Uchaguzi bila ya katiba mpya ni kujitafutia mauti bila sababu

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Kiongozi wa sasa ni katili kuliko yeyote aliyewahi kutokea kwenye ramani ya nchi yetu. Sio tu kwamba haheshimu katiba bali anaibaka iliyopo.

Haya yanatokea kwasababu katiba ya sasa inampa nguvu kubwa Mkuu wa nchi na hivyo akitokea anayeweza kuitumia vibaya kama wa sasa matokeo ndio yanakuwa hivi.

Chaguzi ndogo zilizopita na zinazoendelea hivi sasa ni vielelezo vya wazi kuwa chaguzi zimekuwa ni za dhuluma, uonevu, mauji, utekaji, kesi za kubambikizwa, uzushi wa kutafutiwa uraia na kila aina ya madhila - kufilisiwa, kuwekwa ndani na matokeo kubadilishwa hadharani huku polisi wakibadili masunduku ya kura hadharani kwa mitutu ya bunduki.

Kauli za kibabe, na kila aina ghasia.
Haya yote yanatokea huku mahakama zikiwa mfukoni mwa mwenye ikulu -kesi zinaamuliwa kwa jinsi apendavyo - hakuna uhuru hakuna haki.

Nchi inaendeshwa kwa kauli -

Ni heri tufe na kuvunjwa miguu , tufungwe tukiwa barabarani kudai katiba mpya -Rasimu original ya Warioba usiku na mchana bila kuchoka - Tuachane na chaguzi za mauji na uonevu - Tuje na katiba ambayo mahakama zitakuwa huru na kila mtumishi au mteule wa Rais pamoja na raisi mwenyewe watakuwa subject kushtakiwa kwa makosa yao wenyewe - ukitumwa na usipofuata sheria ushtakiwe - tunahitaji tume huru ambayo wote wanaofanyakazi tume kuanzia boss wake wawe subject kushtakiwa kwa makosa ya kuharibuchaguzi liwe kama kosa la uhujumu uchumi halina dhamama na hukumu yake yeyote ndogo kabisa iwe sio chini ya miaka 5 bila msamaha wowote na kiwango cha juu miaka 40.

Hizi adhabu zianzie kwa mwenyekiti wa tume mpakakwa wakala - kuwa yeyote anayeshiriki fraud kwenye sanduku la kura akiwa mfanyakazi wa Tume apewe adhabu kali.


Tukiendelea kushiriki chaguzi za damu ni sawa na kusubiri embe chini ya mnazi
 
Bila katiba mpya hamna kitu. Period. Siasa zote ni kazi bure If come uchaguzi katiba ni ile ile.
 
umeongea umemaliza kila kitu.bila katiba mpya nashauri hata upinzani usijaribu kusimamisha mgombea.
 
Hili siyo tatizo la vyama nadhanini kubwa kuliko vyama.wananchi wote walivalie njuga. La sivyo tutaingia vitani! Hakuna aliye salama. Wake up jamani!
 
Back
Top Bottom