Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020: Tuambiane Ukweli tu, Tundu Lissu na Maalim Seif hakuna atakayekuwa Rais

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Sisi wengine tutasema ukweli hata kama ni mchungu. Tutasema tu. Hata kama nitabaki peke yangu kuusema ukweli nitasema tu

Tundu Antipas Lissu - hatokuwa Rais wa Tanzania hata iweje. Hawezi apishwa kuwa Rais iwe jua iwe mvua.

Seif Shariff Hamad - hatokuwa Rais wa Zanzibar hata iweje. Hawezi apishwa kuwa Rais iwe jua iwe mvua.

Hao watabaki marais wa mioyo ya watu ila kimwili na kiuhalisia haitatokea. CCM bado ipo sana. Wenye faida ya CCM kuwa madarakani ni wengi na wana nguvu kuliko wachache wasio na faida nayo.

Bernard Membe - huyu hata kumwongelea najisikia uvivu. Hamna kitu kwa huyu huko mbeleni ataomba msamaha atarudi CCM. Kwa sasa mwacheni tu aume ume maneno hata kuongea hajui.Havutii.
 
Hii ni 2020 ndugu,acha ndoto za alinacha.
Ccm inakalishwa kando asubuhi mapema,na nchi mnakabidhi kwa washindi!
Msishupaze shingo kwa ujeuri wa kijinga.
Mungu anawaona.
 
Dawa ya leo ya Mwanza, Bunda na Musoma tu imekufanya upanic hivyo????

Tulieni dawa ziwaingie vizuri, mlishazoea kuweka mamluki kupambana na Ccm eeh??? Sasa Safari hii ni baasi!! Chuma kisicho hata na chembe ya umamluki kinapambana na nyie. Jiandaeni tu kukabidhi nchi na kama hamtaki mtaikabidhi kwa nguvu ya umma mwaka huu.
 
Nani atatilia maanani maneno ya "chizi"
Pamoja na uchizi wako Umekubali kuwa watashinda uchaguzi isipokuwa hawataapishwa
 
Huo ndo ukweli jembe, iwe jua iwe mvua, iwe joto iwe baridi mropokaji lisu na sultan seif hawatakuwa maraisi.
 
Sidhani kama kuna m mtu yupo tayari kuharibu kura yake kwa lisu,

Aliharibu chama cha mawakili tanganyika asipewe nafasi ya kuharibu nchi yetu.
 
Weka akiba ya maneno, kwa kuwa hakuna mwenye kuweza kutambua mambo yatakayomtokea ktk siku ya kesho yake achilia mbali hata dakika moja iliyopo mbele yake. Kwa kuwa sisi sote ni wanadamu, Mola wetu ndiye mwenye kutambua nani ambao watakuwa viongozi wa Taifa letu. Na mapenzi yake yapate kutimizwa.
 
Kama hawajakuelewa, basi tuwaache
Itakuwa ni ujinga na uendawazimu kwa wananchi wa Tanzania kumkabidhi nchi mtu asiye na chembe ya maadili Wala uzarendo kwa nchi yake, kisa eti ni demokrasia!
Nyerere baba yetu alituasa
" Uongozi wa nchi haujaribiwi"
 
Back
Top Bottom