Uchaguzi kata 46 tulianza na mungu na tutamaliza na Mungu

daza steven

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
359
357
Hili neno silisikii siku hizi sijajuwa kwanini.

Kwa huu uchaguzi mdogo wa madiwani unaoendelea ni kipimo tosha kwa walioanza na mungu na kumaliza na mungu kwa ushindi wa kishido. Miaka miwili ya serikali ya JPM kunaonekana mabadiliko makubwa hadi wengi tunabaki midomo wazi kwa kushangaa kwani kunafanyika mabadiliko ya haraka sana ya kasi na muda mfupi.

Ni kweli Chadema walianza na Mungu na kumaliza na Mungu?
Jibu ni kweli walianza na Mungu lakini tumeona wameshindwa kumaliza na Mungu. Ikumbukwe kuwa msemo huu ulikolea mwanzoni mwa miaka ya 2007 na ilikuwa ni kweli.

Mungu alionekana Chadema kwa macho ya nyama kwani kuanzia 2005 chama kilikuwa kikikuwa kwa kasi sana, chama kilizidi kuenea mijini na vijijini, kona zote za Tanzania zilisikika Chama Cha Democrasia na Maendeleo Chadema (CHADEMA) (MAKAMANDA)

Mungu aliwaongeza wabunge na madiwani wa kuchaguliwa, waliongezeka uchaguzi hata uchaguzi, Mungu alikaa ndani ya chadema na kutulia na mafisadi walikuwa maadui wakubwa kwa Chadema. Fisadi hakusogelea Chanema wala kuweka pua yake, Watanzania walimpenda Mungu wa Chadema kwani alionekana kwa macho na watu walijiunga na chama cha Democrasia na maendeleo (CHADEMA) kila ilipoitwa siku.

Ilifika wakati kadi za chama cha Chadema zilikuwa dili maana ilikuwa demand over supply, kwani bei ya kadi iliyowekwa na chama ni 1500/- lakini sokoni ilifika hadi 3500/- nahili halijawai kutokea katika chama chochote cha siasa Tanzania iwe CCM, CUF, UMD, Chama cha LUNGWE, ACT WAZALENDO, NCCR Mageuzi wala chama cha Mapesa Cha Cheyo kadi kuhitajika kiasi kile, Yaani huyu hakuwa mtu, ila alikuwa ni Mungu wa Chadema na Mungu wa kweli. Leo hii ukipewa kadi ya Chadema na BUKU juu mtu anachomoa.

Je. Mungu wa Chadema yupo au kalala au aliondoka?

Jibu ni kuwa Mungu aliondoka, kwa sababu mungu hapendi kukaa na wezi ndiyo maana Chadema waliwapokemea wezi na mafisadi, Mungu hakai sehemu chafu, na aliamua kuondoka baada ya chama kubadilika na kuwapokea mafisadi na wezi na kuwasifu na kilianza kuwatetea wezi waziwazi bila hata kuficha na hapo ndiyo mungu alipo amua kuondoka na shetani kuingia.

Tukumbuke kuwa Mungu anapenda TOBA lakini hata toba wale mafisadi walikataa walihama na zambi zao na kuingia nazo Chadema. Na kugundua kuwa mungu alikuwemo Chadema, chama kilikuwa na viongozi wa dini wengi kama Prof. Safari, Dr Slaa na wengine wengi kama mchungaji Msigwa lakini shetani ananguvu ni Dr, Slaa ndiyo alisema, aina noma waje ila wafanye TOBA yaani wajisafishe kabla ya kuingia. Matokeo yake Dr. Slaa alionekana ni mbaya sana.

Sasa tukubaliane shetani akiingia naye anafanya kama Mungu ila yeye baada ya muda mfupi hali inakuwa mbaya sana hata kidogo kilichokuwepo kinaondoka.
Na mungu aliwaongoza Chadema kuwataja mafisadi kwa majina na ufisadi walioufanya kwani hakuna kabla ya hapo aliyekuwa anawajuwa mafisadi na ushaidi mungu alisaidia kupatikana, Makamanda waliwataja kwa majina mafida na ushahidi ulitolewa kwauwezo wa mungu.

Mfano. Tundu Lisu alisema Ccm kumpa Lowasa bendera ya kugombea uraisi katika nchi hii ni hatari. Sasa tujiulize Mh. Tundu Lisu ana dabo standadi? Jibu ni hapana Tundu Lisu yupo vizuri ila shetani kapewa nafasi kubwa kwani Tundu Lisu ni msomi tuna mwamini na kauli yake ya kwanza ambapo mungu alikuwepo naye ndiyo yakweli.

Sasa tunaona tena kwa macho Mungu kaamia kwa serikali ya awamu ya tano, maana mafisadi wanakosa raha ndani ya Chama Cha Mapinduzi hata raisi kutangaza kuwa wale mafisadi ambao wako Ccm uchaguzi ujao watafute vyama vya kugombea na siyo CCM.

Hivyo CHADEMA wategemee kupokea mafisadi wengi kama Ngereja, Vijisenti na wengine wengi kwani kwa sasa huku hawana nafasi.

UTABILI.
Kwa kuwa Mungu aliachwa na CHEDEMA na shetani akakaingi na ule msemo haupo tena wa kusema TULIANZA NA MUNGU NA TUNAMALIZA NA MUNGU na kukemea ufisadi ukiwa chadema kwa sasa nikuhatarisha kadi yako, natabiri kwa jina la mungu aliyekuwepo chadema kuwa katika kata 46 zinazo gombewa wakipata kata 6 wapige magoti.

Nawasilisha
Mzalendo Daza
0714 733 111.
 
Umeongea point na ukweli unaojulikana lkn usiokubalika(wanajua ila hawataki)
Uchaguzi utakuwa kipimo tosha.

Ngoja nikae pembeni kuona mapovu.
 
Back
Top Bottom