Uchaguzi Kenya: Lowassa alienda kama mwanachadema au mmasai?

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Kampeni za urais nchini Kenya zikiwa zimepamba moto, huku wagombea urais nchini humo na kambi zao wakiwa katika hatakati na mchuano mkali .

Wagombea urais wa nchi hiyo hasa wawili wenye wafuasi wengi na ushawishi mkubwa sana ambao ni Uhuru Kenyatta ambaye ni rais anaetetea kiti chake na Raila Odinga ambaye ni mgombea mzoefu na pia waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, wakinadi sera zao na moja ya mambo makubwa yaliyozungumzwa na wagombea wote na kuzungumzwa sana ilikua ni suala la ukabila na ufisadi.

Kampeni hizi ambazo kuanzia ngazi ya chini kabisa ya uongozi zilitawaliwa na jina la Rais wa Tanzania,mhe J.P.J.Magufuli kama kioo cha kujilinganishia.Kila mgombea alisema atafanya kama Magufuli afanyavyo iwapo atachaguliwa kiasi cha kuvaa mavazi na kubeba mabango yenye jina la Magufuli.

Lakini kwenye moja ya mikutano mikubwa iliyofanywa na kambi ya Uhuru Kenyatta alionekana mgombea urais alieshindwa kwenye uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2015 nchini Tanzania na waziri mkuu aliyewahi kukataa haki yake ya kujieleza kwenye tuhuma za ufisadi wa Richmond na kuamua kukimbia,ndugu Edward Lowassa.Ndugu Lowassa alionekana jukwaani hapo sambamba na ndugu Kenyata, Ruto na watu wengine waliovaa mavazi ya kimasai,na yeye pia alivaa mavazi ya kimasai.

Swali: Je, ndugu Lowassa ambae ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo nchini Tanzania, alienda kwenye kampeni hizi kama mwanachadema au kama mmasai?

Tafakuri: Kama alienda kama mwanachadema,kwa nini hakuvaa mavazi ya chadema? Na wala hakusema kuwa chadema imemtuma kwenye hilo?

Lakini pia chadema wenyewe kupitia kwa uongozi wake wa ama mwenyekiti wao bwana Freeman Mbowe au katibu mkuu wake bwana Dr Mashinji au msemaji wa chama, hawakuwahi kutoa tamko lolote la kichama kuwa chama hiko kimetuma mwakilishi kwenye kampeni za urais nchini Kenya ili kuunga mkono upande mmoja dhidi ya mwingine!!!!

Na kama alienda kama mmasai au kiongozi wa watu wa kabila la wamasai,kama ambavyo mavazi yake na mavazi ya wengine walioonekana pamoja na yeye yalivyoonyesha,je;

1:Alitumwa na wamasai?

2: Huu ni msimamo wa jumla wa wamasai wote Tanzania?

3:Je,kambi ya Rais Kenyata ilihitaji uungaji mkono wa makundi ya kikabila,huku
wakinadi kupinga ukabila?

4:Na je, kwa taswira hii iliyoonyeshwa na Ndugu Lowassa ambae ameshatamka
Kuwa atagombea tena urais mwaka 2020, kama watanzania tujiandae na harakati za Kikabila?

5:Ni picha gani dunia inaipata kutoka uhusika siasa za Tanzania kwa mwakikishi wa moja ya vyama vikubwa kabisa nchini

(a) Kwenda kuingilia harakati za chaguzi za nchi jirani(nchi nyingine)

(b) Kidiplomasia baada ya uchaguzi kama nchi tutakua kwenye nafasi
gani kama nchi na mahusiano yetu na Kenya?

(c) Endapo wakati wa uchaguzi kukitokea vurugu zenye mrengo wa kikabila,
Je, nani atabeba mzigo wa lawama wa maafa ya maisha ya watu na mali zao?

Tanzania na Kenya ni majirani na ndugu,uhusika huu wa lowassa na au chadema na au wamasai hautaleta athari katika mahusiano na jirani zetu na jumuia ya Afrika Mashariki kwa jumla?

Kuna haja ya kuweka tofauti zetu za kiitikadi pembeni na kuukabili ukweli na kukemea yote yenye dalili ya kuleta madhara kwetu au kwa jirani zetu, ikitokea uhusika wa Lowassa ukasababisha kuvurugika kwa amani,nani atabeba mzigo wa wakimbizi?

Najaribu tu kuwaza kama mtanzania na kama binadamu! Huku Kwetu ligula,tunasikiliza tu.
 
Kenyatta alihojiwa na vyombo vya habari kuwa kwa Nini alimwalika mtu mwenye tuhuma za ufisadi lowasa kwenye mkutano wake? Kenyatta aliwajibu kuwa yeye Lowasa alijileta mwenyewe hakumwalika
Lowassa akawaambia Wakenya,"kura kwa uhuru,kura kwa nani?"
Wananchi wakajibu: "Kwa uhuru"!!!!!!!!!!
Yametimia!!!!!!!!!!!!!
Hongera Uhuru,kwa niaba ya Rais wa JMT,watanzania wote na mimi mwenyewe nakupongeza sana!
 
5c4d35e39506d91f57b5c18b63fbe5cd.jpg
 
Kenyatta alihojiwa na vyombo vya habari kuwa kwa Nini alimwalika mtu mwenye tuhuma za ufisadi lowasa kwenye mkutano wake? Kenyatta aliwajibu kuwa yeye Lowasa alijileta mwenyewe hakumwalika
heeeeeeeeeeee!!!!!
 
kumbe tz na Kenya ni ndugu Sasa kama Lowassa kaenda kuna shida gani mtu kumtembelea nduguye? Au wewe ulitakaje? mleta mada ni mpuuzi kila ukihema
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom