Uchaguzi Igunga: DC apata kisago kutoka kwa wana- CHADEMA

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,016
649
Punde nimepokea habari kutoka Ingunga kuwa DC wa wilaya hiyo kapata kipigo kutoka kwa wana chadema waliomtuhumu kuhusika katika njama za kuwahujumu katika moja ya mkutano.

UPDATE ONE VIDEOUPADE TWO-NEWS STORY
Chadema wamkamata Mkuu wa Wilaya Igunga

VURUGU zimezuka jana katika Kata ya Isakamaliwa, wilayani Igunga zikiwahusisha viongozi wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.Katika sakata hilo, wanachama wa Chadema walimkamata Mkuu huyo wa Wilaya kwa tuhuma za kuendesha mkutano wa ndani na watendaji wa serikali za vijiji, wakati akijua kuwa kulikuwa na mkutano wa kampeni za chama hicho karibu na eneo hilo.

Msafara wa Chadema ulifika katika eneo la kampeni saa 8.00 mchana na kabla mkutano haujaanza, Meneja Kampeni wa chama hicho, Sylivester Kasulumbai, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa wilaya ya igunga alikuwa akifanya kikao cha ndani katika eneo hilo kinyume na taratibu, hivyo wanakwenda kumshughulikia.

Kasulumbai ambaye ni Mbunge wa Maswa Mashariki akiwa na Mbunge wa Viti Maalum, Susan Kiwanga, baadhi ya wananchi na vijana wao, walifika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata kulikokuwa kunafanyika mkutano huo na kuanza kuhoji aliko Mkuu huyo wa Wilaya.

Mmoja wa wananchi alimnyooshea kidole mama ambaye alikuwa amekaa mbele na kusema; "..yule ndiye Mkuu wa Wilaya".Kundi hilo la vijana na viongozi wa Chadema, waliingia katika ukumbi huo na kumtoa nje mama huyo huku wakimtaka aeleze kwa nini anafanya vikao vya ndani katika Kata hiyo wakati anajua kuwa chama hicho kilikuwa na mkutano katika eneo hilo.

Kitendo hicho kilizua purukushani na kutokuelewana kati ya waliokuwa kwenye mkutano wa ndani na viongozi wa Chadema, jambo lililovuta umati mkubwa wa watu.

Maelezo ya DC
Baadhi ya vijana wa Chadema walikuwa wamewashikilia watu waliokuwa wakishiriki mkutano huo huku mama huyo akitolewa nje na kuketishwa kwenye kiti alitakiwa atoe maelezo kuhusu mkutano wake.

Baada ya kukaa kwenye kiti huku akionekana kuchanganyikiwa, alisema yeye ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga, jina lake ni Fatma Kimario na kwamba, hakuwa na taarifa za mkutano wa kampeni za Chadema.

"Sina ratiba, iko katika ofisi za halmashauri, hivyo sikujua kama kuna mkutano hapa, hata hivyo watu walikuwepo niliwaruhusu waende mkutanoni na mimi nilikuwa naondoka sasa hivi," alisema na kuongeza:

"Nilichokuwa nafanya ni mkutano wa viongozi wa serikali kwa ajili ya kuangalia hali ya mifugo inayoibwa sana, elimu kwa wote hasa watoto na ujenzi wa nyumba bora na masuala ya amani".

Kimario aliwasihi wafuasi wa Chadema kusoma karatasi ya ajenda ili wafahamu kilichokuwa kikijadiliwa kwenye kikao hicho.

Karatasi aliyokuwa akiizungumzia Mkuu huyo wa Wilaya ilikuwa na ajenda tano za kikao hicho ambazo ni; Uhamishaji wa mifugo; Kuwa na choo chenye ubora na nyumba bora; Elimu; Mipaka ya shule na ajenda ya mwisho ilikuwa Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga.

Hata hivyo mbunge Kiwanga alimtaka mkuu huyo wa wilaya aeleze tangu lini kikao cha viongozi wa serikali kikahudhuriwa na wazee maarufu na mabalozi wa nyumba kumi, swali ambalo lilionekana kumchanganya mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa majibu tata.

Mkutano wa Chadema
Wakati hayo yakiendelea, mkutano wa kampeni ulikuwa nao ukiendelea, hivyo viongozi hao wa Chadema walimtaka DC huyo afike kwenye mkutano huo ili aweze kuonana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Kimario alikubali, lakini akataka dereva wake atangulize gari na kwamba yeye angefuata. "Nitakwenda kwani napaswa kuwepo pale kama msimamizi wa usalama, sijahudhuria mkutano wowote hivyo nitakwenda," alisema.

Akizungumzia tukio hilo kwenye mkutano wa kampeni, Dk Slaa alisema wakuu wa wilaya na mikoa kufanya mikutano wakati wa kampeni ni kinyume cha sheria, hivyo Kimario alienda kuanzisha vurugu.

"Hapaswi kufanya mkutano wowote hapa hasa akijua kuwa sisi tuna mkutano wa kampeni na yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Wilaya," alisema Dk Slaa na kuongeza:

"DC anafanya nini huku wakati hiki ni kipindi cha uchaguzi au ndiyo wanapanga mikakati ya uchakachuaji halafu wanadai sisi ndiyo tunaofanya vurugu?"

Mkutano wa kwanza na wa pili wa Chadema, hakukuwa na ulinzi wa polisi kama ilivyokuwa kwenye mikutano mingine.

Askari wamwagwa
Wakati gari la waandishi wa habari likirejea mjini Igunga, lilipisha na magari mawili ya polisi yakiwa yamejaa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambayo yalikuwa katika mwendo kasi yakielekea eneo la tukio.

Magari hayo yalifuatiwa kwa nyuma na gari aina ya Toyota Landcruiser ambalo lilikuwa na vioo vyeusi yote yakiwa yamewasha taa kuashiria hali ya hatari.

Hata hivyo polisi wilayani Igunga kupitia kwa Mkuu wake (OCD), Issa Maguha, waliliambia Mwananchi kuwa hawakuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba magari hayo yalikuwa katika doria za kawaida.

Chanzo-Mwananchi
 
Last edited by a moderator:

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Kwanza walianza kutumwagia tindikali sasa wameanza kuwapiga viongozi wetu wa nchi na mwisho wataanza kurusha mawe ikulu. Hili halikubaliki na lazima wafungiwe kufanya kampeni kabla ya uchaguzi ili washike adabu. Narudia tena, hili halitavumiliwa.
 

John Marwa

JF-Expert Member
May 25, 2011
275
28
Mungu ilaani Chadema,walaani Viongozi na wanachama wote wanaoleta uvunjifu wa amani! Walaaniwe kabisa!
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Mnahubiri vita, siku watu wetu wakawajibu mtatafuta pakutokea

Kuna mambo ccm wameasisi lakini sina hakika kama walikaa chini na kufikiria madhara yake. 'Mfumo' wa kuandaa vijana (Green Guard) matokeo yake ni ndio haya ya DC kupigwa. Watu wamechoka na siasa za ubabaishaji na pale wanapodai mabadiliko ccm inaonekana kutumia mabavu. Kuchapwa kwa DC (kama ni kweli) ni alama tosha kuwa yeyote atakayeshiriki (directly & indirectly) kuminya haki na madai ya wananchi ya kutaka mabadiliko basi anakuwa kwenye kundi la 'kuchapwa' viboko. Ma-DC na wakuregenzi wamekuwa na tabia ya kuvuruga watu, sasa nguvu ya umma imeamua enough is enough. Green Guard was a mistake!
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Kwanza walianza kutumwagia tindikali sasa wameanza kuwapiga viongozi wetu wa nchi. Mwisho wataanza kurusha mawe ikulu. Hili halikubaliki na lazima wafungiwe kufanya kampeni kabla ya uchaguzi washike adabu. Narudia tena, hili halitavumiliwa.

mzee hii ni tetesi labda wamekuwekea mtego wewe ili waone reaction yako . kwa bahati mbaya nchi aiendeshwi kwa amri ama hisia zako kwa kukumbusha wahusika inabidi waende mahakamani na kuthibitisha tuhuma zao ili hayo yafanyike au umeshahau kauli zako kuwa nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na siyo kwa hisia au jazba za MWITA25.
 

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Kuna mambo ccm wameasisi lakini sina hakika kama walikaa chini na kufikiria madhara yake. 'Mfumo' wa kuandaa vijana (Green Guard) matokeo yake ni ndio haya ya DC kupigwa. Watu wamechoka na siasa za ubabaishaji na pale wanapodai mabadiliko ccm inaonekana kutumia mabavu. Kuchapwa kwa DC (kama ni kweli) ni alama tosha kuwa yeyote atakayeshiriki (directly & indirectly) kuminya haki na madai ya wananchi ya kutaka mabadiliko basi anakuwa kwenye kundi la 'kuchapwa' viboko. Ma-DC na wakuregenzi wamekuwa na tabia ya kuvuruga watu, sasa nguvu ya umma imeamua enough is enough. Green Guard was a mistake!

Mtaishia aibu na adhabu period!

Aibu kwa kushindwa, adhabu kwa kuleta vujo kwenye nchi ya amani..mambo yenu ya mererani siyo kila mahali....
 

NEW TANZANIA

Senior Member
Aug 15, 2011
101
25
mzee hii ni tetesi labda wamekuwekea mtego wewe ili waone reaction yako . kwa bahati mbaya nchi aiendeshwi kwa amri ama hisia zako kwa kukumbusha wahusika inabidi waende mahakamani na kuthibitisha tuhuma zao ili hayo yafanyike au umeshahau kauli zako kuwa nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na siyo kwa hisia au jazba za MWITA25.

imeshathibitishwa mkuu kwenye post ya pili ya kwamba ni kweli dc kalamba kibanopicha hiyo hapo chini mambo yaliyo jili
igunga.jpg
attachment.php
 

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,076
7,792
serious kweli ,chapa hao ningekuwepo ningechapa na mimi hao wanahujumu maendeleo
Siafiki namna hii ya kukabiliana na watu tusiokubaliana nao.

Mkuu, kama wasomi sisi tuwe wa kwanza kuhubiri amani na ufuatwaji wa sheria tulizojiwekea. Naamini mzee wangu Slaa na Lissu wangeweza kuchukua maamuzi sahihi kuwawakilisha wadau/wanachama wao katika kudai haki zao.

Hivi tunaelekea wapi? Imekuwaje hadi akapewa kisago? Hakukuwa na ulinzi? Naye kwanini afanye hujuma?
 

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
619
Mungu ilaani Chadema,walaani Viongozi na wanachama wote wanaoleta uvunjifu wa amani! Walaaniwe kabisa!
Mungu hawezi kuilaani CDM, atakulaani wewe na ccm yako. Hivi ujionei huruma kutokwa mapovu ya mdomo kisa kuitetea ccm inayojifia mda si mrefu? zinduka mkuu!
 

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,785
1,635
Kwanza walianza kutumwagia tindikali sasa wameanza kuwapiga viongozi wetu wa nchi na mwisho wataanza kurusha mawe ikulu. Hili halikubaliki na lazima wafungiwe kufanya kampeni kabla ya uchaguzi ili washike adabu. Narudia tena, hili halitavumiliwa.
tindikali mmemwagiana wenyewe kwa uroho wenu wa pesa. SHAME ON YOU
 

NEW TANZANIA

Senior Member
Aug 15, 2011
101
25
Mungu ilaani Chadema,walaani Viongozi na wanachama wote wanaoleta uvunjifu wa amani! Walaaniwe kabisa!

hii dua ungewaombea ccm kwanza kwa kusababisha vifo na njaa kwa maeflu hapa nchini ama la litakuwa dua la kuku kwa mwewe


Mnahubiri vita, siku watu wetu wakawajibu mtatafuta pakutokea

watu wenu ni kina nani? kama ni polisi ni lini hajafanya ugaidi? CCM haina mtu mkuu ni nyie tu mlioko kwenye payroll ya mafisadi ndio mmebaki
 

Mafuluto

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
1,862
859
Kabla sijatoa comments nasubiri kwanza kujua ukweli na facts za tukio zima. Unaweza kujikuta unamwaga pumba just kwa kutojua facts.... !! Wengine nyie mnaolaani hapa, ni wale wale mliomsifia yule rafiki ya Riziwani, mgombea ubunge wa CCM aliyempiga OCD kule shinyanga, na yule **** RPC akadai eti ni sehemu yao ya kazi..!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom