Uchaguzi Ghana: Akufo-Addo ametangazwa mshindi

ng'ombo

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
418
619
ghana.jpg

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Ghana (New Patriotic Party) Bwana Nana Akufo-Ado pichani juu ameshinda uchauguzi mkuu wa urais uliokuwa na upinzani mkali uliofanyika jumatano. Rais wa Ghana John Mahama amekubali kushindwa.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa upinzani kuongoza nchi toka mfumo wa vyama vingi uanze nchini Ghana 1992. Msemji wa chama cha upinzani amesema Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amemtangaza Bwana Akufo-Addo ameshinda kwa 53.85% wakati Bwana Mahama amepata 44.40%
 
Wenzetu Ghana walisha jifunza, walipinduana weee! Baadaye wakaona haina maana, wamerehea kwenye demokrasia ya kweli kama hivi
 
Hawa viongoz wa africa wanaanza kuelewa maana ya democracy kidogo, Ila tutafika tu juz rais Jameeh kakubal leo NANA Kashinda na nadhan bwana John mahama kakubali
 
View attachment 444725

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Ghana (New Patriotic Party) Bwana Nana Akufo-Ado pichani juu ameshinda uchauguzi mkuu wa urais uliokuwa na upinzani mkali uliofanyika jumatano. Rais wa Ghana John Mahama amekubali kushindwa.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa upinzani kuongoza nchi toka mfumo wa vyama vingi uanze nchini Ghana 1992. Msemji wa chama cha upinzani amesema Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amemtangaza Bwana Akufo-Addo ameshinda kwa 53.85% wakati Bwana Mahama amepata 44.40%
Masahihisho;sio kweli kuwa hii ni mara ya kwanza upinzani kushinda Ghana.

Mara baada ya Jerry Rawlings kuachia madaraka,mpinzani John Kuffour alishinda urais na kutawala kwa awamu mbili akimshinda mgombea wa chama tawala, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jerry Rawlings, Prof John Atta Mills.

Baada ya John Kufour kumalizia vipindi vyake viwili madaraka,mpinzani Prof John Atta Mills alichukuwa madaraka akimshinda aliyekuwa mgombea wa chama tawala na Waziri wa Mambo ya Nje wa John Kufour ndugu Nana Akufo Ado.

Prof John Atta Mills akafariki kabla ya kumaliza kipindi chake, makamu wake John Mahama akachukua madaraka kumalizia term hiyo.

Kisha uchaguzi uliofuata John Mahama alimshinda mgombea wa upinzani sasa, Nana Akufo Ado.

Baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza sasa,.ndio uchaguzi huu sasa Rais John Mahama ameangushwa na mpinzani wake wa chama cha Rais Mstaafu John Kufour ndugu Nana Akufo Ado.

Hivyo toka vyama vingi vianze vyama vya NDC cha Jerry Rawlings na chama cha NPP cha John Kufour vimetoa marais wawili wawili kila Kimoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom