Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 tunaenda kukamilisha ratiba tu, bingwa yupo

Michael Andrew Jr

JF-Expert Member
Jul 1, 2020
219
665
Wakuu salute!
Jioni ya leo nikiwa maeneo ya Tegeta namanga Dsm, nilipitia pub moja at least kupoza koo kwa 'kabia kamoja' kupoza machungu ya utafutaji. Si unajua ukiumbwa mwanaume...

Kumekuwepo na tambo, mbwembwe na ubishani baina ya upinzani hususani CDM dhidi ya chama dola CCM kuelekea uchaguzi mkuu october 2020. CCM wakitamba kupeta na Upinzani ukiapa kuliangusha 'jabari' .

Binafsi naamini uchaguzi uliisha toka kipindi kile cha kukarabati daftari la kudumu la wapiga kura. Kwa wakati ule vijana wengi walisusa kujiandikisha, wengi wakisema siasa sasa basi, hasa ukizingatia wabunge walivyokua wanaunga mkono juhudi. Wengi wanakumbuka machungu jinsi walivyowapambania 2015, na jinsi usaliti waliokua wanaufanya wa kuunga mkono juhudi.

Wakati vijana wa kimapinduzi wengi wakisusa kujiandikisha, CCM walikua wakihamasisha akina mama na akina bibi kwenda kupanga foleni kujiandikisha. Ni dhahiri walikua wanajua wanachofanya hasa ukizingatia vijana kama machinga, boda boda,wavuvi nk walikiua wazito kwenda kujiandikisha. Ni kama walitengeneza tatizo makusudi, bila shaka ule ulikua ni 'mkakati' mahususi.

Tofauti na wengi tunavyodhani kua uchaguzi unaweza kuendeshwa kibabe ili kuibeba CCM. Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kua wa haki na wazi sana kuliko chaguzi zilizopita... Ila utakua na wapiga kura wachache ambao wengi ni akina mama na wazee ambao ni wakereketwa wa CCM. Upinzani ulizubaa sana katika kuhamasisha watu, na hii ilichangiwa na 'kibano' walichopewa cha kukataza siasa na mikutano, isipokuwa kwa wabunge ndani ya majimbo yao.

Yale mambo ya upinzani kuchukua watu CCM then baadaye wanarud walipotoka yalikua yanaboa sana na kukatisha tamaa... Watu waliona siasa ni kama maigizo!

Wanasema "no research no right to speak" jaribu kuuliza kati ya vijana 10 wangapi wamejiandikisha hapo ulipo... Ni ukweli mchungu lakini lazima usemwe. Kwenye mikakati na figisu CCM they are far better, Upinzani jifunzeni.
Michael Andrew JR
 
Kwa hiyo wewe ulikuwa mratibu wa huo mpango?
Ni hivi hayo yote uliyoyataja hapa yamefanywa na CCM Ili itawale milele mm nakwambia wazi kuwa hivyo vibibi na vibabu havina mpango na CCM kwa sasa utaelewa baada ya Uchaguzi.

Endelea kujifariji kwa sasa majibu halisi utayapata Oct 28
 
Ishu mnapaniki... Mie nimetoa maoni mnaweza chukua au kuacha
 
Subiri kampeni zianze , acha kuandika porojo.
Anacho ongea ni kweli,ata tujaze vipi watu kwenye kampeni ,Kama wengi hawataweza kupiga kura ni kazi bure,Kama vile mziki ukitoka bila ya utaratibu ni kelele,kiukweli wengi haswa vijana hawatakua na sifa ya kupiga kura,fanya reaseach ndogo tu mtaani kwako ,vijana wangapi wana kadi ya kupiga kura?ccm ilijitaidi kuhimiza watu Kuhusu kadi ya mpiga kura,Apo ndo upinzani tunafeli,
 
Acha waukatae lkn .ndio ukweli hata mimi sijaboresha.
Ikumbukwe kwenye uchaguzi wa serkali za mitaa ndipo upinzani ulikanyaga waya wa mashine ya kupumulia.
Kwenye mikutano wataona nyomi kumbe haipigi kura, hiyo itakusifu, kusukuma gari lkn waulizeni ulijiandikisha?
 
Bro you nailed it, watu hawajiulizi kwanini CCM wamelegeza kamba.. upinzani ungefanya kama 2015 kuhamasisha then wangetafuta namna ya kulinda kura zao. Lakini mwaka huu walizembea sana. Saizi ccm wanajua wapi upinzani ulikosea
 
Acha waukatae lkn .ndio ukweli hata mimi sijaboresha.
Ikumbukwe kwenye uchaguzi wa serkali za mitaa ndipo upinzani ulikanyaga waya wa mashine ya kupumulia.
Kwenye mikutano wataona nyomi kumbe haipigi kura, hiyo itakusifu, kusukuma gari lkn waulizeni ulijiandikisha?
Braza ishu kubwa watu hawataki kuukubali ukweli na kujifunza... Ccm always they are good kwenye figisu, upinzani wanahitaji kujifunza
 
Kwa upinzani huu wa Mbowe na Lissu hakuna jipya wanaloweza kufanya, inahitajika vichwa vipya vianze upya, Mbowe na Lissu wakiendelea kuwa ndio image ya CDM , then CDM kitakuwa kama TLP kitazaliwa au kitapanda chama kingine kuchukua nafasi zao maana wananchi wanaopenda upinzani bado wapo.
 
Back
Top Bottom