Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu hatutaki kusikia sera, tunahitaji mwendo mdundo wa kuing'oa CCM

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,819
Wacha CCM wazungumzie sera mpaka washikwe na presha, huku upinzani ni kampeni za kuisaga CCM na kuonyesha uovu wake wote na hawastahili kuongezwa hata dakika moja.

Waende mitaani na sera zao za ajabu ajabu wanampigia mbuzi gitaa, wananchi walio wengi tumechoka na sera na mikakati hio hio kila siku, hawana jipya. Wanajua Lissu amewashika pabaya sana na hawatoki wala kuona nje, huku hakuna cha sera yaani mtazisikia sera baada ya kuwaondoa kwenye viti na meza, yaani CCM tutawaajiri watengeneze barabara na madaraja ndio jambo wanaloliweza, hawana habari na mwananchi wa kawaida wanajisifu kwa kuwa wao ndio wanamiliki magari mazuri ya kifahari, sasa watakaa pembeni na kuajiri kusuka barabara.

Lissu endelea kuwaanika na katika hii lala salama wapige virungu wapigike kwelikweli, sera utatupa ukiwa Raisi hapo tarehe 29/10/2020.
 
Sasa kuanzia sasa tunaanza kuchimba kaburi la CCM,na tutaandika na kibao tusije tukalipoteza kaburi la maiti mtarajiwa.
 
Kumbe wakati watanzania wanakero ya umasikini na miundombinu mibovu, kumbe nyie upinzani kero yenu ni ccm? Sisi tulidhani mnasera madhubuti kumbe ni mbwembwe ya kutuhadaa huku kero yenu ikiwa ccm?
 
JPM wakati anapambana na Lowassa alipiga push-ups nyingi mara kadhaa, ulifahamu maana yake? Dhihaka kwa Lowassa kuhusu afya yake. Rhetorical language.

Wakati huu anapambana na amepigishwa magoti mara mbili akiomba kura, unajua maana yake??

Mataga Tafuta thamani ya X......
 
YALIYOJIRI KTK SIKU 30 ZA MWANZO ZA KAMPENI YA SIKU 60 ZA UCHAGUZI 2020

Haya tena, hatimaye uchaguzi mkuu 2020 umefikia hatua ya Kati na CHADEMA imefanikiwa kujenga mahusiano na waTanzania kupitia ushawishi wa Maendeleo ya Watu siyo Maendeleo ya Vitu, kuondoa umasikini na kusisitiza kutilia mkazo demokrasia bila kusahau Ilani iliyo maarufu ya Uhuru na Haki na Maendeleo ya Watu.

Tanzania chini ya serikali ya awamu ya 5 inatilia mkazo mkubwa Maendeleo ya Vitu kama miundombinu ya madaraja, flyovers, viwanja vya ndege na reli ya SGR Dar-Mwanza. Pia serikali ya awamu ya 5 haitaki 'makelele' ya mikutano ya kisiasa ya vyama vingi maana awamu ya 5 ni 'hapa kazi tu', demokrasia baadaye wakimaliza ujenzi wa miundombinu.

Kwa ufupi misheni na visheni ya serikali ya CHADEMA 2020 na visheni ya serikali ya CCM awamu ya 5 yaTanzania zinapishana zikielekea pande mbili tofauti, moja inaelekea pande za mashariki nyingine magharibi.

Ni Nani atamshawishi mwenzie abadili muelekeo. Wananchi watanzania wanataka maendeleo ya watu, serikali ya CCM inasema hapa kazi tu miundombinu kwanza.

Hitimisho wananchi watanzania kelele zao kuhusu ugumu wa maisha ni kama zinaiambia serikali ya awamu ya 5 wanataka maendeleo ya watu na demokrasia ili kusikilizwa vilio vyao na hilo tumeliona katika mahudhurio ya maelfu ya wananchi ktk mikutano mikubwa ya Hadhara ya CHADEMA kipindi hiki cha Kampeni ndani ya siku 30 zilizopita.
 
Back
Top Bottom