Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Wakati kura zikiendelea kuhesabiwa kufuatia Uchaguzi Mkuu nchini Marekani, mtandao wa Twitter umetoa tahadhari kuhusu chapisho la Rais wa Marekani, Donald Trump alilochapisha katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter akiwashutumu wapinzani wake (Joe Biden) kuiba kura.
Trump aliandika: "Tunaongoza kwa kiasi kikubwa, ila wanajaribu kuiba uchaguzi. Hatutawaruhusu wafanye hivyo. Kura haziwezi kupigwa baada ya vituo kufungwa."
Twitter imetoa tahadhari kuwa sehemu au chapisho zima la Trump linaweza kuwa la kupotosha kuhusu zoezi la uchaguzi linaloendelea nchini humo.
Trump amesema kuwa atatoa taarifa zaidi baadaye.