Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020: Sioni hoja za Magufuli na CCM kutushawishi Watanzania tuwachague tena!

RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
963
1,927
Habari zenu wana JF!

Mimi naomba wakereketwa na washabiki wa uongozi wa awamu ya tano watushawishi kwa hoja za msingi kwa nini Magufuli na CCM tuwape kura 2020!

Tunajuwa uwezo wa kujitangazia ushindi wanao, kwa kuwa wao ndiyo wafugaji haliali wa magobore!

Kwa upande wangu nawashawishi Watanzania tusiwachague hawa watu kwa sababu zifuatazo:

1. Uchumi: Hali ya maisha ya watu kifedha ni mbaya kuliko kawaida. Tujiulize tu kila mmoja tangu awamu ya tano ianze, simu unazopokea tu kwa siku, watu wakiomba kusaidiwa pesa zimeongezeka zaidi. Hii ni dalili kuwa hali ya watu kiuchumi siyo nzuri!

2. Biashara nyingi zimedorora au kufa kabisa. Ukipita katika miji mikuɓwa utakuta wachuuzi wamepanga bidhaa mpaka baraɓarani lakini bado wanalalamika kutopata wateja!

3. Wakulima nao hali ni mbaya kuliko kawaida. Mazao hayana wanunuzi na kama wapo yananunuliwa kwa bei ya chini ambayo wakulima hawapati faida bali ni hasara! Kama unabisha waulize wakulima wa korosho!

4. Wavuvi nao hawajaachwa salama! Tingatinga limefanyakazi ambayo si rahisi kusahaulika! Umasikini umewakuta kwa kasi ya dreamliner! Ukibisha waulize walishudia samaki wakipimwa kwa rula wakati taƴari wameshaƙuwa supu!

5. Usalama nalo ni jambo lingine linalonishawishi kutowachagua hawa watu. Siku hizi vibaka mtaani ni wengi sana! Ukipona viɓaka basi wewe utapambana na wasiojulikana.

6. Rushwa nayo imeongezeka badala ya kupungua. Utambiwa mara 1.5T hazijulikani zilipo, mara 2.4T hazionekani mara kuna shimo linaitwa 'vote 20' linameza pesa ɓila kutafuna!

7. Kodi nazo hazihesabiki na wala hazina mpangilio! Wakiamka tu hawa mabwana wakubwa kuwa wauza matembele nao tuwakamue, wanatengeneza vitambulisho visivyo na kichwa wala mkia na kuanza kuwatoza feɗha! Natamani waTz wote tuseme hapana inatosha!

8. Demokrasia na uhuru wa maoni navyo vipo kwenye ncha ya upanga. Ukitaka kuhoji matendo ya serikali inabidi uangalie aliye karibu yako kama unamfahamu au la. Tofauta na hapo utatembelewa na Wasiojulikana. Hofu ni kila mahali.

9. Tanzani ƴa Viwanɗa tuliyohubiriwa haionekani, kumbe uliƙuwa ni ulaghai mtupu! Wajenga viwanda wametokomea kusikojulikana! Tunasubiri viwanda ya umma vilivyomshinda Mwalimu!

10. Wahisani nao amewatibua, ambao walikuwa wanasaidia kwa kiwango kiwa katika maendeleo ya taifa katika nyanja mbalimbali mfano elimu, afƴa nk! Sasa wanawaita mabeberu eti sisi ni 'donor country'! Ngoja tusubiri kipigo cha mbwa mwizi!

11. Huduma za jamii nazo ni hoi! Maji, afya, elimu nk vyote bado ni duni

12. Ajira kwa vijana waliomaliza vyuo hakuna. Hivi ni kipi mtawaeleza WaTz wawaelewe na kuwaunga mkono!?

13. Mishara kwa watumishi wa umma haijaongezeka tangu muingie madarakani! Je huu ni uungwana kweli!?

14. Hata wana CCM wenzenu huku mashinani wanalalamika, vikao mnawaitisha hata soda hawapati! Hivi awamu ya tano faida yenu ni nini!

15. Sasa mvua nazo hazinyeshi sababu Mungu amechukizwa matendo yenu yasiyofaa ya kurudisha maendeleo ƴa watu na taifa nyuma!

16. Chuki na mgawanyiko miongoni mwa wananchi mmeuleta Srikali ya awamu ya tano! Mnasema yapelekwe kwenye madiwani na wabunge wa CCM na si maeneo yote! Ubaguzi ubaguzi!

Kwa haya machache nashawishika kusema, JPM na genge lake si wa kupigiwa kura wajipange kujitangaza kwa nguvu!
 
Watakuambia tunajenga mabarabara, tumenunua madege, tunajenga stiglers gorge, tumejenga fly overs, tumejenga ubungo interchange, tunajenga daraja jipya la salender, nk

Sasa unajiuliza, ujenzi wa hivyo vitu una mahusiano gani na kutowapandisha wafanyakazi madaraja na kuwaongezea mishahara! ambavyo vyote hivyo kimsingi ni haki yao? Mbaya zaidi unawaongezea makato ya bodi ya mikopo kutoka 4% hadi 15%! Ukishawaumiza wafanyakazi maana yake wafanyabiashara na wakulima hawatapona.
 
Nchi imejaa laana hata mvua hazinyeshi,kuwarudisha hawa madhalimu mazulumati ni kutaka kuigeuza nchi kuwa kuzimu,uzuri kila mmoja kaona rangi halisi,wakirudi tu
Kikokotoo kitarudi
Machinga watafukuzwa kama mbwa wameachwa ili wapate kura
Bomoabomoa itarudi kwa kasi ya 10G
Usalama wa RAIA utakuwa shakani tutaishia siku zake zilifika,
Kuongezeka kwa kisasi
Utekaji, viroba
Wasiojulikana wataongezeka
Hali ya maisha itakuwa ngumu mara 20 ya sasa tutakula hadi nguo,
Fedha zetu zitaporwa kwenye mabenk,
Kodi zitaongezwa na mpya kuanzishwa
Kosa ni kurudia kosa,zamu yao kusomesha namba.
 
Wakiona uzi wa hivi ndio wataongeza wanajeshi zaidi ili kuja kupiga raia ambao hawatawachagua. Huku mitandaoni wataongeza watu wa kufuatilia IP zaidi ili kuteka watu. Nakuhakikishia unyama watakaofanyiwa wapinzani 2020 utakuwa sio wa dunia hii. Inabidi tuendelee kuwaandaa wazungu wangalau watoe kauli ya kuwatisha kama kutafanyika unyama basi watasusia bidhaa zetu na kukata misaada zaidi.
 
Watakuambia tunajenga mabarabara, tumenunua madege, tunajenga stiglers gorge, tumejenga fly overs, tumejenga ubungo interchange, tunajenga daraja jipya la salender, nk

Sasa unajiuliza, ujenzi wa hivyo vitu una mahusiano gani na kutowapandisha wafanyakazi madaraja na kuwaongezea mishahara! ambavyo vyote hivyo kimsingi ni haki yao? Mbaya zaidi unawaongezea makato ya bodi ya mikopo kutoka 4% hadi 15%! Ukishawaumiza wafanyakazi maana yake wafanyabiashara na wakulima hawatapona.

Kwa MTU wa kijijini kwake havina tija MTU wa Songea,katavi,Kigoma, Mara, Lindi,IRINGA ananufaika vipi na hayo,hali naye kalipa kodi kuna miradi gani nje ya dar hata nao wafurahie kodi yao?
Tunataka utawala wa Sheria,
Usalama wa kodi zetu,
Usalama wa RAIA na Mali zao
Watu waruhusiwe kuuza mazao nje
Demokrasia watu wawe huru
Wasibomolewe nyumba zao Bila fidia sababu la uzembe wa watendaji wengine
Mikopo ya Chuo Bila ubaguzi
Hatutaki ujamaa ni adui wa maendeleo na haki,watu wawe huru wafanye biashara kwa ushindani.
 
Wakiona uzi wa hivi ndio wataongeza wanajeshi zaidi ili kuja kupiga raia ambao hawatawachagua. Huku mitandaoni wataongeza watu wa kufuatilia IP zaidi ili kuteka watu. Nakuhakikishia unyama watakaofanyiwa wapinzani 2020 utakuwa sio wa dunia hii. Inabidi tuendelee kuwaandaa wazungu wangalau watoe kauli ya kuwatisha kama kutafanyika unyama basi watasusia bidhaa zetu na kukata misaada zaidi.

Mungu amesikia mateso ya wengi. Atatenda kulingana na matakwa ya wengi.
 
Watakuambia tunajenga mabarabara, tumenunua madege, tunajenga stiglers gorge, tumejenga fly overs, tumejenga ubungo interchange, tunajenga daraja jipya la salender, nk

Sasa unajiuliza, ujenzi wa hivyo vitu una mahusiano gani na kutowapandisha wafanyakazi madaraja na kuwaongezea mishahara! ambavyo vyote hivyo kimsingi ni haki yao? Mbaya zaidi unawaongezea makato ya bodi ya mikopo kutoka 4% hadi 15%! Ukishawaumiza wafanyakazi maana yake wafanyabiashara na wakulima hawatapona.

Hima Wafanyakazi msigeuzi midoli!
 
Vyote hivyo viko Dar sisi wa huku Manyovu Kigoma tunafaidikaje na keki ya taifa
 
Million 50 kila kijiji ziko wapi?.....

Kurudi kwa kodi ya kichwa 20000 kwanini??

Kumsafisha fisadi aliyemkataa na kusema mafisadi yamekimbilia upinzani?........

Kumsafisha Rostam fisadi wa siku zote utawaambia nini watu 2020?.......

Ajira ndio bomu hatari kwa serikali yake utawaambia nini wahitimu?.....

Kutumia pesa za umma kuwanunua wapinzani utawaambia nini watu?.....

Only fool can vote to Magufuli na atakuwa Rais wa wajinga akishinda ..........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watakuambia tunajenga mabarabara, tumenunua madege, tunajenga stiglers gorge, tumejenga fly overs, tumejenga ubungo interchange, tunajenga daraja jipya la salender, nk

Sasa unajiuliza, ujenzi wa hivyo vitu una mahusiano gani na kutowapandisha wafanyakazi madaraja na kuwaongezea mishahara! ambavyo vyote hivyo kimsingi ni haki yao? Mbaya zaidi unawaongezea makato ya bodi ya mikopo kutoka 4% hadi 15%! Ukishawaumiza wafanyakazi maana yake wafanyabiashara na wakulima hawatapona.
Kwa hoja hizo ni bora aseme anaijenga DSM pekee.Maana 97 % ya hayo yanafanyika DSM.Kwa hiyo amepata urais aijenge DSM?
 
Back
Top Bottom