Uchaguzi ccm vituko,apata ajali akiwa na fedha za rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi ccm vituko,apata ajali akiwa na fedha za rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WABHEJASANA, Oct 2, 2012.

 1. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wadau habarini na Alasiri?

  Habari za uhakika nilizonazo ni kwamba asubuhi ya leo majira ya saa 2 kuna kijana mmoja (jina nalihifadhi kwa sasa)amepata ajali katika kijiji kimoja kinaitwa Ikina katika kata ya Bukoli wilayani Geita,akiwa amebeba fedha taslimu shilingi milioni 50.

  Taarifa za uhakika nilizo nazo ni kwamba fedha hizi alikuwa akipelekewa mgombea mmoja (Jina tunalihifadhi) ambaye anawania nafasi ya UNEC kwa ajili ya shughuli za uchaguzi ambao unaendelea hivi sasa katika UKUMBI WA shule ya sekondari ya Geita(GESECO).

  Habari kutoka katika eneo la tukuio zinaeleza kuwa baada ya kijana huyo ambaye ni mdogo wake na mgombea huyo ambaye pia ni Diwani kupata ajali,alinyanyuka baada ya kupata fahamu na kukusanya fedha ambazo wakati huo zilikuwa zimetapakaa chini na kudhani amezimaliza kumbe zingine kiasi cha shilingi milioni 15 zilikuwa zimebaki nje kwenye majani pembezoni mwa barabara.

  Baada ya wasamaria wema kufika katika eneo la tukio kwa lengo la kumuokoa walikutana na noti za shilingi na hivyo badala ya kumuokoa wakaanza kunyang'anyana pesa,kwa hiyo wananzengo wakawa wamefaidi shilingi milioni 15 ambazo zilikuwa zinakwenda kwa wapiga kura.

  Hata hivyo ndugu zake akiwemo na mgombea huyo ambaye kiukeli ni mtu anayenuka noti kwa sababu ni mchimabji mzuri sana wa dhahabu Mkoani geita waliwahi kufika na kumchukua njemba iliyokuwa na pesa na kumkimbiza hospitalini,hivi ninavyotoa taarifa hii amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa matibabu hata hivyo hali yake inaendelea vizuri.

  Ni hayo tu kwa sasa nitaendelea kuwahabarisha kama jamaa hilo ambalo kwa sasa limebakiza shilingi milioni 35 litashinda pamoja na kundi lake.

  Nawasilisha.
   
Loading...