Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,407
- 31,392
- Thread starter
- #161
Kuhusu suala la vyombo vya habari, hapa napata tatizo kidogo.Mkuu nadhani matatizo ya Trump unayoyataja ndiyo yale yale yaliyokuwa yanatajwa tangu mwanzo. Alichosema mwanakijiji ndiyo hali halisi. Kwamba vyombo vya habari vilijaribu sana kuyasema hayo kwa nguvu ili kumkwamisha trump lkn vimeshindwa,labda km watakuja na mbinu mpya ukiacha hizi zilizoshindwa.
Kwa maoni yangu na kwa wamarekani hawa walioteseka na ugaidi kipindi chote cha utawala wa obama,hakuna tena wa kumzuia Trump kuwa mrithi wa obama. Wamarekani hawatakubali kumrudisha Bill clinton ikulu kwa mara ya pili.
Trump anapenda kusikika/kuonekana katika habari kwa 'vanity and narcissism'
Haya ni mambo anayopenda yasikike, ni kwa mkakati au mazoea au tabia hatujui. Tukubaliane anapenda vyombo vya habari viwe vya kijamii au main stream.
Akiwa huko, Trump huzua 'controversy' ambazo ni chakula cha waandishi wa habari
Habari zake zinakuwa nyingi kuliko inavyotarajiwa na kuvilaumu vyombo vya habari.
Mfano mdogo, aliposhindwa na Cruz chaguzi zilizoongozana, Trump akaingiza habari za wake zao kupunguza nguvu za matokeo yaliyokuwa mabaya. Na amefanya hivyo kila mara
Kulaumu vyombo vya habari anavyovilisha habari ni jambo la kuangaliwa
Trump yupo katika uso wa jamii kama businessman na sasa Mwanasiasa.
Kuna curiosity nyingi juu yake, ni halali tu kama sehemu ya media coverage.
Kuhusu Ugaidi unaosema kwa Obama, hapa kuna vitu viwili.
i)Kuna 'lone wolf' ambao hawajulikani walipo na wanafikiri nini.
Ni mtu anaamua kama yule Meja (Fort Texas) na kuwacharanga wenzake.
Hawa lone wolf wamesababisha madhara sehemu zote kubwa duniani.
ii)Kuna ugaidi ambao ni 'organized' ndio tunayoyasikia Alshabab, Boko,ISIS, Qaeda n.k.
Unaposema Wamarekani wameteseka sana, hadi siku ya leo kuna lone wolf na siyo 'organized' ugaidi kama ule wa Sept 11, Madrid 11, London, Paris, Brussles n.k