UCHAGUZI CCM; Mgogoro wafukuta, ni ule wa jumuiya ya Wazazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UCHAGUZI CCM; Mgogoro wafukuta, ni ule wa jumuiya ya Wazazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, May 7, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Na Mwandishi Wetu

  UCHAGUZI wa viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tawi la Vigaeni, Kata ya Ndugumbi Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, unafukuta kutokana na kudaiwa kuwa na mchezo mchafu.
  Uchaguzi huo bado haujajulikana utafanyika lini, ingawa zoezi la urudishwaji wa fomu za wagombea ulishakamalika tangu Jumapili iliyopita.


  Baadhi ya wanachama wa jumuiya hiyo, wamesema zoezi la uchaguzi wa viongozi wao unaonekana kuwa katika zengwe kutokana na kurudishwa kwa majina ya wagombea.
  Wanachama hao walidai kuwa kurudishwa kwa fomu ya mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Tawi la Vigaeni (jina linahifadhiwa) kunatokana na kutakiwa kuwepo kwa majina ya 'wateule' wao.
  "Unajua kuwa kuna mambo ambayo hata hatuyaelewi kabisa, kwa mfano jina la mgombea wa nafasi ya mwenyekiti limetakiwa kurudi kisa liko moja, na mgombea hawezi kuwa peke yake," alisema mmoja wa wanachama hao.


  Wakizungumza kwa nyakatio tofauti, wanachama wa tawi hilo wamedai kuwa kuwepo kwa tofauti ya jina moja kuondolewa, huku nafasi ya katibu ikiwa na mgombea mmoja, sambamba na nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu kata.
  lilipowasiliana na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Tawi la Vigaeni, lilijibiwa kuwa katibu huyo hayupo kazini kutokana na kusumbuliwa na maradhi.


  Mmoja wa wafanyakazi wa ofisi hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Shida, alisema yeye si msemaji, na kumtaka mwandishi kuwasiliana na katibu, ambaye kwa wakati huo alidai yuko nyumbani kwake na anaumwa.
  Tawi hilo linadaiwa kufukuta kutokana na baadhi wa wagombea kuwekewa kauzibe kwa vigezo vya kutokuwa wakazi, kitu ambacho kinavumishwa ikidai kuna mbinu kwa baadhi ya watu kutakiwa kushika baadhi ya nyadhifa.
  Hata hivyo, wagombea wote wa nafasi tofauti walizoomba wamefanyiwa usaili jana, huku nafasi ya mwenyekiti ikitakiwa kutafutiwa mpinzani, baada ya awali kuwasilishwa jina moja hadi siku ya mwisho ya kurudisha fomu iliyokuwa Mei 6.

  SOSI; Fullshangwe!!

   
 2. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  waache wafu wazikane
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Hivi bado kuna binadamu wenye akili timamu wanaogombea Uongozi katika chama ambacho kimeshakufa!!
   
 4. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45

  Tai wanagombea Mzoga, ukiisha huwaoni hapo tena.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Kiganyi,
  Hivi hiki chama bado kipo huko? Mbona huku kilishazikwa siku nyingi? Na kama wapo watakuwa wanajificha kufanya shughuli zao. yaani watakuwanafanya uchaguzi kwa siri, kama vile wanywaji wa gongo wanavyokunywa pombe kwa siri.
   
 6. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu
  Hiki chama kimeshakuwa mzoga hao wanaogombana hapo ni TAI tu, kama alivyosema jamaa hapo juu!!

  BTW, Dr. Martin Luther King's Final Message: "Poverty is a civil rights battle!'

  Tutapambana na magamba hadi kieleweke!!
   
 7. M

  Mwanandani Senior Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tulikipenda ila Mungu kakipenda zaidi.
   
Loading...