Uchaguzi IFM wavurugika,vyama vya siasa vyahusishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi IFM wavurugika,vyama vya siasa vyahusishwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sem2708, Jun 16, 2011.

 1. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Wakuu JF,uchaguzi uliokuwa umepangwa ufanyike leo tar 16 June 2011,umeahirishwa baada ya mgombea nafasi ya uenyekiti ya tume ya uchaguzi wa serikali ya wanafuzi aliyeshindwa kwenda mahakamani kuchukua pingamizi kwa madai kuwa hakutendewa haki.
  Anadai kuwa yeye ndo alipaswa kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ambayo ndo yenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa serikali ya wanafunzi IFMSO,hivyo amekataa kumtambua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya sasa ambayo ilikuwa katika hatua za mwisho za kuwezesha uchaguzi kufanyika.
  Baada ya pingamizi hii toka mahakamani,msajili wa wanafanzi kwa amri ya mkuu ya chuo akatangaza kuwa uchaguzi huo umeahirishwa.

  katika kudodosa chanzo hasa cha kuvurugika kwa uchaguzi huo,nimeambiwa kuwa mtoa pingamizi huyo inasemekana anafandiliwa na chama tawala kupitia mbunge wa eneo hili kilipo chuo cha usimamizi wa fedha na pia kuna agents wake ama wa chama chake ndo wanashikilia bango mtoa pingamizi huo asimamie uchaguzi na hivyo iwe rahisi kuweka watu kwa interest za chama...

  kwa upande mwingine imesemekana huyo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aliyemshinda mweka pingamizi ,ana muelekeo wa siasa za upinzani dhidi ya chama tawala....

  nawakilisha.
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  hivi hawa magamba walijua wakiwaweka mamluki kwenye vyuo ndo kubadilisha misimamo ya wananchi au? peoples mind are in their hearts.
   
 3. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35

  Sielewi Jf inaelekea wapi sasa.Nathamini sana ngazi za uongozi mlizo nazo huko japo kwa sasa zinaelekea kuwa na upuuzi mwingi sana.Bado mnahitajika kusoma na baadae kuja kuliongoza Taifa,hivyo your main objective ni "shule".Inashangaza siasa zimewatawala na mnakoelekea ni kudai pia Mkuu wa Chuo ama walimu wanaowafundisha ni Chama Tawala ama Upinzani.Msipo kuwa makini dhambi hii itawatafuna na vizazi vyenu.

  Uchaguzi wa IFM na vyuo vingine unatija gani kisiasa na kwa Wananchi/Watanzania?Huyo ni Kiranja Mkuu wenu na influence yake huishia kwenye maslahi yenu (posho na elimu bora).Kiongozi wa miezi 8 anakuwa na influence gani kwa hao wanasiasa mnaowataja eti wameingilia uchaguzi.Jamani....jamani....hii Nchi inaenda wapi kwa wadogo na watoto zetu mlio vyuoni?.Hivi hamsomi mmekalia politics tu,kila kukicha?

  Mjumbe huwa hauwawi,lakini hata wewe mleta hoja hii umenidisappoint kwani nawe hujui kilichokupeleka hapo Chuo.Mbali na taarifa yako,nakushauri wambie wenzio wazingatie masomo na si politics ambapo mwisho wake ni uongo tu.Mnapaswa kujiandaa kuwa wataalam wa Nchi na Wananchi si "wanasiasa",ikitokea nafasi ya kisiasa basi iwe subsidiary kwenu na si kujiwekea kama ajira.Nimechoka!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mnavitwisha vyama vya siasa mizigo isiyo wastahili. kila kitu vyama vya siasa.
   
 5. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mi nilisoma hili bango lenye lugha gongana kule kwa Michuzi nikapigwa butwaa kuona hata kwenye chuo muhimu kama IFM bado hawajui kunyoosha senstensi japo hata kwa kutumia dictionary.
  2011-06-16_1520.png
   
 6. K

  KIJIGOJUNIOR Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu JF,uchaguzi uliokuwa umepangwa ufanyike leo tar 16 June 2011,umeahirishwa baada ya mgombea nafasi ya uenyekiti ya tume ya uchaguzi wa serikali ya wanafuzi aliyeshindwa kwenda mahakamani kuchukua pingamizi kwa madai kuwa hakutendewa haki.
  Anadai kuwa yeye ndo alipaswa kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ambayo ndo yenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa serikali ya wanafunzi IFMSO,hivyo amekataa kumtambua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya sasa ambayo ilikuwa katika hatua za mwisho za kuwezesha uchaguzi kufanyika.
  Baada ya pingamizi hii toka mahakamani,msajili wa wanafanzi kwa amri ya mkuu ya chuo akatangaza kuwa uchaguzi huo umeahirishwa.

  katika kudodosa chanzo hasa cha kuvurugika kwa uchaguzi huo,nimeambiwa kuwa mtoa pingamizi huyo inasemekana anafandiliwa na chama tawala kupitia mbunge wa eneo hili kilipo chuo cha usimamizi wa fedha na pia kuna agents wake ama wa chama chake ndo wanashikilia bango mtoa pingamizi huo asimamie uchaguzi na hivyo iwe rahisi kuweka watu kwa interest za chama...

  kwa upande mwingine imesemekana huyo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aliyemshinda mweka pingamizi ,ana muelekeo wa siasa za upinzani dhidi ya chama tawala....

  nawakilisha.

  Wana JF,

  Nadhani pia mleta mada amekurupuka kuripoti kile ambacho hajakifanyia utafiti. Kuna msemo kuwa "No Research no Right to Speak". Na nadhani hii ndiyo inayojionesha kati ya wanafunzi wa IFM na wakutoka vyuo vingine hapa nchini. Maelezo aliyoyatoa hapo juu si ya kweli. Nimepata bahati ya kuonana na aliyefungua kesi na kuongea naye kwa kirefu zaidi. Suala ni kwamba Katiba ya Uongozi wa Serikali ya wanafunzi imekiukwa kwa kiasi kikubwa. Tarehe 3 Juni Mwaka huu, bunge la wanafunzi (ISRC) lilichagua Kamati ya Uchaguzi (Electoral Committee) kwa ajili ya kusimamia shughuli za uchaguzi chuoni hapo, na Mlalamikaji alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa tume hiyo. Kamati hiyo ilikuwa ya watu nane. Ikumbukwe tu kuwa mara baada ya uteuzi wa Kamati ya Uchaguzi, basi Bunge huvunjwa kupisha shughuli za uchaguzi. Kwa kuwa Katiba inasema Kamati yapaswa kuwa na wajumbe 10, basi, Spika wa Serikali ya Wanafunzi IFM, aliwateua wajumbe wengine wawili.Lakini chini ya Katiba, Spika huyo hakuwa na Mamlaka ya Kuteua wajumbe hao. Uteuzi wa wajumbe unapaswa kufanywa na Wajumbe 8 waliokuwa wameteuliwa. Baada ya kuona kuwa Katiba haikufuatwa, basi Mlalamikaji alipeleka barua ya "anomalies" hizo kwa Rector tarehe 6 Juni. Baada ya kuona hivyo, tarehe 7 juni Rector akashauri Bunge (Lililokuwa limevunjwa tarehe 3 juni) liitishwe ili uchaguzi wa wajumbe wa tume ufanyike. Bunge likaitisha kikao within a very short time na kuchagua wajumbe wengine wa tume. Argument hapa ni kuwa Bunge halikuwa na malaka ya kuitisha kikao hicho kwa kuwa Kisheria halikuwepo kwa kuwa lilivunjwa tangu tarehe 3 juni 2011. Mlalamikaji pia baada ya kuona mapungufu na kutokufuatwa kwa katiba, tarehe 9 juni 2011 aliandika barua nyingine kwa Rector, na mpaka leo hakuna hata barua moja juu ya aliyoyaomba yafanyiwe kazi ambayo imejibiwa. Kwa hiyo mambo yote ambayo yamekuwa yakifanywa tangu tarehe 8 juni na "the purpoted electoral committee" kisheria ni nulity, na hivyo ilikuwa ni muhimu kupata Amri ya Mahakama kuweza kuzuia "illegalities" ambazo zilikuwa zinafanyika leo, yaani uchaguzi.

  Ni hayo tu kwa sasa. Chamsingi Katiba ya IFMSO ifuatwe
   
Loading...