Uchaguzi Huru ni kielelezo cha kukua kwa Demokrasia

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Ndugu wanajamvi habari za majukumu!!!

Demokrasia ni neno linalotambulisha kuwa katika jamii fulani ya watu kuna utawala uliowekwa na watu wenyewe kwa ajili yao na manufaa yao wenyewe. Kwa maana nyingine ni mfumo wa utawala unaowezesha Wananchi kuchagua viongozi kutokana na matakwa yao wenyewe na sio kutokana na matakwa mtu fulani au kikundi fulani cha watu wenye maslahi yao binafsi.

Kama tunavyojua Tanzania imepita katika chaguzi mbalimbali za kuwapata viongozi ambao ndio wawakilishi wa wananchi. Katika hili tunaona kuwa Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu uliohusisha Vyama Vingi vya Siasa mwaka 1995, 2000, 2005, 2010 na mwaka 2015. Kwa kuzingatia jambo hilo Tanzania tumekuwa tukifanya Uchaguzi Mkuu kila baada ya miaka 5. Uchaguzi huo umekuwa ukiruhusu kuwepo kwa kushindana kwa wagombea kutoka katika Vyama mbalimbali vya Siasa ili kupata uwakilishi Bungeni na Serikalini.

Kikubwa tunachojifunza hapa ni kwamba mfumo huu wa Utawala wa Kidemokrasia unaheshimu mawazo na mitizamo tofauti, pamoja na kuvumiliana katika nyanja za Kisiasa.

TUZITAZAME KANUNI MUHIMU ZA DEMOKRASIA.
Demokrasia ya kweli ina kanuni ambazo zinabidi zifuatwe ili jamii itambulike kuwa ina utawala wa Kidemokrasia, hizi ni pamoja na;

1. Ushirikishwaji wa wananchi; Hii inamaanisha kuwa wananchi wanashirikishwa katika maswala yote yanayohusu jamii na nchi yao, Kupewa fursa mbalimbali katika Utawala wa nchi yao ambayo hupatikana kupitia Uchaguzi ulio sawa na huru kwa kuwapa wananchi haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi na wanayo haki ya kuhoji utendaji wa Viongozi waliowaweka madarakani.

2. Kuheshimu Haki za Binadamu; Utawala wa Kidemokrasia huheshimu Haki za msingi za Binadamu, Haki hizi ni kama vile Kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi, Kupatiwa Ulinzi na Usalama, Kufanya Mikutano na Kuchagua Chama au kundi la Siasa apendalo mtu bila kubughudhiwa ama kutishwa n.k.

3. Mgawanyo wa Madaraka; Katika Utawala wa Kidemokrasia Uongozi wa nchi hutawaliwa na mihimili 3 ambayo ni Utawala, Bunge na Mahakama, Mihimili hii huwa huru na haiingiliani katika ufanyaji wa Kazi.

4. Staha na Uvumilivu wa Kisiasa;Utawala wa Kidemokrasia unawezesha watu wenye Itikadi, Mawazo na maono ya kisiasa kupata nafasi ya kuyaeleza wapendavyo na watu wengine wanapaswa kuyaheshimu.Ni kinyume na na Utawala wa Kidemokrasia kutumia nguvu, vurugu, vitisho na fujo kulazimisha watu kukubaliana na Sera au Itikadi za chama au kikundi fulani. Uamuzi wa kukubaliana au kutokukubaliana hufanywa kupitia SANDUKU LA KURA.

5. Uwazi na Uwajibikaji. Utawala wa Kidemokrasia unamtaka kiongozi awajibike kwa wananchi waliomchagua na uwepo uwazi katika matumizi ya mali za umma ili zitumike kwa manufaa ya wote, Anayetumia vibaya mali hizo lazima apelekwe Mahakamani na akibainika na Makosa anahukumiwa kwa makosa aliyoyatenda.

6. Chaguzi Huru na za Haki;Chaguzi katika Utawala wa Kidemokrasia lazima zifanike kwa Uhuru, uwazi na katika muda uliokubalika na muda huo ukifika wa kufanya chaguzi lazima uheshimiwe. Chaguzi hizi ni lazima zishirikishe watu wote wenye sifa za kupiga kura. Mpiga kura apige kura kwa Uhuru bila kuingiliwa na kura yake iwe ni Siri yake mwenyewe. Ikumbukwe kuwa katika kuomba ridhaa ya wananchi vyama vya Siasa vinapaswa kupewa Uhuru ulio sawa wa kufanya mikutano na kuelezea Sera na Mipango yao vilevile kukosoa Sera za vyama vingine BILA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI.

7. Huru wa Vyombo vya Habari; Vyombo vya habari vinatakiwa kutoa habari kwa uwazi juu ya mambo yote muhimu kwa maslahi ya Taifa.Vyombo vya Habari vinatakiwa kutoa umuhimu sawa kwa wadau wote wa siasa ili kuwapa watu fursa ya kupata habari na hatimaye wafanye uamuzi sahihi.

8.Utawala wa Sheria, Hii ni kanuni yetu ya mwisho tutakayoiangalia ya Demokrasia kwamba katika Utawala wa Demokrasia Hakuna mtu yeyote ambaye yuko juu ya Sheria na hakuna ubaguzi katika kutekeleza Sheria. Yeyote atakayevunja Sheria ni lazima ahukumiwe kwa makosa aliyoyatenda bila kujali cheo, wadhifa au umashuhuri wa kwa umma.

Nawatakia siku njema, Naomba Kuwasilisha.

 
Uwezo wa kuendesha chaguzi zetu mfano ule wa 2015 kwa amani na Utulivu ni ishara tosha ya ukomavu wa Demokrasia nchini, na hili halina ubishi, nchi kibao zinajifunza hili tatizo tu Nabii siku zote hakubaliki nyumbani kwao!
 
Back
Top Bottom