Uchaguzi Jimbo la Kalenga: Vitus Lewa mwana wa Kalenga umma unakuhitaji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Jimbo la Kalenga: Vitus Lewa mwana wa Kalenga umma unakuhitaji!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Bw.Daffa, Feb 4, 2014.

 1. Bw.Daffa

  Bw.Daffa JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2014
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 422
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Habari WanaJF,

  Bila shaka Wanachi wa Kalenga wanasubiri kwa hamu List ya Wagombea kupitia vyama mbalimbali,ktk uchaguzi mdogo wa ubunge utakaofanyika mapema mwezi Machi.

  Ama kwa upande wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) bila shaka kuna makamanda tayari wameshatangaza nia ya kugombea ubunge,miongoni mwao ni Mwl.Vitus Lawa.

  Huyu ni kamanda ambaye ameongoza harakati hasa kanda ya kaskazini(hivyo namfahamu vilivyo)
  Pengine Jina VITUS LAWA likawa geni wa baadhi yetu,basi kama ni hivyo;
  VITUS LAWA ni Mwalimu aliehitimu shahada yake pale Mwenge Univesity. Kwa kuwa alipangwa kikazi maeneo ya Lushoto hivyo harakati alizifanyia kanda ya kaskazini.

  Bw.Vitus Alianza harakati za kisiasa mwaka 2010 akisimama kama mshauri mwezeshaji Kwa wagombea wa Udiwani na Ubunge wilaya ya Lushoto kupitia Chadema. Alihusika pia kwenye uanzishaji Na ufunguzi wa ofisi mbalimbali za chama ikiwemo kuandaa mikutano ya Chama.

  Kwa kifupi,huwezi kutaja maendeleo ya Chadema Lushoto bila kumtaja Mwl.Vitus Lawa kwani kwa sasa ni bado ni mshauri Chadema Lushoto na akiwa kama mlezi wa chama Kata ya Ngwelo.

  Ama kwa upande wa Wilaya ya Simanjiro alisimama kama wakala wa chama kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki uliomuingiza kamanda Joshua Nassari bungeni.

  Pia amekua mjumbe wa sera,utafiti na Irani ya Chama kanda ya kaskazini.

  Nyota njema huonekana Asubuhi, Kwa wale Mlio soma Chuo kikuu cha Mwenge kati ya mwaka 2010-2013 mtakubaliana ma mimi kwamba Bw.Vitus Lawa amekua mshauri wa baraza la wazee,akisimamia ushawishi wa Chama kwenye serikali ya wanafunzi na Ngazi nyingi
  kwa Upande wa Kalenga alianza harakati tangu mwaka jana hivyo bila shaka baadhi wanatambua mchango wake.

  Ni Mwaka jana alipotangaza nia yake kwa maandishi akiomba Wanachama wenzake kumpa ridhaa ya kuwa Mrithi wa nafasi ilochwa wazi na Dkt.Mgimwa aliefariki.

  Sisi watu wa kanda ya kaskazini kwa kweli tunaamini Chama kitampa ridhaa na hivyo kumpa nafasi ya kukomboa wana KALENGA

  Kila la kheri Bw.Lawa
   
 2. House of Commons

  House of Commons JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2014
  Joined: Oct 1, 2013
  Messages: 1,683
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kila la heri...
   
 3. MFUKUZI

  MFUKUZI JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2014
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Umemueleza vizuri hujo bwana Lewa na jinsi alivyopiga kazi huko Kanda ya Kaskazini...Swali, vipi huko Kalenga Iringa anamtaji wa watu!!?? kwa ninavyowajua wahehe kama kijana alikupa kisogo kwao kaumia kwa wale jamaa!!
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2014
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Unajipigia debe,haya mkuu tumekusoma
   
 5. Bw.Daffa

  Bw.Daffa JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2014
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 422
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Usijali mkuu, kama nilivyobandika hapo juu,najaribu kuwapa Wana Kalenga ninayoyafahamu kuusu uyu bwana..naamini pia watakuepo wanaomfahamu zaidi yangu..zote kheri
   
 6. kutwamara3

  kutwamara3 Senior Member

  #6
  Feb 4, 2014
  Joined: Jul 16, 2013
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe ndio kamanda vitus,tumeishakufahamu!
   
 7. L

  Lilambo JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2014
  Joined: Jun 5, 2013
  Messages: 2,526
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mh! Kalenga! Huyu jamaa nahisi atakula za uso! Yaan kaskazini tu kaskazini tu mh! Kila la kheri.
   
 8. L

  Lilambo JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2014
  Joined: Jun 5, 2013
  Messages: 2,526
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ingekuwa vizuri akagombea tu huko anakofahamika zaidi... Maana huku Kalenga Imigo Iva Ngomi....
   
 9. Bw.Daffa

  Bw.Daffa JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2014
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 422
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwa kiasi flani uko sahihi mkuu,ila kama nilivyokuja kueleza pale juu kuwa Alishiriki Jimboni kalenga tangu mwaka jana na Kumbuka Alkua yupo kikazi kanda ya kaskazini ni kawaida watu wanatoja hata marekani kuja kugombea nafasi kikubwa awe na Nia thabiti ya kukomboa wananchi..Tusiamini hivyo mkuu
   
 10. kyoma kulala

  kyoma kulala Member

  #10
  Feb 4, 2014
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  safi sana mheshimiwa LAWA! nakumbuka ulitangaza nia mapema kwamba 2015 uko ulingoni,ila ya Mungu mengi,kinyang,anyiro kimekuwa karibu,wana Kalenga mpeni kura Mwl LAWA atawawakilisha vyema!
   
 11. mwaikenda

  mwaikenda JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2014
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha Kuzingua Mwenge ndiyo Chuo gani...Tunataka wa UDSM
   
 12. chikutentema

  chikutentema JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2014
  Joined: Dec 10, 2012
  Messages: 6,411
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Kila la kheri kamanda Lawa
   
 13. T

  The Name JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2014
  Joined: Jan 30, 2014
  Messages: 812
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  kama ana nia njema big up!
   
 14. n

  nkongu ndasu JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2014
  Joined: Jan 19, 2013
  Messages: 22,474
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Ana uwezo wa kugawa ngawira kwa wahehe? Teh teh, natania tu! Kila la heri kamanda!
   
 15. East African Eagle

  East African Eagle JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2014
  Joined: Jul 26, 2013
  Messages: 3,768
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  CHADEMA mmewackoza wahehe.Hata siku 40 toka marehemu afariki za maombolezo hazijaisha mmeanza siasa mjiandae kupokelewa na marungu na mikuki kutoka kwa wanakalenga.
   
 16. z

  zwangendaba2014 New Member

  #16
  Feb 5, 2014
  Joined: Jan 13, 2014
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Evaristo Mtitu upo wapi?
   
 17. S

  SHILLINGS Senior Member

  #17
  Feb 5, 2014
  Joined: Oct 24, 2013
  Messages: 108
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kuweka kumbukumbu sawa Kamanda Vitus Innocent Lawa (Mtoto wa Walimu) ameshiriki kwa kiasi kikubwa kujenga jimbo la Kalenga kupitia programu ya "CHADEMA NI MSINGI".Pamoja kuwa mwalimu anatumia muda anaopata kushiriki katika ujenzi wa chama.

  Kamanda Vitus Innocent Lawa ni mzizi imara ukilinganisha na wagombea wengine kwa kuwa na mtaji mkubwa wa kisasa kutokana na historia yake na wazazi wake.Ni kamanda aliyekulia kwenye familia ya walimu,Wazazi wake wamefundisha shule mbalimbali za jimbo la Kalenga, ametokeo kwenye ukoo wenye historia kubwa kwa wananchi wa Kalenga. Naamini atapeperusha vizuri bendera ya CHADEMA.
   
 18. S

  SHILLINGS Senior Member

  #18
  Feb 5, 2014
  Joined: Oct 24, 2013
  Messages: 108
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Vitus Innocent Lawa amezaliwa Iringa,amekulia Iringa, ni mtoto wa Iringa jimbo la Kalenga.Pita maeneo ya Ifunda,mgama,kalenga,wasa na nzishi ulizia Mwl.LAWA jibu linapatikana. Ni Kamanda mwenye jina jimbo la Kalenga.
   
 19. S

  SHILLINGS Senior Member

  #19
  Feb 5, 2014
  Joined: Oct 24, 2013
  Messages: 108
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Anacheza ngoma anayoijua,huyu ni mtoto wa Kalenga
   
 20. Bw.Daffa

  Bw.Daffa JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2014
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 422
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Naaam ndio uzuri wa JF,
  Mkuu Shilings umenena vyema bila shaka kwa watu wa Iringa mna mengi ya kusema kuhusu Kamanda Lawa.
   
Loading...