Uchaguzi Arumeru, nahisi utata na tarehe ya Uchaguzi: 01 April

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,138
01 April is "All Fools Day'. Generally speaking, the April Fool's Day is spent trying to get people to believe in falsehoods or otherwise run a "fools" errand or unnecessary action. Some of the most hilarious practical jokes are pranks pulled by worthy sources. Fake news headlines or marketing stunts that got into the headline, many news sites take advantage of All Fools day and create fake news headlines.


Kutokana na dondo hapo juu, na kwa kadri ya kumbukumbu zangu, kila asubuhi ya tarehe 01 April, ambayo wakati mwingine inajulikana kama siku ya wajinga, magazeti ya Tanzania hutoka na vichwa vya habari vyenye utata. Hisia yangu ni kuwa magazeti yatakayochapishwa na kusambazwa siku ya uchaguzi yanaweza kuwakwaza wapiga kura.

Nahofia vichwa vya habari kama: "Uchaguzi wa Arumeru Mashariki Umeahirisha, Usiende Kituoni!"; "Mgombea wa chama ..... Kajitoa, hivyo kamchague ..... pekee!!"; "Mgombea ....kahamia chama ....." etc. Je kuna sheria inayoweza kudhibiti uchapishaji wa vichwa vya habari kama hivi??? Chonde chonde viongozi wa vyama, kuweni chonjo na tarehe hii muwaelimishe kuhusu hili wapiga kura wenu. Nawasilisha!!!!
 
Uchaguzi wa igùnga ulifanyika siku ya kawaida lakn gari la alshabab mmoja likapita mtaani likingaza mgombea wa cdm amejito.Mara hii watasema mgombea wa cdm ameKUFA
 
Back
Top Bottom