Uchaguzi: Amani au haki kwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi: Amani au haki kwanza?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by emalau, Sep 23, 2010.

 1. e

  emalau JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana JF nimekuwa nikiangalia kwenye vyombo vya habari katika kipindi hiki cha uchaguzi, kuanzia wakuu wa vyombo vya usalama wanasistizia amani iwepo kipindi cha uchaguzi, pia nikienda kwenye ibada wachungaji, masheih na mapadri wanaongea hivyo hivyo.

  Viongozi wa chama tawala ndo kabisa wimbo wao "amani na utulivu". Sijaona hata siku moja kiongozi wa yeyote anasistizia haki itendedeke, hili jambo ni la kushangaza, inanipa impression kwamba watu wanataka kulinda amani kwa nguvu.

  Nionavyo mimi amani ni zao la haki, haki ikitendeka na kila mmoja akaona kwaba haki imetendeka amani itakuwa automatic outcome. Katika uchaguzi huu na chaguzi nyinginezo vyombo ambavyo ni potential ya uvunjifu wa amani kwanza ni polisi wanaowapiga raia waondoke kwenda nyumbani ili mchakato ufanyike bila bugudha, pia waalimu ambao ni wahusika wakuu katika chaguzi zetu.

  Kwa hiyo badala ya viogozi particularly wale wa dini kuimba wimbo wa amani nawaasa wabadilishe mashairi waanze kuimba wimbo wa haki na sisi tutakuja na tune mpya.
   
 2. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Emalau;
  Tofautisha kati ya "amani" na "utulivu". Amani watanzania walishaipoteza siku nyingi, wakabakiza utulivu,.., yaani wametulia ila hawana amani, ndiyo kitu hicho wanachajaribu kukirudisha possibly kupitia uchaguzi huu!
   
 3. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  Dr. Slaa amekuja na jambo ambayo ktk bara la Africa sijui kama kuna mwanasiasa amekwiwahi kuliona hili jambo. This is a great concept/ideology. Huwezi ukaubiri amani wakati hakuna haki. Amani itatoka awapi kama hamna haki? Huyu jamaa is a genius. CCM wanahubiri amani amani, lakini wanawanyanyasa wananchi, wanaendekeza rushwa. Kila mahali pa mejaa rusha. Haki inanunuliwa!!!. Je kuna amani tanzania?.

  Dr. Slaa ni zaidi ya mwanasiasa. naweza kusema ni mwalimu wa haki za binadamu and uraia. This guy is more than a mere politician. A great resource/thinker in a poor country like tanzania. Huu jamaa kwangu mie shule yake ipo juu sana. Ndo kina albert Einstein wa Tanzania. Inahitaji kulindwa, ni tunu za taifa.

  Dr. Slaa kwa mchango wake hadi sasa anastahili kutunikiwa degree ya udaktari wa heshima wa falsafa. Zile zilizopewa kina kikwete ni za kifisadi, hamna lolote.

  Tungekua na watu 10 tanzania kama Dr. Slaa basi shida zote zingeisha. Huyu Jamaa ana kichwa, siyo sawa na wanasiasa wengi ambao wana mdomo tuu kama kina kikwete
   
 4. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe mkubwa,nimelijua hilo tangu alipoamua kugombea Urais mwaka jana, hotuba zake hazikuwa na majungu, alikuwa akisema mambo ambayo katika hali ya kaiwada huitaji kuvutwa mkono ili umpigie kura.

  But kutokana na unafaiki wa watanzania na ushabiki wa kisiasa usioangalia manufaa ya Taifa wapo waliombeza na kumuona hana maana.Ukweli ni kwamba hatutaweza kupata mwanasiasa kama huyu kwa miaka mingi ijayo.

  Hata ndani ya CCM wanatamani wangekuwa naye cause wangeshinda uchaguzi kirahisi sana but hayupo huko.I think kwenye taifa hili, kwa maoni yangu binafsi baada ya Mwalimu Nyerere, yeye anafuata.

  If Dr. Slaa contest in the next election and we dont elect him the i will never ever vote in my life.
   
 5. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Habari zenu Wana JF..?

  Its another beutifull day ....Thanks God kwa kutufanya Wazima Wa Afya...

  Mada yangu hapa ni kwamba kwa Takriban Miaka 50 iliyopita Watanzania tumekuwa watu wa kupanda milima na mabonde bila kufika climax ya safari yetu.....Wanafalsafa wanasema "asiyejua aendapo kamwe hawezi potea" mi nakubaliana asilimia 100% na maneno haya kutokana na ukweli kwamba Watanzania tumekuwa tukiumizwa kichwa na Cheap propaganda kwamba Nchi yetu ina Amani na tusiombe kuivuruga Amani tuliyonayo..

  Imefikia hatua viongozi wa Chama Tawala kutumia upeo mdogo wa asilimia kubwa ya Watanzania kwa kuwajaza SUMU kwamba wakithubutu kuingiza Wapinzani kuiongoza Serikali basi AMANI ITATOWEKA... kwa visingizio kuwa Wapinzani Ni wavunjifu wa Amani na kwamba ni watu ambao wameelekeza fikra zao kwenye umwagaji damu pekee.

  Napinga vikali kauli hii na nadiriki
  kusema kwamba kama wapinzani wangekuwa wavunjifu wa Amani basi leo hii wakina SLAA,MBOWE,LISSU,MNYIKA na wengineo mda huu wangekuwa wameshaingia Msituni kutokana na uovu ambao wamekuwa wakifanyiwa na serikali dhalimu isiyo na utu huku ikijifunika kwenye Mwamvuli wa AMANI.

  Hivi kweli mtu unaweza kulala na Njaa bado ukawa na Amani,huna kazi,unaumwa huna uhakika wa matibabu,huna mbele wala nyuma,haya ni mateso.Nasema hivi kwa sababu mpaka sasa kuna Watanzania wamechoka kiasi ambacho wanaomba wasingezaliwa kabisa...leave alone watu wanaojiua aidha kwa kunywa sumu au kujinyonga kutokana na maisha magumu..
  AMANI IPO WAPI?

  HIVI NI NANI ALIYEAMBIWA KUWA AMEKUJA KUURITHI ULIMWENGU?NASHANGAA WATU TUNAOMBA PEPO LAKINI HATUKOTAYARI KUFA...sasa ili iwepo AMANI ni dhahiri kabisa lazima kuwepo na HAKI na USAWA kama hivi vitu havipo kamwe hatuwezi kuipata hiyo AMANI itaendelea kuwa nyimbo ya Chama tawala kuwa defeate wapinzani..

  Nasema hivi tusipothubutu kupambana kwa ajili ya Haki na Usawa hakuna Amani ni uongo tuu..na Kufundishana uoga tuu.....Hao viongozi wanaohubiri Amani wao wenyewe mioyoni mwao hakuna Amani sababu udhalimu wanao tufanyia Watanzania.

  WE DONT NEED NO PEACE UNTILL PEOPLE GET EQUAL RIGHTS & JUSTICE

  Wasalaam,
  Naomba kuwasilisha.
   
 6. T

  Tata JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti kati ya amani na utulivu. Wanachoongelea wanasiasa ni utulivu na wala siyo amani ila wao wanauita amani. Utulivu hata ndani ya magereza unakuwepo.
   
 7. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  A song by Peter Tosh
  "everyone is crying out for peace none of them is crying out for justice
  I don't want no peace
  I need equal rights and justice"
  Kama ni nyumba ( ya amani na utulivu) then msingi wa hii nyumba ni equal rights and justice!
   
 8. M

  Morrison Senior Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Viongozi watawala wanajifanya hamnazo kwa kujisahaulisha ukweli kwamba AMANI NI TUNDA LA HAKI, (Biblia). Huwa ninapata taabu na kuhisi hasira nyingi ninapoona na kusikia pambio za kwaya za watu wa Mungu wanapoungana na watawala waovu katika wimbo huu wa amani badala ya kuimba pambio za kuchagiza haki na usawa ndani ya jamii za kitanzania.
   
 9. E

  Etairo JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakika umenena. Wakati fulani niliwahi kusema-kwa Mtz Amani ni utulivu kwa maana ya watanzania, lkn si haki na usawa.

  Kutokana na ukweli huo ndo maana mTZ yuko tayari alale njaa, akose matibabu, akose elimu stahili, akose ajira stahili, akose kila kitu ambacho kinamsaidia kufikia maisha stahili akabaki na umasikini, maradhi na ujinga akaona bado ana amani (utulivu wa uoga).

  Haiwi amani kama una shida kuliko mafanikio,maji ya kunywa, uhakikia wa chakula na malazi.

  Watoto wa mjini wanasema holla
  yaani hakuna kitu hapo lkn ukaimbishwa wimbo wa mabwanyenye wanaojilimbikizia mali na kusaza amani itatoweka.

  Ni bora itoweke amani ya utulivu wa uoga ili amani ya kweli ije inayotokana na uwepo wa Haki na usawa.

  Hivi havipatikani kwa watu kuwa waoga bali kujitoa mhanga ikibidi wengine wafe ili wanaobaki na wanaokuja waipate amani, haki na Usawa. Je, ni nani wa kuanzisha ufungaji wa paka kengere?
   
 10. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa wale wote ambao wanasema wanataka amani, inabidi pia wahakikishe kunakuwa na hakii sawa katika jamii. Bila hivyo kuwepo, amani ni ndoto.


  [video=youtube_share;1SN7Pko_jCM]http://youtu.be/1SN7Pko_jCM[/video]​
   
 11. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #11
  Aug 25, 2015
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Sasa Kama Mkapa baada ya kutuibia miaka yote ameona ahitimishe kwa kutuita malofa
   
 12. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2015
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Siongezi neno.
   
 13. maganjwa

  maganjwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2015
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 1,629
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  matunda ya haki ni amani na matunda ya amani ni upendo, furaha na matumaini ktk jamii. viongoz wa dini zote tuombee haki itendeke wakati huu wa uchaguzi kwa kuwa haki isipotendeka hakuna amani. mbowe amesema tume wafanyakaz wake wamebadilishwa na wanaofanya kazi ni usalama wa taifa na jeshi kama ni kweli ni kwa maslah ya nani?
   
 14. maganjwa

  maganjwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2015
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 1,629
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  ccm msituletee vita jamani ebu kubalini matakwa ya wananchi acheni izo rafu
   
 15. F

  FUSO JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2015
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  Kwa CCM hilo linawezekana, walishawahi kuuombea hadi UCHUMI itakuwa AMANI.
   
 16. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2015
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,692
  Likes Received: 13,632
  Trophy Points: 280
  Wananchi wanasema kuwa CCM inakubalika kwa asilimia 70 na Magufuli asilimia 62 mpaka 65. Sasa wewe unataka nini?
   
 17. H

  H.T.P JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 1,086
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  Wananchi gani unawazungumzia hapa...maana mi sipo
   
 18. PRINCE CROWN

  PRINCE CROWN JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2015
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 4,491
  Likes Received: 1,537
  Trophy Points: 280
  Wananchi wapi Lizabon? kenya zilipita tafiti 7 zikimwonyesha Raila omolo odinga anaongoza.

  Mwisho wa siku akatangazwa uhuru kenyatta mshindi. Upo? Wanaopiga kura sio kampuni za tafiti, wanaopiga kura ni wananchi, tukutane oct 25.
   
 19. m

  muhindo JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2015
  Joined: Aug 5, 2015
  Messages: 787
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  haki ndio msingi wa amani. Neno amani lisitumike kuficha majambazi wa haki!!!!!
   
 20. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,531
  Trophy Points: 280
  Pole HAKI haipo sababu ishanunuliwa na RUSHWA za pesa,chakula,Tshirt na vitenge.Kumbuka ADUI number moja wa haki ni RUSHWA.
   
Loading...