Uchaguzi CCM:Nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM moto

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,886
Posted Date::10/31/2007
Uchaguzi CCM:Nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM moto
*Ngeze, Kimiti wapewa nafasi kubwa

*Malecela, Lowassa, Sumaye nao wamo

* Kiti cha Katibu Mkuu pia kitendawili

* Mwambi, Nchimbi, Kinana huenda wakakikwaa


Na Waandishi Wetu, Dodoma

WAKATI Manispaa ya Dodoma na vitongoji vyake imeanza kuchangamka na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kubandika matangazo kwenye magari kwa ajili ya kuomba kura, mazungumzo yanayotawala katika maeneo kadhaa mjini humo ni kuhusu safu mpya ya uongozi wa chama hicho ngazi ya taifa, hasa nafasi ya Makamu Mwenytekiti.

Nje ya Ukumbi wa Bunge, wagombea wamekuwa wakipigana vikumbo kila mmoja akijitahidi

kusambaza kipeperushi chenye wasifu wake na kujaribu kuwakumbusha wabunge ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu, kuwa waliwahi kukutana.

Huku kampeni hizo zikiendelea, mjadala ambao umetawala vinywa vya wabunge na makada wengine wa chama hicho ni juu ya safu mpya ya uongozi inayotarajiwa kutangazwa baada ya Mkutano Mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika mjini hapa mwishoni mwa wiki.

Habari kutoka ndani ya viongozi waandamizi wa CCM zinasema kwamba kuna mabadiliko makubwa yatatangazwa mara baada ya mkutano wa chama hicho kuchagua wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC)

Nafasi kubwa na nyeti zinazopigiwa chepuo zaidi ni zile za Makamu Mwenyekiti (Bara) inayoshikiliwa na John John Samwel Malecela na Katibu Mkuu inayoshikiliwa na Yusuf Makamba.

Watu wanaotajwatajwa na kupewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kushika umakamu ni mbunge wa zamani wa Ngara na ambaye pia ni mwenyekiti mstaafu wa CCM, Mkoa wa Kagera, Pius Bakengesa Ngeze, Mbunge wa Sumbawanga, Paul Kimiti, Yussuf Makamba, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Makamu mwenyekiti wa sasa John Malecela.

Aidha, kinyang'anyiro kikubwa ni katika wadhifa wa ukatibu mkuu, nafasi kubwa ikitolewa kwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Kapteni Jaka Mwambi na Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CCM.

Pia kuna habari kuwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdulrahman Kinana naye anaweza kupewa nafasi ya ukatibu kwa kuwa ni mtu makini na ambayo ana uwezo mkubwa wa kuandaa mikakati ya kujenga chama.

Kinana ana uzoefu katika siasa, kwani katika Uchaguzi Mkuu mwaka 1995, alikuwa kampeni meneja wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na ameendelea kushauri mambo mengi katika chama siku za hivi karibuni.

Pia Chama kimekuwa kikimtumia kutembelea katika maeneo kadhaa kusuluhisha migogoro ambayo imetokana na makovu ya Uchaguzi Mkuu wa 2005.

Katika uchaguzi huu, Ngeze ambaye ameandika vitabu vingi hasa kuhusu masuala ya kilimo aliamua kung?atuka, ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo. Mwaka 1995, aling?atuka nafasi hiyo na kwenda kugombea ubunge wilayani Ngara, ingawa sheria ilikuwa haimbani kufanya hivyo.

Mwaka 2000, aliamua kuachana na ubunge na uchaguzi wa chama mwaka 2002, aliwania tena uenyekiti wa CCM Mkoa na kushinda. Wakati huo kulikuwa na mchafuko kutokana na aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa huo, Anatoly Amani, kukumbwa na kashfa ya kunyang?anywa uraia.

Ngeze inaelezwa kuwa ni mwanamtandao, kundi lililopo ndani ya CCM ambalo ndilo lililomsaidia Rais Jakaya Kikwete kuteuliwa na chama kugombea urais. Pia ni miongoni mwa viongozi wachache wa chama hicho waliotangaza hadharani kumuunga mkono.

Kimiti, ambaye ni mbunge wa siku nyingi, aliwahi pia kushika ukuu wa mkoa katika mikoa mbalimbali. Anadaiwa kuwa msikivu na kupenda kupata ushauri kutoka kwa wengine.

Pia, mwanasiasa huyu ni miongoni mwa wabunge ambao wana uhusiano mzuri wa watu wa rika zote, yaani vijana na wazee.

Mtu mwingine anayetajwa kushika nafasi hiyo ni Makamba, anayeshikilia wadhifa wa Katibu Mkuu, wadadisi wa masuala ya siasa wanasema hatua ya kutaka kuhamishiwa kwenye umakamu imetokana na kuonekana mtu wa majukwani zaidi.

Katibu Mkuu wa CCM, ndiye hasa Mtendaji Mkuu wa chama, lakini inadaiwa nafasi hiyo imepwaya baada ya Makamba kuonekana zaidi akizunguka nchini kuendesha mikutano ya hadhara, kazi ambazo zinatakiwa kufanywa na Mwenyekiti, Makamu wake na Katibu Mwenezi.

Makamba aliwahi kuwa Mkuu wa wilaya na mikoa mbalimbali nchini, mara nyingi imekuwa vigumu kupata wasifu wake tofauti na viongozi wengine. Pia kwa sasa ni Mbunge wa kuteuliwa katika nafasi 10 za Rais.

Waziri Mkuu, Lowassa pi ni miongoni mwa watu wanaofikiriwa kushika nafasi hiyo hasa ikizingatiwa ni Mtendaji Mkuu wa serikali, hivyo anaweza kuunganisha chama na serikali katika kufanikisha utekelezaji wa Ilaani ya CCM.

Hata hivyo, nafasi nyingine inatolewa kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kwa kile kinachoelezwa kuwa Kikwete atapenda kuonyesha kuwa hana kinyongo na amedhamiria kuvunja makundi ndani ya chama.

Sumaye, anapewa nafasi hiyo kwa sababu hakuwa kwenye kundi la mtandao na ni mmoja miongoni mwa viongozi waliomtoa jasho Rais Kikwete kwenye kinyang?anyiro cha urais.

Malecela anapewa nafasi finyu, ingawa amekuwa hapendi kuzungumzia kama atakubali kuendelea iwapo Rais Kikwete atamteua, lakini sio mtu wa kumdharau katika mbio hizo.

Kuhusu nafasi ya Katibu Mkuu, alama nyingi zinatolewa kwa Kapteni Mwambi ambaye katika kipindi kifupi ameonyesha uwezo mkubwa wa utendaji.

Kapteni Mwambi ni kada wa chama hicho na amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Tanga na Iringa kabla ya kuteuliwa kushika nafasi ya Naibu Katibu

Mkuu. Mbali na utendaji wake pia ni rafiki wa Rais Kikwete kutoka sekondari, Chuo Kikuu hadi kukitumikia chama na serikali.

Mwingine anayepewa nafasi hiyo ni Dk Nchimbi, ambaye hakugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, lakini tetesi zinadai kuwa atateuliwa na mwenyekiti kwenye nafasi zake 10, ili kumwezesha kushika wadhifa huo au kujaza nafasi ya Kapteni Mwambi.

Mkutano Mkuu wa CCM utafanyika mjini hapa kuanzia Jumamosi hadi Jumapili ijayo na mji ukiwa unapambwa na kuwekwa taa za barabarani.

Katika hatua nyingine, wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wamelalamikia posho ndogo wanayopewa katika kuhudumia Mkutano Mkuu huo wakisema kuwa posho ya Sh60,000 waliyoahidiwa ilikuwa ni kiwango cha miaka mingi iliyopita.

Vijana hao wamepania kujadili suala hilo na Katibu Mkuu wa CCM, Makamba ili kujua kama ni kweli wanatakiwa kulipwa kiasi hicho mwaka huu au la.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao walisema baada ya kuambiwa kuwa watalipwa fedha hizo juzi waliitwa na Katibu wa Vijana wa Mkoa, Neema Adam na kupewa Sh 30,000 na kuambiwa kuwa watapewa tena Sh30,000.

Walisema kuwa walishangaa kwa nini malipo yalifanyikia nje ya ofisi huku mlipaji alikuwa ndani ya teksi.

Adam alisema vijana hao hawatakiwi kulalamika kwani kanuni za umoja huo zinawaelekeza kuwa kazi zao ni za kujitolea siku zote kwa ajili ya kukijenga chama.

"Chochote mtakachopewa ni bora mkapokea, hivyo sioni kwa nini mlalamike wakati ninyi wenyewe mnajua fika kuwa kanuni ya vijana inasema kuwa kazi zenu ni kazi za kujitolea na kwamba hazina malipo yoyote," alisema Neema.

Miongoni mwa kazi walizofanya vijana hao ni pamoja na ulinzi katika ukumbi wa Kizota, kufua mashuka, kupanga viti na usafi wa maeneo yote yatakayofikiwa na wajumbe wa mkutano huo utakafanyika Novemba 3 na 4, mwaka huu.
 
Nashauri makamu mwenyekiti apewe Ngwilizi ili viongozi wanne wa juu wa ccm wawe waislam ili mchambuzi aliyekuwa anataka kulazimisha kuwa rais ajaye lazima awe mkristo akome ubishi!
 
i dont think it realy matters, ccm wote sawa.

atakaekuja hakutokuwa na mabadiliko ya maana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom