Uchaguzi leo TUCTA: Ni wakati wa kukata mzizi huu dhaifu!

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
Wadau huwa tunalaumu makofi yasiyo na Tija Bungeni.

Sasa leo ndio nitaamini kama ile research iliyosema panapo watu wanne mmoja ni hamnazo.

Kwanza suala la fao la kujitoa linaathiri vibaya sana sector yotote binafsi ktk nchi ya uchumi huu unaofanyiwa ukarabati.

Inashangaza sana kuona wao ndio walipendeza fao jipya la kukosa ajira kama mbadala wa kujitoa wakati wanajua wazi kuwa, kwa mujibu wa ILO fao la kukosa ni allowances wanayopewa ambao hawajapata kazi hivo serikali inabidi iwalee.

Mfanyakazi ambaye amefanya muda mrefu na kazi yake kukoma kwa namna yoyote akitaka kujitoa ktk fao ni ahueni kwa nchi maana ataanzisha mgahawa au mradi wowote na kuajiri wengine huku akiacha NAFASI wasio kazi kuingia ktk ajira na NGUVU mpya MAWAZO mapya na MBINU za kisasa.

Kuendelea kurundika watu wasubiri miaka sitini matokeo yake zile pesa wanazipata na hawawezi kuzisimamia.

Sema kweli TUCTA haina tija kama shirikisho iwapo leo watawapitisha hao wasiliti ambao kiuhalisia ni wabunge wa tarajiwa kwa hiyo ni makada.

Kuna vyama vingi vinaumia kwa mawazo finyu pendekezwa, ni dhahiri pasipo shaka leo ndio mtakata mzizi huu dhaifu.

Vyama vya wafanyakazi vimekuwa matawi ya vyama vya siasa, fanyeni jambo na sisi tuone kuwa tunawawakilishi.

Shukrani
 
Huyu Mgaya kuna kipindi alikaza mpaka JK akaja na msemo wa mbayuwayu na akili za kuambiwa .....????
 
Huyu Mgaya kuna kipindi alikaza mpaka JK akaja na msemo wa mbayuwayu na akili za kuambiwa .....????

alitulizwa huyo, Mwaka jana aligombea ubunge kupitia chama changu akapigwa chini kura za maoni.

Saizi hakuna kuremba aamue atembeee ahamie rasmi kwenye majukwaa hata ualimu hatafanya umri umekwenda
 
Utamtoa ukiwa Jamii forums au kwa kupiga kura

Katika kada ya ajira yako una chama kinachokuwakilisha ktk uchaguzi.
Mfano:
Waandishi wa habari.ule mswaada ulipitishwa juzi TUCTA wangesimama kidete usingepita.

Ishu ya fao la kujitoa balaa lake ni vyama vyote sekta binafsi vitaumia maana hakuna security kazini
 
Nguvu ya kura itaamua kama Mgaya must go or Stay in

Ni kipimo kizuri cha wawakikishi wetu ktk vyama mbalimbali kama wanawaza sawasawa.

Hao Jamaa wanapesa na wanaweza kutumika pia ili baadae Mipango miswaada mibovu ipite.

Wajichanganye wa kwa utamu wa jojo, watatuuumiza sisi tunaokatwa michango kila mwez
 
Atabaki, ungejua Watanzania ni watu wa aina gani usingesema hayo. Mgaya na Mkoba wanalindwa na system, wanayotumikia Serikali sio wanachama.

Atashinda tena kwa kishindo, Mkoba hata walimu wasipomchagua atashinda, Kumbuka ya Jecha
 
Fao lakujitoa jamani ni muhimu sana................mie nadai 28,000,000/= na nina miaka 36 muda huu....na mkataba wangu umebakiza miaka 2 tu sasa niake mpaka baada ya miaka 17 ndo nipewe hiyo fedha jamani sijui kama nitakuwepo mwenzenu
 
Fao lakujitoa jamani ni muhimu sana................mie nadai 28,000,000/= na nina miaka 36 muda huu....na mkataba wangu umebakiza miaka 2 tu sasa niake mpaka baada ya miaka 17 ndo nipewe hiyo fedha jamani sijui kama nitakuwepo mwenzenu
We jamaa kila kitu na wewe kinakuhusu duu
 
Fao lakujitoa jamani ni muhimu sana................mie nadai 28,000,000/= na nina miaka 36 muda huu....na mkataba wangu umebakiza miaka 2 tu sasa niake mpaka baada ya miaka 17 ndo nipewe hiyo fedha jamani sijui kama nitakuwepo mwenzenu

Yaani kwa kweli inauma sana, umelipa PAYE 30%, NSSF 10%, chama cha wafanyakazi 2%, HESLB 15%


More than 60% wanabeba hii ni dhuluma
 
Kama unajua maana kura za kidemokrasia usipopiga utaamuliwa na waliopiga.

Maamuzi watakayofanya leo yatatugarimu sote

Mkuu kwa upuuzi Wetu wafanyakazi hao jamaa watabaki...jiulize mkoba ni raisi Wa CWT kwa mihula mingap? kwani wanachama tunampenda?

ndio upuuzi Wa demokrasia Mkuu kama ulivyosema..itatugharimu sote!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom