti maalum vya ubunge, viti sita vilivyobaki ? Nipeni hesabu.
 
Chadema imetetea jimbo la Mpanda Mjini, CCM imepata majimbo ya Nkenge, Mpanda Vijijini na Magogoni Zanzibar, CUF wamepata Jimbo la Mtoni, Mwanakwerekwe na Wete.
CUF imeongeza majimbo mawili mengine kutoka Unguja.

CUF imeshinda majimbo mengine Unguja!! Hii inazidi kutia shaka kutangazwa kwa Shein kama mshindi wa Urais Zanzibar.
 
Kwa hesabu hii inamaana CUF watakuwa na 35+ CHADEMA 43. Kwahiyo inamaana CUF wakiongeza na NCCR +TLP +UDP wanaweza kuwazidi CHADEMA?
 
Mbona matokeo haya yamewahi sana kutangazwa, leo saa 1 asubuhi kwa majira ya E.A matokeo yalikuwa tayari, mbona wa 31st yalichukua week nzima, NEC tuelezeni tuelewe.
 
hali halisi chadema inakubalika kwa wasomi tu

Nyang'ware,Mbozi Magharibi,Bukombe,Maswa mashariki, Maswa Magharibi na ukerewe kuna wasomi wengi kuliko kinondoni na Ilala ?Kama hii siyo kweli basi umeeongea pumba mtu wangu!!
 
Nyang'ware,Mbozi Magharibi,Bukombe,Maswa mashariki, Maswa Magharibi na ukerewe kuna wasomi wengi kuliko kinondoni na Ilala ?Kama hii siyo kweli basi umeeongea pumba mtu wangu!!

Mkuu hebu nitajie maeneo GANI KINONDONI yenye wasomi?.
 
Kwa hesabu hii inamaana CUF watakuwa na 35+ CHADEMA 43. Kwahiyo inamaana CUF wakiongeza na NCCR +TLP +UDP wanaweza kuwazidi CHADEMA?

Wadau mnaofahamu mahesabu haya tufahamisheni? Chadema na wale wengine (CUF, TLP, NCCR +UDP) kambi ipi yenye wabunge wengi?
 
Wadau mnaofahamu mahesabu haya tufahamisheni? Chadema na wale wengine (CUF, TLP, NCCR +UDP) kambi ipi yenye wabunge wengi?

This is bullshit! Wapinzania hawana budi kuacha tofauti zao..nilimsikia Maalim Sif akisema kama CUF walifuatwa na CHADEMA ili watengeneze kambi ya upinzani ila kwa sharti ya kutoshirikisha vyama vingine. CUF waka kataa na matokeo yake CHADEMA wakatangaza kambi yao peke yao na the rest (CUF, NCCR,TLP na UDP) wakatangaza kambi tofauti waliyoiita the minority utumbo gani sijui.

Mimi ushauri wangu wapinzani wote bado wana muda wa ku-revisit maamuzi yao ili wawe na win-win situation. Kuunganisha nguvu ni muhimu hasa kuelekea kwenye mgombea mmoja miaka ijayo. Naamini NCCR kuna vijana wazuri tu ukuinganisha na baadhi ya vichwa vilivyomo CUF plus CHADEMA wanaweza kutengeneza alliance nzuri sana. Haya mambo ya kutoiaminiana hayana maana..the most important wawe na bylaws zao na do's na dont's zoeleweke vizuri kwa washiriki wote badala ya kushutumiana na kutoaminiana bila mpango.
Yaani kama wangejipanga vizuri wangeweza hata kuleta ushindani mkubwa kwenye chaguzi za speaker.

Sheikh Yahya- Magomeni.
 
Kwa hesabu hii inamaana CUF watakuwa na 35+ CHADEMA 43. Kwahiyo inamaana CUF wakiongeza na NCCR +TLP +UDP wanaweza kuwazidi CHADEMA?

Viti maalumu hupigiwa asilimia ya kura za wabunge majimboni. Ndio maana CHADEMA walipata viti maalumu vingi zaidi kuliko CUF (23 v/s 10) japo CUF walikuwa na viti 24 na CHADEMA 22. Pamoja na ukweli kuwa waliojitokeza kupiga kura Mpanda mjini ni wachache; hata hivyo CHADEMA inaweza kuongeza viti maalumu viwili zaidi kutokana na wingi wa kura za jumla za wabnge ikiwa ya pili kwa CCM
 
Back
Top Bottom