Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 na usiri wa Tume yetu juu ya mfumo wa kuchakata kura

Chivundu

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
7,239
5,532
Wanabodi,

Najua wengi wenu mtakuwa mmesahau ule mchezo wa Kenya unaitwa "Kivuitu system".

Pamoja na kwamba mfumo wetu uchaguzi kikatiba na kitume haupo huru bado ni jukumu la wapenda haki na wanamageuzi kuhoji na kujua mbinu za kimfumo kama hizi za kucheza takwimu za kura.

Sijasikia chama chochote kikiibua hii mijadala watu wamejikita kutafuta "wadhamini" na makatibu wa vyama "uwezo mdogo sana"

Mtakumbuka ujio wa Biometric Voter Registration (BVR) na mfumo wake wa utambuzi "Electronic Voter Identification EVID au Polibooks" na mfumo wake wa kuchakata na kutuma kituo kikuu cha kuhesabia kura "Eletronic Results Transmission System RTS".

Mfumo huu ulianza kutumika 2010 na unafanyiwa maboresho na mwaka huu kwa taarifa za "vipepeo" umeboreshwa zaidi na ndio maana unaona "jengo jipya la kura" limejengwa kiufundi na lipo full-equips hapo kwa wagogo. Jengo hilo ndilo litaratibu utaratibu mzima wa kucheza na takwimu chini ya "jaji mteule" na mwisho wa siku sisi tutatangaziwa tuu matokeo jumla jumla na asilimia na wala hatutaweza ku "challenge" matokeo hayo katika mahakama yeyote ile.

Kwa bahati mbaya sana mwaka huu "jaji mteule" wala ofisi yake haijaweka wazi juu ya mfumo upi utatumika katika zoezi hadi kwenye kutuma hizo kura "transmission" kwenda kituo kikuu hapo kwa wagogo.

Haijajulikana kama tutahesabu kwa mkono,au kwa sayansi na kama ni kisayansi vituo vikubwa vitakuwa kikanda au kimkoa na uwazi wake upoje.

Kiufupi haijawekwa wazi japo chama dume wameshajipanga kama chama na wamezindua "data center" yao na kutuaminisha kwamba ni "kituo cha habari zao".

Sijamsikia Katibu yeyote wa chama cha upinzani akizungumzia usiri na sintofahamu ya hili suala hili au hata kufanya press kuleta hamasa na muda unakwendaù. Nawasikia tuu watu wapo zenji na wengine wapo kutafuta wadhamini huku wakilingishiana "nyomi" wanazokutana nazo.

Sijawasikia wanaharakati kushinikiza "jaji mteule" na ofisi yake atoke mafichoni na kuweka haya mambo bayana kwa wadau pawepo na mjadala wa kitaifa, wananchi wapewe elimu na mwamko,ndio kazi ya tume kikatiba kutoa elimu ya mpiga kura na mchakato mzima. Na wana fungu la kufanya hivyo ila mpaka waambiwe na waliowateua ndio bongo ilivyo. Anaemlipa mpiga zumari ndie anaechagua wimbo. Bongo nyoso.

USHAURI KWA WAPINZANI
Kwanza mtoeni mafichoni jaji mteule kwa kumsema sema na anzisheni mjadala wa kitaifa.

Anzeni kuandaa semina za mawakala mapema na kuwajengea uwezo mawakala kuzijua mbinu chafu za hapa na pale mmepaniwa sana walahi.

Anzisheni "data center" na nyie kama ya kwao walioizindua majuzi na nyie mseme ni "kituo cha habari" na mtapatumia kuchakata matokeo yenu toka kwa mawakala wenu kupata uhalisia "reflection" ya mchakato. Sio mje kusema tuu mmeibiwa halafu mkashindwa ku-justify ni aibu kuwa "outsmarted" kiboya boya.

Komalieni sana ishu ya "uangalizi wa kimataifa" hua inaleta aibu kwenye mbinu za hapa na pale chafu. Maana jamaa watataka mfumo uwe wazi itakuwa faida kwenu kiasi flani,kataeni ile dhana ya "mabeberu" ni mteģo ule.

Msiruhusu mfumo wa BVR wala EVID au Polibooks pekee mtapigwa kwenye tallies za kitakwimu. Fanyeni kama Kenya kina Raila walipoona BVR inanajisiwa wakashinikiza kura zihesabiwe kwa mkono.

Uchaguzi ni mchakato na sio afya kuamini mchakato "Trusting the process".

"Kupiga kura sio kazi kazi kulinda kura".

"Mwaka wa tabu huu na JK ni raisi bora kuwahi kutokea bongo hii"

"JK ndiye baba wa demokrasia hutaki unaacha"
 
Msiruhusu mfumo wa BVR wala EVID au Polibooks pekee mtapigwa kwenye tallies za kitakwimu. Fanyeni kama Kenya kina Raila walipoona BVR inanajisiwa wakashinikiza kura zihesabiwe kwa mkono.

Uchaguzi ni mchakato na sio afya kuamini mchakato "Trusting the process".

"Kupiga kura sio kazi kazi kulinda kura".
 
Haijajulikana kama tutahesabu kwa mkono,au kwa sayansi na kama ni kisayansi vituo vikubwa vitakuwa kikanda au kimkoa na uwazi wake upoje.

Kiufupi haijawekwa wazi japo chama dume wameshajipanga kama chama na wamezindua "data center" yao na kutuaminisha kwamba ni "kituo cha habari zao".
Kituo cha bao la mkono.
 
Back
Top Bottom