chamilo nicolous
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 1,991
- 1,364
-Wengi wao ni vibaraka wa Wakurugenzi na Maafisa Elimu (DEO);Wametumwa
--Wakuu wa shule, Waratibu Elimu Kata (MEK) hawafai kuchaguliwa
Siku na Tarehe ya kufanya uchaguzi wa kupata viongozi wa Chama Cha Walimu (CWT) utatangazwa muda wowote, hii ikiwa ni baada ya tarehe ya awali kuhairishwa kufuatia tishio la ugojwa wa CORONA. Poleni kwa usumbufu uliojitieza.
Wapiga kura (Walimu wawakilishi wa kila shule) kuweni makini sana na aina ya Walimu waliojitokeza kugombea nafasi ndani ya chama.Miongoni mwa Walimu waliojitokeza baadhi yao ni Wakuu wa shule na Waratibu Elimu Kata (MEK), na hawa wanaonekana wanahushawishi wa kifedha kwa sababu ya posho ya madaraka, hivyo elfu kumi, kumi kwao sio shida.
NIWAKUMBUSHE WALIMU: Miongoni mwa watu wanaofanya kazi ya ualimu kuwa ngumu ni wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata. Hii inanipa kigugumizi , kundi hili la viongozi wanaotaka tena uongozi watawatetea vipi walimu ikiwa migogoro mingi ya walimu inatengenezwa na Wakuu wa shule na Waratibu Elimu Kata? Walimu mlioko mashuleni mnalijua hili. Walimu wengi wanaohoji masuala ya msingi kama vile mapato na matumizi ya shule, wakuu wa shule huwajengea hoja kuwa ni walimu wakorofi na wasumbufu, na wanaanza kuwaandikia barua mbaya za kuwachafua.
LAKINI: Wakuu wa shule na Waratibu Elimu Kata (MEK), kwa sababu ya posho ya madaraka huwa mnajisahau kuwa na ninyi ni walimu kama walivyo walimu wengine. Mnabadilika kuwa vibaraka wa Wakurugenzi na Maafisa Elimu (DEO). Mnadiliki muda mwingine kutoa maneno ya shombo kwa walimu wenzenu wanapotoa madai ya msingi, mara nyingine mnaficha barua za walimu ili madai yao yasiwafikie waajiri.
UTAKUBALIANA NA MIMI: Ili uwe mkuu wa shule au Waratibu Elimu Kata (MEK) lazima uwe na mahusiano ya karibu na Mkurugenzi na Afisa Elimu (DEO) wakupeleka taarifa za walimu wengine, kujipendekeza(Kibaraka). Mkurugenzi anasimama kama Mwajiri, kwa Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata (MEK) mwajiri (Mkurugenzi na Afisa Elimu (DEO))wananafasi kubwa kuliko walimu.Je katika hali ya kawaida mtadhubutu kuwahoji bila kupepesa macho?
Chamilo Nicolaus nasema ili chama kirudi wenye misingi kama inavyoainishwa katika Katiba ya Chama Toleo la Sita la mwaka 2014: Sehemu ya I Wapiga kura (Walimu wawakilishi wa kila shule) kuweni makini sana na aina ya Walimu waliojitokeza kugombea, Vinginevyo tutabaki kukiona chama kisicho na muelekeo.