MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Katika Uchaguzi wa Ubunge mwaka 2015, Maulid Mtulia akiwa CUF yenye UKAWA alipata kura 70,300 wakati Idd Azzan wa CCM alipata kura 66,000.
Hizi ni kura ambazo zilijumuisha Vyama vinne ndani ya UKAWA.
Leo hii UKAWA ni historia kwa sababu hata salamu za NCCR-Mageuzi hazisemwi achilia mbali uwepo wa bendera ya NCCR-Mageuzi katika mikutano ya CHADEMA.
Sina shaka kura za CCM ziko palepale kutokana na historia ya CCM inayobainisha chama kushikamana pale kimapoingia kwenye mapambano/chaguzi.
Anayedhani kuwa kuna wanaCCM wengi watampigia kura mgombea wa CHADEMA lazima atakuwa hajui historia ya CCM.
Ninajua Mtulia ameenda CCM na kundi lake kwa kiwango kikubwa kutoka CUF huku CHADEMA wakibaki kuvutana na kundi lililompigia kura Mtulia wakati akiwa UKAWA.
Sio uwongo kuwa Kinondoni ilikuwa ngome ya CUF.
Historia inaonyesha kuwa mwanaCUF kindaki ndaki hawezi kuipigia CHADEMA kura infact, ni bora aipigie CCM kuliko CHADEMA.
Mbaya zaidi, Kinondoni ina wazee wengi kuliko vijana. Utafiti unaonyesha hili ni kundi ambalo linapiga kura mara nyingi kwa CCM au CUF.
Kutokana na uwepo wa wazee wengi Kinondoni ndio maana kampeni za CCM zitafungwa na Mzee Makamba.
Kwa mantiki hii, sioni CHADEMA wakishinda katika jimbo la Kinondoni.