Uchaguzi EALA usogezwe mbele, uteuzi umekiuka Mkataba wa Afrika Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi EALA usogezwe mbele, uteuzi umekiuka Mkataba wa Afrika Mashariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Apr 15, 2012.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mchakato wa uchaguzi wa Afrika Mashariki unaoendelea hivi sasa sio huru na wa haki hivyo Spika, Katibu wa Bunge na serikali wanapaswa kuchukua hatua za haraka kurekebisha kasoro zilizojitokeza ili kuhakikisha uchaguzi huo unawezesha wabunge kupatikana kidemokrasia na kwa kuzingatia maslahi ya umma. Aidha, natoa mwito kwa wananchi na wadau wote kufuatilia kwa karibu uchaguzi huu muhimu kwa taifa kwa kuwa unahusu uwakilishi wa nchi katika chombo muhimu cha kuwakilisha wananchi, kuvisimamia vyombo vya kiutendaji vya Jumuia ya Afrika Mashariki na kutunga sheria za kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki na mipango muhimu ya maendeleo katika masuala ya ushirikiano.

  Baadhi ya hatua za haraka zinazopaswa kuchukuliwa ni: Msimamizi wa kuzingatia kuwa amefanya uteuzi bila kuzingatia ibara ya 50 ya Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki; kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi ili kutoa fursa kwa wagombea walioteuliwa kufanya kampeni rasmi na pia kutoa nafasi kwa mapingamizi kuwekwa kwa wagombea wasiokuwa na sifa kwa mujibu wa Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki na kanuni husika; kueleza wazi kwa vyama, wabunge na wananchi ni mfumo uliotumika kugawanya idadi ya nafasi tisa zinazogombewa kwa kuzingatia matakwa ya ibara ya 50 ya Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki; kufanya marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bunge zinazosimamia uchaguzi wa Afrika Mashariki.
  Izingatiwe kwamba kwa mujibu wa Katibu wa Bunge ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi husika uteuzi wa wagombea ulipaswa kufanyika tarehe 10 Aprili 2012; hata hivyo uteuuzi wa wagombea umetangazwa tarehe 14 Aprili 2012.

  Aidha, vyombo mbalimbali vya habari vimenukuu kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeteua wagombea 24, kwa msingi wa majina matatu ya wagombea kwa kila kundi hali ambayo inaonyesha kwamba kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi, chama hicho kimoja kinatarajia kuwa na nafasi nane miongoni mwa nafasi tisa za wabunge wa Afrika Mashariki.Tafsiri ya suala hili ni kwamba inatarajiwa kuwa vyama vya upinzani vitapata nafasi moja tu hali ambayo ni kinyume kabisa na ridhaa ya wananchi ambayo waliionyesha kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na pia ni kinyume na Ibara ya 50 ya Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambao unataka uwakilishi mpana.

  Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita ambayo yanapaswa kuwa msingi mmojawapo muhimu katika maamuzi kuhusu mgawanyo wa viti CCM (asilimia 74 ya uwakilishi bungeni hata kama ikichukua zote na kuacha kutoa kwa vyama vingine inastahili nafasi zisizozidi 7), CHADEMA (Asilimia 13.7 sawa na nafasi 1) na CUF (Asilimia 10.3 sawa na nafasi 1).

  Izingatiwe kwamba ibara ya 50 (1) ya Mkataba wa Afrika Mashariki inatamka bayana kwamba "The National Assembly of each member Partner State shall elect, not from among its members, nine members of the assembly, who shall represent as much as it is feasible, the various political parties represented in the National Assembly, shades of opinion, gender and other special interest groups in the partner state, in accordance with such procedure as the National Assembly of each Partner State may determine".

  Hivyo, Kanuni ya 12 na Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2007 inakinzana na kugongana na Ibara ya 50 ya Mkataba wa Afrika ya Mashariki hali ambayo inadhihirisha umuhimu wa Kanuni husika za Bunge kufanyiwa marekebisho au mabadiliko kwa mapendekezo yangu au ya Kamati ya Kanuni kama nilivyoomba kwenye barua yangu kwa Katibu wa Bunge ya tarehe 8 Februari 2012.Kutokana na upungufu huo, ili kuhakikisha uteuzi na uchaguzi unafanyika kwa mchakato huru na wa haki niliwasilisha mapendekezo ya ziada ya marekebisho yenye kulenga kanuni husika zibadilishwe kabla ya uchaguzi kufanyika tarehe 17 Aprili 2012.

  Kwa mujibu wa Kanuni ya 115 Nyongeza ya Nane 3 (3) (b) na Kanuni ya 152 (1); nimependekeza marekebisho yafanyike katika Kanuni ya 12 kwa: kuondoa maneno "uwiano wa idadi ya wabunge wa vyama mbalimbali vinavyowakilishwa bungeni' na kuingiza maneno "vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni"; kuongeza maneo "maoni mbalimbali (shades of opinion) na makundi maalum ya kijamii" mara baada ya neno ‘jinsia' na kabla ya maneno ‘uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano"

  Pia, kwa mujibu wa Kanuni ya 115 Nyongeza ya Nane 3 (3) (d) nimependekeza kufanyike mabadiliko katika Nyongeza ya Tatu ya Kanuni kwa: kufuta kifungu cha 5 (5); kufuta kifungu cha 11 (3) na kubadili mpangilio wa namba kuanzia kifungu kidogo cha (4); Kufanya marekebisho kwenye vifungu vya 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12 na 13 kama nilivyopendekeza kwa barua yangu ya tarehe 4 Aprili 2012.Aidha, nimewaandikia rasmi barua Spika na Katibu wa Bunge kuwaomba wachukue hatua za haraka kurekebisha mchakato wa uchaguzi husika ikiwemo kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Kanuni kwa ajili ya kuchukua hatua zinazostahili ili kuhakikisha uteuzi na uchaguzi unakuwa huru na haki kuepusha kasoro zilizojitokeza mwaka 2006 wakati wa Bunge la tisa kujirudia mwaka 2012 katika Bunge la kumi.

  John Mnyika (Mb)
  Bungeni-Dodoma
  14/04/2012
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Rekebisha font zako mkuu then weka paragraphs ili tukusome vizuri hoja zako. Nimeshindwa hata kuendelea kusoma maana macho yanauma sasa. Mods msaidieni kama jamaa hana utaalamu sana na mambo haya
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mnyika umesome, Hongera sana kwa umeakini wako
   
 4. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Good observation Mnyika ingawa naona kama umechelewa kuwasilisha maombi hayo na serikali ya CCM niniavyoifahamu kwa ubabe wanaweza kulazimisha uchaguzi ikafanyika bila kuzingatia kanuni husika. Inabidi wapinzani msimame kitede kulitetea hilo kuhakikisha kanuni hazikiukwi. Solidarity forever...
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Thank You kamanda sasa unasomeka vema baada ya marekebisho. Una hoja ya msingi lakini ni kawaida ya watawala kukaidi hoja zitokazo upinzani, no matter what! Sitashangaa wakipuuzia hoja zako hizi licha ya kwamba ni muhimu iwehivyo
   
 6. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu huu ni ukiukwaji mkubwa wa article 50 of EAC treaty,je iwapo bunge na serikali ya c.c.m hawatakubali kurekebisha kasoro hizo na kulazimisha uchaguzi uendelee jambo ambalo ni very likely kwa jinsi tunavyowajua C.c.m,je kutakua na uwezekano wa suala ili kupelekwa mahakamani na kupatiwa ufumbuzi huko?
   
 7. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwa vile EAC ina mahakama zake hilo linawezekana.

   
 8. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Viongozi wetu hawasomi mikataba au wanavunga hawajaona vifungu hivi? Wanapnda vyeo vyote vitoke upande mmoja asif wao ndio wenye haki ya kutawala! Tanzania ni ya watanzania wote jamani hivyo basi tuthamini haki za watanzania wote bila kujali ideologies zao.
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hoja ya kuchelewa kuwasilisha ombi la mabadiliko ya kanuni hapa haina nguvu. Mnyika anasema aliandika barua Februari 8, 2012. Kulikuwa na miezi miwili ya kujadili hilo swala na kubadilisha.

  Kama serikali na Bunge watagoma na kuamua kuendelea na mchakato, then CHADEMA waende Mahakama ya Afrika Mashariki kusaka haki yao. Mkataba wa Afrika Mashariki uko wazi na unataka uwakilishi kwa kuangalia vigezo vyote muhimu lakini muhimu zaidi uwakilishi kwenye Bunge la nchi husika.

  Jana kwenye thread moja nilisema kwamba bila kubadilisha kanuni, CHADEMA haitakuja kupeleka mwakilishi kwenye Bunge la Afrika Mashariki. CCM watakuwa wanatumia wingi kuikomoa CHADEMA kwa kuwa CCM wana uwezo wa ku-influence uchaguzi wakienda kupiga kura huku wamekubaliana kwamba wanamuunga nani mkono.
   
 10. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kila la kheri kwa wapigania demokrasia ya kweli hapa nchini,MUNGU atawalipa sawa sawa na kujitolea kwenu.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  hoja yako ya msingi....
  Ila wale wazee wa wanaokubali waseme ndio: ndiyooooooooooooooooooooooo
  sijui kama itapita hii.....
   
 12. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  If they don't change the rules of the game, CHADEMA should not participate in these elections. Instead, it should quickly file a case with the EACJ. If it is not too late we could put an injunction so that the elections are suspended until these pending issues are resolved. Otherwise, tunaingia kwenye uchaguzi ambao CCM wanatuamulia nani awe mwakilishi wa opposition katika EALA, na tunajua hawawezi kumchagua mgombea kupitia CHADEMA.
   
 13. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Mh.Mnyika you may be right on the misconduct on how MPs are represented in the EAC seats contest.....lakini nikuulize tu nyie wabunge wa CDM huwa mnakuwa wapi mpaka mnakuja kutoa malalamiko haya mwishoni????maana mchakato huu wa uteuzi wa majina ya wagombea umeanza mda mrefu na mlikuwa mnaona hili....sasa najiuliza mbona hamkulalamika tangu mapema??...inauma sana maana wenzenu kina UG wamepeleka muda mbele ili kuweka mambo sawa....kuna tatizo kubwa sana kwenye kupata true representation ya mawazo ya watanzania kwenye EAC parliament na nilitegemea hili nyie kama wabunge makini muwe mmeliona tangu mwanzo.........lakini mnashtuka mwishoni....kwanza sijui nyie kama wapinzani mnajipangaje kupigia kura hao wabunge wa CCm..maana kwa taarifa ni kwamba kuna rushwa kubwa inatembea currently hapo dodoma...watu wanahonga wabunge ili wachaguliwe kutuwakilisha watanzania...hii haingii akilini kabisa.....na nyie wabunge hatuoni mkipigia kelele hili jambo......tunasikia rushwa inatembea lakini hatusikii mkipiga kelele kupinga wakati na nyie mtatakiwa kuwapigia hao watoa rushwa watuwakilishe.....mtu anaenunua kura kwa wabunge ili achaguliwe anawezaje kutuwakilisha???????...Please...please.....its high time now for you MPs from TZ to adopt the just proposed protocol which will allow EAC MPs to be elected directly by people from their respective countries...hii itaondoa haya matatizo ya vyama tawala kuwa na wabunge wengi ambao wengi wao wanateuliwa/kuchaguliwa kwa sababu za kimaslahi kwa vyama/watu wanaowateua/wachagua.........please...kwa nafasi yako bungeni jaribu ku introduce hii proposal kwa wabunge woote ili muifanyie discussion.......EAC: EALA MPS will soon be directly elected by the voters in their respective counties before being sent to the EAC « Jaluo
   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180

  nakubaliana na wewe. CDM ikaweke ijuction katika mahakama ya Afrika Mashariki ili uchaguzi huo usimamishwe kwanza
   
 15. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Siyo Mara ya kwanza kwa hawa jamaa kwa makusudi kukiuka sheria ambazo wamezitunga na kuzikubali wenyewe na si kwa sababu hawafahamu bali kwa sababu ya kuihofia CDM na kuikandamiza CDM..

  Sasa nawashauri CDM ni mara chache sana haki itapatikana kwa hawa wezi waliolelewa katika uwizi kwa miaka 50, Dawa yao ni kutumia utaratibu alioutoa Dr Mkumbo na ikishindikana ni kutumia Peoples power.

  Na naiomba CDM katika hiyo Peoples Power Target yenu iwe ni JK na si hawa kina Lusinde ambao masikio yao ni ya Kufa wala hayasikii tena dawa..
   
 16. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Nivema CDM wakaweka msimamo wa kuweka pingamizi kwanza tupate muafaka kwani hawa wahuni çcm ukiwaachia wanafanya kama wanavyotaka kama hakuna waelewa wa sheria.

  Na ikiwa Makinda aliandkiwa barua toka feb mbona hakujibu hii ni dharau kubwa.
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kitila

  Naungana na CDM kama bunge lisiporekebisha kanuni basi wajitoe, after all you won't lose anything kwa vile hata kama mkishiriki itakuwa formality tu kwa vile inajulikana kwa hizi rules mgombea wa CDM will never be voted in.

  Mkumbo naomba CDM iwe inafanya vitu kwa vitendo, kama katibu wa bunge na Spika wataendelea kupuuza, by tomorrow mnatakiwa muwe mmesha-file case Arusha East African Court of Justice kuweka injunction, mjue demokrasi ni gharama. Kwa sababu in any case(ratio ya wabunge au kura za urais) wapinzani wanatakiwa kuwakilishwa na at least wabunge wawili. Haiwezekani CCM ku monopolise kila kitu, No one owns this country.
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mwaga mboga na wao wamwage ugali!
  If they stand for election they know who'll win even before the vote!
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa mara nyingine tena Spika wa CCM na wabunge wake wanapindisha kanuni kwa manufaa ya chama chao CCM. Mara ya kwanza alibadili kanuni za bunge kwa kutoa tafsiri mpya ya chama kikuu cha upinzania nia na madhumuni ikiwa ni kujaza mamluki CHADEMA lakini pia kuhakikisha kamati muhimu za bunge zinaenda kwa wapambe wao Mrema na Mzee Cheyo. Lakini mkakati wao huo umeingia sumu maana Mrema na Cheyo hawawezi kuficha ukweli kuwa serikali ina matumizi ya hovyo na sasa iko ICU.

  Tukurudi kwenye huu uchaguzi wa EALA, madhara yake ni makubwa mno kwa sababu wabunge wanaoenda kwenye hili bunge wanatakiwa wasimamie maslahi ya Tanzania. Lakini nikiangalia orodha ya wagombea wa CCM sioni mtu wa kutetea Tanzania. Tunatakiwa tuwe na watu wa aina ya John Mnyika, watu wanaosoma mikataba neno kwa neno, lakini mtu kama Angella Kizigha anaweza kusoma hata ukurasa mmoja? Ana uwezo wa kuchambua mikataba iliyojaa 'hila'? Kwa nini Makinda na wabunge wa ccm wanataka kupeleka watu wachovu kwenye bunge lenye wasomi? CCM na Makinda wake wana nia gani na Tanzania?

  Nakubaliana na wale wanaopendekeza CHADEMA wasishiriki kwenye uchaguzi huu hadi pale taratibu zote zitakapokuwa sawa.
   
 20. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nderingosha,

  Si kwamba nimekuja kutoa malalamiko haya mwishoni, mara ya kwanza kuwasilisha suala hili bungeni ni kupitia mchango wangu wakati wa bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki tarehe 19 Agosti 2011 nanukuu:
  "kuhusu Bunge la Afrika Mashariki, Wizara ishawishi mabadiliko ya
  kimkataba ili Wabunge wake wachaguliwe na wananchi moja kwa moja. Hii itachangia katika
  mtangamano na ushiriki wa umma. Katika kipindi hiki cha mpito, kanuni za Bunge za uchaguzi wa
  wawakilishi wa Afrika Mashariki zirekebishwe kushughulika changamoto zilizotokea 2006"

  Baada ya kuona Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na bunge hawakuchukua hatua kwa wakati kufuatia michango mingine ambayo niliitoa kuhusu suala hili tarehe 8 Februari 2012 nikaandika barua rasmi ya kutaka marekebisho/mabadiliko ya kanuni husika; wakati huo tarehe ya uteuzi bado ilikuwa haijatangazwa.

  Baada ya kuona barua yangu hiyo haikujibiwa wakati wa Mkutano wa sita wa bunge ambapo ndio ilikuwa wasaa muafaka wa kufanya marekebisho nilitoa tamko kwa umma mwezi Februari: JOHN MNYIKA: Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge wa EAC zirekebishwe na vyombo mbalimbali vilinukuu.

  Serikali na Bunge hawakujibu kwa wakati wala kufanya marekebisho husika na badala yake wakatangaza ratiba ya uteuzi wa wagombea hali ambayo ilinifanya niwaandikie barua na pia kutoa kauli kwa umma:JOHN MNYIKA: Turekebishe kwanza kanuni ndipo tufanye Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki!

  Hivyo, maelezo niliyotoa sasa ni ya mwisho; iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa tutawajulisha tutatumia njia gani kubwa zaidi ya kudai haki husika.

  JJ

   
Loading...