Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,555
- 119,066
Salaam wanabodi,
Uchaguzi wa marudio katika majimbo 7 yaliyobakia unafanyika Jumapili hii, ambapo Chadema iko kwenye hatihati ya kulipoteza jimbo la Mpanda Kati kwa CCM, wakati CUF itajivunia majimbo mengine 3 ya Wete ambalo ni lao, lakini pia watavuna jimbo la Magogoni na Mtoni.
Hii ni tathmini yangu ya hali halisi kwa mujibu wa matokeo ya kura za urais kama ifuatavyo...
Jimbo ................KIKWETE (CCM) ................Dr. SLAA (CHADEMA)............. Prof. LIPUMBA(CUF) ......Mshindi
Mpanda Urban 9,526 (57.11%) ....................6,523 (39.11%) ........................168 (1.01%) ......................CCM
Mpanda Rural 7,817 (62.87%) .....................3,669 (29.51%) ........................378 (3.04%) ......................CCM
Nkenge.......... 26,836 (63.78%) ..................13,593 (32.31%) .......................276 (0.66%) .....................CCM
Mwanakwerekwe 1,646 (51.23%) ...............32 (1.00%) ..............................1,416 (44.07%)................. CCM
Mtoni ................2,417 (37.74%) ................139 (2.17%) ............................3,492 (54.53%).................. CUF
Magogoni .........4,606 (46.93%) ..................94 (0.96%) .............................4,791 (48.82%).................. CUF
Wete.............. 1,293 (16.18%) ...................64 (0.80%) .............................6,354 (79.51%) ...................CUF
Namna pekee ya kulilinda jimbo la Mpanda Kati lisiangukie mikononi mwa CCM ni kwa wale walioko Mpanda kati na hayo majimbo mengine ya Mpanda Mjini na Nkenge, kupigiwa kwa nguvu zote lile tangazo la Utajiri wa Tanzania, kwa nini sisi ni masikini, na lile tangazo jingine la Tamwa la 'Dudu liumalo usilipe kidole', lisambazwe nyumba kwa nyumba, vinginevyo Uchaguzi huo, ni kuhalalisha tuu uchakachuaji uliokwishwa tendekeka.
Kwa upande wa CUF, ushindi ni dhashiri, kwa sababu ya tofauti kubwa kati ya mgombea wa CCM na yule wa CUF, hata wachakachue vipi, kura bado zinabaki za kutosha!.
Kwa wale wapenzi wa Chadema, naombeni sana, msinishambulie mimi, shumbulieni hoja niliyoiweka na data na sio kumshambulia mtoa hoja!.
Angalizo: Ushindi wa Chadema bado unawezekana, kama wananchi wa eneo hilo wanaweza kuwa wamempa kura nyingi JK kama rais wao, lakini wakanyima kura mbunge wa CCM au vise versa kama walivyofanya wapiga kura wa Bokoba Mjini, wamempa kura nyingi Dr. Slaa kwenye kura za urais, halafu wakanyima kura mgombea wa Chadema kwenye ubunge na bado wakampigia kura nyingi mgombea wa CCM!.
Nawasilisha.
Pasco.