Uchaguzi Mali: Wagombea 24 akiwemo mwanamke mmoja wanaowania kiti cha urais

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Uchaguzi Mali, Zaidi ya Raia milioni nane wajitokeza kupiga kura
Zaidi ya raia milioni nane nchini Mali wamepiga kura leo katika uchaguzi muhimu kwa taifa hilo la Sahel ambalo limekabiliwa na usalama mdogo kutokana na mashambulizi kutoka kwa makundi ya kijihadi.

Raisi wa Mali Ibrahim Boubacar Keita,mwenye umri wa miaka 71,ni miongoni mwa wagombea 24 akiwemo mwanamke mmoja wanaowania kiti cha uraisi.

Raisi Keita amekuwa akikosolewa na wapinzani wake kwa kushindwa kurejesha usalama kauli mabyo pia imeungwa mono na waliokuwa mawaziri wake ambao walikaririwa wakisema Rais huyo ameshindwa kiusalama.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutereres amesema anatiwa moyo na jinsi ambavyo kumekuwepo na amani wakati wa kampeni licha ya changamoto za usalama kwenye maeneo ya kaskazini na kati mwa Taifa hilo.

Amewataka wapiga kura katika taifa hilo lenye takribani watu milioni 18, wajitokeze kwa wingi kumchagua kiongozi wanaompenda katika hatua hiyo muhimu ya kidemokrasia.
 
Back
Top Bottom