Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu CCM msijichangane kupitisha wagombea wasiokubalika Majimboni na kwenye Kata

Wajumbe

Senior Member
Jul 26, 2020
136
379
Naomba nitoe ushauri kwa chama tawala. Kwanza nirudie maneno ya Mzee Kinana " Hakuna uchaguzi rahisi". Pili naomba nishauri. Katika mchakato wa kura za maoni wagombea wengi walijitokeza.

Kati ya hao wapo vijana wasomi wenye maono. Bahati mbaya vijana hawa hawakuwa na pesa za kuwapa wajumbe na hivyo wamepata kura chache. Waliopata kura nyingi ni wagombea waliowekeza kwenye kugawa rushwa lakini sio viongozi na hawana maono yeyote ya kuyatumikia majimbo au kata zao. Wagombea matajiri wanahitaji mambo matatu tu:

1. Heshima kwamba wamewahi kuwa wabunge
2. Wanafikiria kupata nafasi za uteuzi wa uwaziri
3. Kutumia nafasi zao kuficha ufisadi wanaufanya katika biashara na maeneo mengine ya utakatishaji wa fedha haramu.

Lakini kwa upande wa hawa vijana wasomi nao wamegawanyika katika makundi matatu kwa malengo yao:

1. Wagombea wachache wenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi. Hawa utawagundua kwa kuwa wamekuwa midomoni mwa wanaccm na wananchi wakitajwa tajwa kwa kipindi cha miezi sita, mwaka mmoja, miwili au zaidi. Hawa wapo wachache. Na wengi walikwenda kuandika nia zao katika wilaya au kata

2. Wagombea wapeleka CV. Hawa wamejitokeza kwa lengo la kuonekana na kufikiriwa katika teuzi mbalimbali mfano uDAS, DC, wakurugenzi, nk. Hawa wapo wengi...wanaweza kufikia asilimia 80 ya vijana wengi. Hawa ni chenga. Hawajui changamoto hata moja ya jimbo au kata kwa kuwa hawajaziishi katika kupata uzoefu. Wengine hawajui hata jografia ya kata zao ukiachilia mbali majimbo. Kwa kweli hawa inabidi chama kichukue CV zao tu

3. Wagombea wengine ni wagombea mamluki.
Kuna baadhi ya maeneo ambayo baada ya kuonekana baadhi ya wagombea vijana na wasomi wamekubalika zaidi, basi wagombea matajiri waliwatafuta vijana wengine wasomi kutoka Dar na mikoa mingine ambao wanatoka katika jimbo husika, na kuwapandikiza katika kata au ukanda ambao yule tajiri anapata upinzani. Wagombea wa namna hii .. aah ndio basi tena. Hawa waligharimiwa usafiri wa kwenda jimboni na kufanya kampeni kwenye kata yake, walilipiwa gharama za fomu, michango, malazi, chakula, mavazi, nk. Katika maeneo mengi, wagombea hawa walikuwa wapya na hawafahamiki hata na wajumbe wa kijijini/mtaani kwao. Wengine hata majina ya kata au vijiji vya kata zao walishindwa kuviorodhesha. Hawa ni wagombea " basi tena". Wengi waliambulia kuanzia kura 0 hadi 5 na wachache walifika 10-20. Ushauri kwa chama cha mapinduzi. Hapa hakuna kituu

Sasa nirudi kwenye mada:

Tunafahamu kwa chaguzi zilizopita, wapinzani walifanikiwa kuwasimamisha wagombea wenye haiba ya uongozi, wasomi na vijana wenye maono. Naomba nishauri uchaguzi huu una mambo mengi, mengine ya wajumbe; chama kifanye utafiti wa kina na kupata kijana mmoja msomi na mwenye maono aweze kupeperusha bendera ya chama na mwenye uwezo wa kupambana na vijana wasomi watakaosimamishwa na upinzani

Huu ni ushauri wangu tu. Naomba niendelee na utafiti. Ya watoa rushwa tunawaachia takukuru.

Wajumbe oyee
 
Back
Top Bottom