Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu ndiyo unatoa taswira ya CCM kuwa wamoja au hakuna umoja

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,194
Habari zisizo na chembe ya kutaka umma usielewe kinachoendelea ipo wazi kutokana na safari ya uchaguzi wa nafasi ya urais kupitia kampeni tunazoziona wakati huu.

Mwaka 2015 ilichezwa mechi (uchaguzi) ambayo ilikuwa na marefarii watatu moto wakiwa wamekaa katikati wakiunganisha krosi zinazokuja kutoka kwa mawakala kwenda nec, wana ccm wangi wanafanya kampeni kwa kulazimisha nafsi zao ila siyo kutoka moyoni, maana wanajua usipojitoa kwa chama b'na mkubwa anakushugulikia ipasavyo.

Wadau wa siasa wanakumbuka week iliyopita kulikaa kikao cha kutathimini na kuwataka viongozi wastaafu wajiunge ili kuokoa jahazi linaloelekea kuingiza maji na kuzama.

Kuna mzee Kinana, Makamba Jr na Nape kijana wa bao la mkono hawa jamaa hatuji kwa sasa wako wapi ila kutokana na njia waliyoipitia awamu hii sidhani kama wanaweza kutandika red carpet na kuruhusu gip akanyage hilo zulia.

Kinachoendelea kwa sasa ni kukaa kimya wakijionyesha kutenda kazi yao waliotumwa na mkulu huku kila mmoja akielewa huyu mzee hakuna kitu hapo, huyu anatuzuga na akirudi tabia yake ni ile ile, kama anawatukana wananchi katika kipindi hiki cha kampeni itakuwaje kwa sisi ambao tulishatendwa?.

Hakika maji yako shingoni, katika uchaguzi uliowahi kufanyika hapa nchini basi huu ndiyo unatoa taswira ya ccm kuwa moja au hakuna ummoja.
 
Sura halisi za wanaccm walio wengi zitaonekana hadharani mwaka 2025! Kwa hii miaka 10 watajitahidi kuishi maisha ya kinafiki, ya kujificha na ya kujikombakomba kwa mwenyekiti mbabe wa chama.
 
CCM wasipogawanyika, kuna maslahi, na wakigawanyika pia kuna maslahi makubwa zaidi

Yaani Chama hicho, kila kitakachotokea kina faida kwao, ndo ujuwe wale Kwa siasa za TANZANIA na Africa, CCM ni Baba lao
 
CCM hata wakigawanyika hawatakubali chadema waingie madarakani sababu kuna 2025
 
Habari zisizo na chembe ya kutaka umma usielewe kinachoendelea ipo wazi kutokana na safari ya uchaguzi wa nafasi ya urais kupitia kampeni tunazoziona wakati huu.

Mwaka 2015 ilichezwa mechi (uchaguzi) ambayo ilikuwa na marefarii watatu moto wakiwa wamekaa katikati wakiunganisha krosi zinazokuja kutoka kwa mawakala kwenda nec, wana ccm wangi wanafanya kampeni kwa kulazimisha nafsi zao ila siyo kutoka moyoni, maana wanajua usipojitoa kwa chama b'na mkubwa anakushugulikia ipasavyo.

Wadau wa siasa wanakumbuka week iliyopita kulikaa kikao cha kutathimini na kuwataka viongozi wastaafu wajiunge ili kuokoa jahazi linaloelekea kuingiza maji na kuzama.

Kuna mzee Kinana, Makamba Jr na Nape kijana wa bao la mkono hawa jamaa hatuji kwa sasa wako wapi ila kutokana na njia waliyoipitia awamu hii sidhani kama wanaweza kutandika red carpet na kuruhusu gip akanyage hilo zulia.

Kinachoendelea kwa sasa ni kukaa kimya wakijionyesha kutenda kazi yao waliotumwa na mkulu huku kila mmoja akielewa huyu mzee hakuna kitu hapo, huyu anatuzuga na akirudi tabia yake ni ile ile, kama anawatukana wananchi katika kipindi hiki cha kampeni itakuwaje kwa sisi ambao tulishatendwa?.

Hakika maji yako shingoni, katika uchaguzi uliowahi kufanyika hapa nchini basi huu ndiyo unatoa taswira ya ccm kuwa moja au hakuna ummoja.

Umoja upo kwenye wizi tu. Wakishindwa uchaguzi chama kutasambaratika kama mkate uliochovywa kwenye chai.
 
Kuna CCM tatu hapa, CCM wafia chama; CCM migrants ( wale toka vyama vya upinzani) na CCM Maslahi.

CCM wafia chama : Hawa ni wana CCM damu, hawa wapo radhi kulala njaa lakini chama chao wakilinde - wengi wao wamesahaulika kwenye teuzi ila bado hawajakata tamaa.

CCM Migrants: Hawa ni wahamiaji toka vyama vya upinzani, wengi wao walikuwa ni Madiwani, Wabunge na wenyeviti wa vijiji - Hawa wanakula bata ndani ya CCM - wengi wao wamelamba nafasi za uteuzi na wapo kimya wanacheki movi linaendaje ndani ya chama chao.

CCM maslahi: Hawa wao wanasubiri tu uchaguzi uishe ili wawinde fursa za kibiashara... kundi hili linatengenezwa na wafanyabiashara wakubwa wakubwa na baadhi ya wasomi wabobevu..... kwa namna kampeni zinavyokwenda, baadhi ya wanachama wa kundi hili wameanza kupata wasiwasi juu ya hatma yao baada ya oct 28th.
 
Nimewapenda hawa migrants 😁!

Back
Top Bottom