Uchaguzi CCM moto: Vigogo wawahenyesha vijana, wengi warudi, masha, mwakalebela waingizwa kundini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi CCM moto: Vigogo wawahenyesha vijana, wengi warudi, masha, mwakalebela waingizwa kundini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, 29 September 2012
  VIGOGO WAWAHENYESHA VIJANA, WENGI WARUDI, MASHA, MWAKALEBELA WAINGIZWA KUNDINI


  Waandishi Wetu Dar na mikoani

  KINYANG'ANYIRO cha kuwania nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinazidi kupamba moto huku matokeo yakionyesha kuwa vigogo wa chama hicho wameibuka kidedea.

  Katika uchaguzi huo ulioanza juzi katika wilaya kadhaa nchini, watu maarufu ndani ya chama hicho wakiwamo waliokosa ubunge katika uchaguzi uliopita waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali wameshinda.

  Uchaguzi huu unachukuliwa na chama hicho kama sehemu ya kupanga safu ya uongozi ambayo itatumiwa na chama hicho kutetea kuendelea kupata ridhaa ya kuongoza nchi.

  Rais Jakaya Kikwete wakati akifungua kikao cha Halmashuari Kuu (Nec) mjini Dodoma hivi karibuni alisema kuwa wameamua kupitisha majina ya vijana wengi ili wapate timu ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Iringa Mjini
  NEC: Katika nafasi hiyo Mahamoud Madenge alishinda kwa kupata kura 281, huku akiwabwaga Vitus Mushi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Enock Ugulumo na Michael Mlowe.

  Nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa: Katika nafasi hiyo ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela aliibuka kidedea.

  Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa CCM Iringa mjini, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Daudi Yasin aliwataja wengine walioshinda nafasi hiyo inayohitaji wajumbe watano kuwa ni Salim Abri (Asas) Diwani wa Viti Maalumu, Agusta Mtemi, Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi na Fatuma Ngole.

  Mwenyekiti: Mwenyekiti wa zamani wa CCM Wilaya Iringa Mjini, Abeid Kiponza aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake huku akimshinda mpinzani wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Soka Mkoa wa Iringa, Eliud Mvela.

  Aliwataja wajumbe wawili wa halmashauri kuu kundi la wazazi kuwa ni Alli Mbaya na Shadrack Mkusa.

  Walioshinda nafasi hiyo kundi la wanawake ni Nikolina Lulandala ambaye ni Diwani wa Kata ya Gangilonga, Ashura Jongo na Halima Msanya.

  Upande wa vijana walioshinda ni Ally Simba, Salum Kaita, Mwaija Mwinyikayoka na Crala Shirima.

  Kwa upande wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa, wagombea wawili ambao ni Zainab Kufakunoga na Chiku Masanja ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanawake, Iringa mjini walipita bila kupingwa.

  Songea Vijijini

  Nec: Mwanasheria wa CCM makao makuu Dodoma, Glorius Luoga alishinda nafasi ya Ujumbe wa Nec katika Wilaya ya Songea Vijijini.

  Mwenyekiti: Akitangaza matokeo hayo jana Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Mwenyekiti wa UWT Mkoa Ruvuma, Mariam Yusuph alisema nafasi ya Mwenyekiti imechukuliwa na Nelly Due.

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa: Aliwataja walioshinda nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa ni Joseph Muhagama, Vastus Mfikwa, Athon Kantala,Celina Kayombo na Rajab Mtiula.

  Songea Mjini
  Nec: Kwa upande wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Msimamizi wa Uchaguzi huo, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho alimtangaza Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mshindi wa Mjumbe wa Nec.

  Mwenyekiti: Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya imechukuliwa na Gerod Muhenga.

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa: Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ni Anusiatha Ngatunga, Andrew Chatwanga , Charles Muhagama, Consolatha Kilowoko na Mathias Nyoni.

  Nyamagana
  Nec: Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ameibuka kidedea akiwashinda wapinzani wake, Biku Kotecha na James Bwire katika uchaguzi wa mjumbe wa Nec baada ya kuwashinda washindani wake.

  Mwenyekiti: Kada wa siku nyingi wa CCM, Raphael Shilatu ameshinda nafasi hiyo akiwashinda washindani wake, Yahya Nyaonge, Joseph Bupamba na Mashaka Kaguna.

  Ilemela
  Nec: Nafasi ya Ujumbe wa Nec aliyechaguliwa ni Israel Mtambalike akiwashinda washindani wenzake, Nashon Kennedy, Mafuru Eliazar na Ahnes Kingu.

  Mwenyekiti: Katika uchaguzi wa mwenyekiti, Nelson Mesha aliibuka kidedea akiwashinda wenzake.

  Morogoro Mjini
  Nec: Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameibuka mshindi wa nafasi hiyo.

  Mwenyekiti: Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Fikiri Juma ametetea chama hicho baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana.

  Mjumbe afa katika ajali Chunya
  Uchaguzi wa CCM, Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya umeingia dosari baada ya wajumbe wa mkutano mkuu, kupata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja, Isaya Nchimbi (45), ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha Tawi la Madimbwini Kata ya Mamba na wengine 92 kujeruhiwa.

  Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinadai kuwa ajali hiyo ilitokea jana, saa 2:30 asubuhi katika Kata ya Matundasi , baada ya dereva wa gari hilo aina ya Fuso, kudaiwa kupokea simu iliyokuwa ikiita mfukoni, huku gari hilo likiwa kwenye kona hivyo kumshinda na kupoteza mwelekeo na baadaye kupinduka.

  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya, Dk Heny Mwansasu, amethibitisha kutokea majeruhi wa ajali hiyo ambayo imesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 92 kujeruhiwa , ambapo walifikishwa hospitalini hapo saa 4 asubuhi.

  Dk Mwansasu alisema kati ya majeruhi hao, 11 hali zao ni mbaya na 84 walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kwa kuwa wengi wao walipata mshtuko na wengine majeraha madogomadogo.

  Joyce Joliga, Songea, Clement Sanga, Iringa, Moshi Mathias, Chunya, Sheila Sheza, Mwanza, Juma Mtanda, Morogoro.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Oh Lau Masha... Bado hana NYUMBA MWANZA... Kapita bila Matatizo...
   
 3. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Napita tu!
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama mimi vile.
   
 5. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,369
  Likes Received: 8,443
  Trophy Points: 280
  Mbona siwaelewi hawa
   
 6. Ayoub Idd

  Ayoub Idd Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nipo mbio,Nitarudi baadae
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hiyo ajali ya wajumbe wa ccm huko chunya.
  Mtu 1 kafa na 92 kujeruhiwa..... Walikuwa wamepanda air bus au semi trailer? Watu 93??
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Baada ya kushindwa vibaya katika ubunge aliuza nyumba yake nadhani ni hasira na aibu ya kubwagwa na Wenje.

  Btw naambiwa amemwaga mpunga wa kufa mtu. James Bwire ndiye wanaccm wengi walikuwa wanamhitaji kwani wanamuandaa kukabiliana na Wenje hapo 2015!
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu umesahau mambo ya hovyo yanayofanyika nchi hii. Serikali ya magamba imepiga marufuku watu kusafirishwa kwa mafuso lakini bado ccm ndio inaendeleza utamaduni wa kusafirisha watu kwa mafuso.
  Meli ya watu 500 inabeba watu 1200.
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Ya ngoswe....hii ndo thread inayomhusu kamanda Ritz 100%
   
 11. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Chaguzi za Nyamagana na Ilemela zilitawaliwa na rushwa ya waziwazi mpaka ni aibu kwa chama. Hawa CCM sio wa kuwapa nchi tena kama tunataka kutokomeza rushwa nchi hii. Sijui watakuja na wimbo gani safari hii
   
 12. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kweli sura nyingi za vijana wapya zimepita kwenye chaguzi, nimeamini km si fisadi huna chako ccm,hongera chama cha kisanii
   
 13. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Totally confused
   
 14. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwakalebela karudi kapuni sio? Hongera zake.
   
 15. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hoja ni matokeo. Mbona hatujadili watu wanaopora wake za wenzao? Tunajua sehemu husika ya kumchana.
   
 16. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utaelewa polepole.
   
 17. Mmasihiya

  Mmasihiya JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 368
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Unatuletea usumbufu tunaotumia simu, unaquote uzi wote kwa ajili ya kuandika maneno sita yasiyo na uzito?
   
 18. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,885
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 180
  napita tu...salama lakini?
   
 19. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nyinyiemu oyeeeeeeeeeeeeee............!?
   
 20. UPIU

  UPIU JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 602
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani mwanza lazima agombee Wenje. Au ndio mnapanga kuminya democrasia
   
Loading...