Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,754
Siku kama 2 zilizopita nilimsikia Profesa huyu akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC.Katika mahojiano hayo Profesa SAFARI alitangaza nia yake ya kutaka kugombea Uenyekiti wa Taifa Chama cha Wananchi(CUF)..Katika maelezo yake alisema kwamba lengo hasa la kugombe ni kutaka kurudisha uhai wa CUF ambacho(kwa mujibu wa maelezo yake) ni kama kimepoteza umaarufu na kwamba kinahitaji mabadiliko ya uongozi ngazi ya Taifa kwani uongozi wa sasa umekaa muda mrefu na haujaleta mabadiliko yoyote(alizungumzia suala la CUF kutokuwa na mbunge hata mmoja wa kuchaguliwa kutoka Tanzania bara),pia alizungumzia suala la mikutano ya CUF kutokuwa na mahudhurio ya kuridhisha kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo alisema kwamba sasa hivi mpaka wanachama waambiwe kuwa kutakuwa na Pilau ndio mahudhurio kidogo yanakuwa ya kuridhisha...Binafsi namfahamu Profesa SAFARI kama Mwanasheria maarufu na mtaalamu mahiri wa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili...Swali,,Je kwa wanaomfahamu Profesa huyu,ana uzoefu gani katika mambo ya kisiasa???,anaweza kuvaa viatu vya Profesa Lipumba???,hivi uchaguzi mkuu wa CUF unafanyika lini???....Mkuu Mzee Mwanakijiji ninaomba kama inawezekana ufanye mahojiano na Profesa huyu na kuyaweka hapa maana kwa jinsi nilivyomsikia ana uchungu sana na jinsi CUF ilivyopoteza umaarufu(kwa mtizamo wake)..Naomba kuwasilisha wakuu...Mbarikiwe sana
Last edited by a moderator: