UCHAGUZI BAVICHA: John Pambalu aibuka kidedea Uenyekiti. Nusrat Shaaban Hanje ateuliwa kuwa Katibu Mkuu

Emmanuel J. Buyamba

JF-Expert Member
May 24, 2013
1,167
651
Baraza la vijana (Bavicha) la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) linaendelea na uchaguzi wake leo kwa ngazi ya kitaifa.

Muda mfupi uliopita katika ukumbi wa Mlimani City limewapata viongozi wake wakuu ambapo Diwani wa Butimba jijini Mwanza, Bwana John Pambalu ameshinda Uenyekiti kwa kupata kura 150.

Pambalu amefuatiwa na Diwani mwenzake wa kata ya Ari wilayani Babati mkoani Manyara, Bwana Mathayo Gekul aliyepata kura 74.

Katibu wa Chadema jimbo la Kawe jijini DSM, Bi Dorcas Francis amemaliza wa tatu kwa kupata kura 58.

Kwa Makamu Mwenyekiti Tanganyika, Mwanaharakati Bi Moza Ally kashinda kwa kura 136 dhidi ya 72 za Diwani wa Nyansurura huko Serengeti Mkoani Mara, Bwana Francis Garatwa.

Kwa upande wa Zanzibar, Makamu Mwenyekiti ni Bwana Omary Nassor aliyepata kura 110 na kumzidi mpinzani wake, Bi Rukia Mohammed aliyepata kura 94.

Mwanadada Nusrat Shaaban Hanje kutoka Kigamboni DSM amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza hilo.

Bi Nusrat Hanje atasaidiwa na Kaunya Yohana kutoka Bunda Mkoani Mara kama Naibu wake, upande wa Tanganyika.

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ni Haji Abeid Haji.

Katibu Mwenezi amechaguliwa Kamanda Twaha Salim Mwaipaya.

Diwani wa kata ya Kitunda kunako Manispaa ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Bi Nice Gisunte amechaguliwa kuwa mhasibu wa Baraza hilo.

Hongereni sana Bavicha.

#IamTheFutureIwant#.NoHateNoFear.UchaguziChadema2019.
 
Baraza la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) upande wa vijana linaendelea na uchaguzi wake leo.

Muda mfupi uliopita limewapata viongozi wake baadhi ambapo Mkt ameshinda John Pambalu kwa kupata kura 150 dhidi ya 70 za Mathayo Gekul na 58 za Dorcas Francis.

Kwa makamu mkt kashinda Moza Ally kwa kura 136 dhidi ya 72 za Francis Garatwa.

Baadae ni uchaguzi wa Katibu mkuu na manaibu wake.

Hongereni sàna Bavicha.
Hongera kwa wote!
 
Baraza la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) upande wa vijana linaendelea na uchaguzi wake leo.

Muda mfupi uliopita limewapata viongozi wake baadhi ambapo Mkt ameshinda John Pambalu kwa kupata kura 150 dhidi ya 70 za Mathayo Gekul na 58 za Dorcas Francis.

Kwa makamu mkt kashinda Moza Ally kwa kura 136 dhidi ya 72 za Francis Garatwa.

Baadae ni uchaguzi wa Katibu mkuu na manaibu wake.

Hongereni sàna Bavicha.
Ilibidi ashinde tu maana Mwenyekiti alirudi usiku toka mwanza ''kuhesabu'' kura.
 
Mwanza kasoma pamba sekondary advance kasoma ihungo sec bukoba
Binafsi namfahamu tangu akiwa mtoto ni kijana mcha Mungu anayeipenda siasa tangu akiwa mtoto
Hata katambi mlimpamba sana ,mwisho wa siku akawapa mkono wa kwaheri
 
Back
Top Bottom